Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UTAWALA WA SHERIA

RPC Gilles Muroto: Watakaoandamana Dodoma watapigwa hadi kuchakaa

Raia watakaondamana kwa lengo la kuwashinikiza wabunge kushirikiana na Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG nchini Tanzania watakiona cha mtema kuni. Onyo hilo limetoka kwa Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto ambaye amewatahadharisha waliopanga maandamano hayo hapo siku ya Jumanne kwamba watapigwa hadi ''kuchakaa''. Afisa huyo amesema kwamba baadhi ya vyama vya upinzani ikiwemo ACT Wazalendo wamepanga kufanya maandamano kesho kulishinikiza Bunge kufuta kauli yake ya kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad. Muroto ameonya kuwa wale wanaopanaga kufanya safari kuelekea mjini Dodoma ili kushiriki katika maandamano hayo wataambulia kupigwa na kuchakaa. ''Wale wote waliopanga kufanya maandamano mnamo Aprili 9, 2019 wasije kuingia barabarani maana watapigwa na kuchakaa," amesema Muroto. Afisa huyo amesisitiza kuwa maswala ya bunge hutekelezwa ndani ya bunge na wala sio nje hivyoba...

Bunge la Umoja wa Ulaya latoa azimio la kulinda haki za binadamu Tanzania

Rais wa Tanzania akiwa na mjumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Balozi Roeland van de Geer Bunge la Umoja wa Ulaya limetoa njia iitakayo kwa mustakabali wao juu ya uhusiano kati yao na Tanzania kutokana kile walichokiita kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu Tanzania. Azimio hilo limeeleza namna ambavyo hali ya kisiasa nchini Tanzania inavyokandamiza uhuru wa wananchi kutokana na sheria kali zilizopo dhidi ya asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, vyombo vya habari na vyama vya siasa na huku hofu kubwa ikitanda kwa wapenzi wa jinsia moja. Vilevile wamekemea matukio yote ya chuki na vurugu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Paul Makonda anaacha kuwatishia watu jamii hiyo na haki kutendeka. Hata hivyoserikali ya Tanzania ilijitenga na msimamo wa kiongozi huyo wa Dar es salaam. Bunge hilo limetaka uchunguzi huru kufanyika ili ukweli juu ya mashambulio na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari, wapenzi wa jinsia mo...