Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KODI

RAIS WA MAREKANI ASEMA RAIS WA UFARANSA AMEFANYA UPUMBAVU

Trump ametishia kulipiza kisasi kwa sababu ya ''upumbavu'' Macron Raisi wa Marekani Donald Trump amemshutumu raisi wa Ufaransa, Emmanuel Macron kwa ''upumbavu'' kuhusu kodi ya huduma za kidigitali, na kudokeza kuwa atalipiza kisasi kwa kutoza kodi mvinyo wa Ufaransa. Trump alionyesha ghadhabu yake kwenye ukurasa wa Twitter siku ya Ijumaa, akijibu mipango ya Ufaransa kutoza kodi mashirika kama Google. Mamlaka za Ufaransa zimedai kuwa makampuni hayo hulipa kiasi kidogo au kutolipa kabisa katika nchi ambazo si makao yao makuu. Utawala wa Trump umesema kodi hiyo inawalenga makampuni makubwa ya teknolojia ya Marekani isivyo haki. ''Ufaransa inampango wa kutoza kodi makampuni yetu makubwa ya teknolojia. Yeyote anayepaswa kuyatoza kodi ni nchi makampuni yanakotoka, yaani Marekani'', Trump aliandika kwenye ukurasa wa Twitter. ''Tutatangaza hatua za kulipiza kisasi kutokana na upumbavu wa Macron muda mfupi ujao.Siku zote nime...