: Mahakama jijini Nairobi imewahukumu washukiwa watatu wa ugaidi nchini Kenya waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio la mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa. Miongoni mwa waliohukumiwa ni Rashid Charles Mbeserero anayetuhumiwa kuhusika katika shambulio hilo ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, wengine waliohukumiwa na Mtanzania huyo ni Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar ambao wao wamehukumiwa kwenda jela miaka 41 kila mmoja. Wote walipatikana na hatia ya kupanga shambulio hilo chini ya ushirikiano wa wanachama wa Kundi la Al-Shabab.Takriban wanafunzi 148 walifariki dunia katika shambulio hilo. Hukumu hiyo imepitishwa baada ya mahakama kujiridhisha kuwa watatu hao ni wanachama wa Kundi la Al-shabab kutoka Somalia