BAADA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kuanza mchakato wa kumsaka kocha mpya wa Taifa Stars, Mbelgiji, Adel Amrouche ameibuka na kufunguka kuwa, akipewa nafasi ya kuinoa timu hiyo, ataipambania ishiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar. Mbali na Kombe la Dunia, pia Mbelgiji huyo mwenye asili ya Algeria, amesema ataanza kwanza kupambana kuhakikisha Taifa Stars inashiriki Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Cameroon. Hivi karibuni, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred, alisema mchakato huo wa kumsaka kocha, unaendelea vizuri ambapo wanaanza kupitia wasifu ‘CV’ mbalimbali za makocha walioomba nafasi hiyo baada ya kocha wa sasa, Salum Mayanga kumaliza mkataba wake tangu mwezi uliopita. Akizungumza na Championi Jumatatu , Kocha Amrouche aliyezaliwa Machi 7, 1968 katika Mji wa Kouba, Algiers nchini Algeria, amesema: “Nina uzoefu na soka la Afrika, nimefundisha timu ya taifa ya Kenya na Burundi, lakini pia kwenye kl...