Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya AFYA

Tanzania yakiri kuwa na Chikungunya, Dengue

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto nchini Tanzania imekiri kuwepo kwa magonjwa wa homa ya Chikungunya na Dengue katika taifa hilo kubwa kabisa Afrika Mashariki. Akitoa taarifa kwa wadau na waandishi wa habari mapema leo (Juni 25), Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amebainisha kuwa mnamo tarehe 20 Juni wasafiri wanne wa familia moja waliotokea Mombasa, Kenya, walibainika kuwa na ugonjwa huo kwenye kituo cha mpakani cha Holili, mkoani Kiliamanjaro. Awali jumla watu sita walibainika mwezi wa Januari mkoani Tanga kuwa na ugonjwa wa Chikungunya kupitia kwenye kituo cha mpakani cha Horohoro wakitokea pia Mombasa. Wakati huo huo, Tanzania imethibitisha pia kuwepo kwa homa ya Dengue, ambapo hadi sasa watu 226 wamethibitika kuwa na ugonjwa huo katika mkoa wa Dar es Salaam pekee, ambao ni kitovu cha kiuchumi na biashara.  Kwa mara ya kwanza homa ya Dengue iliripotiwa nchini humo mwaka 2010

WHO yatoa tahadhari kuhusu watu kuumwa na nyoka

Mashambulizi ya nyoka yameleta madhara makubwa duniani Nchi wanachama wa mkutano wa shirika la afya duniani wamepitisha azimio la kutambua kuumwa na nyoka kuwa ni suala linalohitaji kupewa kipaumbele katika kulishughulikia. Maelfu ya watu hufa kila mwaka na wengine kuwa walemavu kutokana sumu inayotokana na shambulio la nyoka. WHO inasema athari zinazotokana na kuumwa na nyoka zimeendelea kuwa moja kati ya magonjwa ya kitropiki ambayo hayatiliwi maanani. Kufikiwa makubaliano hayo kwa nchi wanachama wa WHO , kuna nia ya kuhakikisha kuwa kunakuwa na mbinu za kuzuia, kutibu na kukabili mashambulizi ya nyoka. Makundi ya mbalimbali ya wanaharakati wa masuala ya afya yamesifia azimio hilo na kusema kuwa hatua hiyo inafungua milango katika kupunguza vifo na ulemavu duniani kote. Shirika la Afya duniani sasa lina jukumu la kuja na mpango wa pamoja kuimarisha programu za tiba, kuzuia na kurekebisha. Hii itahusisha kutoa dawa za kupambana na sumu kwa bei rahisi, dawa...

Donald Trump alijitungia barua kuhusu afya yake, daktari Harold Bornstein asema

Aliyekuwa daktari wa Donald Trump amesema kwamba si yeye aliyeiandika barua iliyomweleza mgombea huyo wa chama cha Republican wakati huo kuwa aliyekuwa na "afya nzuri ajabu", vyombo vya habari Marekani vinasema. "[Trump] alitunga na kuamrisha kuandika kwa barua yote," Harold Bornstein aliambia runinga ya CNN Jumanne. Ikulu ya White House haijazungumzia tuhuma hizo za daktari huyo. Bw Bornstein pia amesema maafisa wa serikali walitekeleza "uvamizi" katika afisi zake Februari 2017 na kuondoa nyaraka zote zilizohusiana na taarifa za kimatibabu za Bw Trump. Katika mahojiano na CNN, Bw Bornstein amesema barua hiyo ya mwaka 2015 iliyodokeza kwamba Bw Trump angekuwa "mtu mwenye afya bora zaidi aliyewahi kuchaguliwa kuwa rais" haikuwa utathmini wake wa kitaalamu wa hali yake ya afya. "Nilitayarisha nilipokuwa nasonga," anasema. Haijabainika ni kwa nini Bw Bornstein anatoa tuhuma hizo kwa sasa. Barua hiyo ilisema...