Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Biashara ya shirika la ndege la Air Tanzania yaimarika


Biashara ya shirika la ndege la AIR Tanzania Company Limited (ATCL) imepanda thamani kwa kipindi cha miaka miwili licha ya kuwa na abiria wachache waliotumia ndege zake kusafiria


Mkurugenzi wa biashara wa ATCL Patrick Ndekana aliambia gazeti la Daily News kwamba biashara za shirika hilo la serikali iliongezeka kutoka asilimia 2.5 mwaka 2016 hadi asilimia 42.6 mwisho wa mwaka jana huku ikiwa na ndege mbili pekee zinazofanya kazi.

Amesema kuwa wana matumaini kwamba biashara hiyo itaimarika zaidi baada ya kununuliwa kwa ndege mpya.

''Mwaka huu biashara yetu itaongezeka hususan baada ya kuwasili kwa ndege ya tatu kubwa aina ya Bombadier Q-400s na baadaye kuwasili kwa Bombadier nyengine mbili za Cs 300s ambazo zitakuwa na viti vingi'', alisema.


Kwa sasa shirika hilo linamiliki ndege tatu aina ya Q-400 katika maeneo 10 tofauti nchini, mbali na kuelekea Comoro.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka jana, shirika hilo limekuwa likisafirisha abiria wachache na kufanya safari chache ikilinganishwa na washindani wao.

ATCL inapanga kuleta ndege hizo mpya kupitia kuongeza safari hususan katika maeneo ya Kaskazini , magharibi kaskazini mashariki.

Ndege hizo za serikali zinapanga kuanzisha safari za kuelekea Bujumbura, Burundi kupitia Kigoma na Entebbe, Uganda kupitia Kilimanjaro.


Bwana Ndekana amesema kuwa kufikia mwisho wa mwaka huu kampuni hiyo itazindua safari nyengine za kuelekea Lusaka, Zambia na Harare, Zimbabwe. "

''Safari hizo mpya za kuelekea Lusaka na Harare zitaanzishwa mwezi Novemba, iwapo kila kitu kitafanyika kwa mpangilio'', alisema.

Kampuni ya Boeing pamoja na shirika la ndege la Tanzania zimethibitisha ununuzi wa ndege moja aina ya 787-8 Dreamliner, yenye thamani ya $224.6 million

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...