Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UWEKEZAJI

Mwanamfalme wa Saudia asema hana mpango wa kuinunua klabu Manchester United:

Manchester United: Mwanamfalme wa Saudia asema hana mpango wa kuinunua klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amekanusha madai kuwa anantaka kuinunua Manchester United kwa kitita cha pauni bilioni 3.8. Tetesi ziliibuka mwishoni mwa wiki zikimuhusisha mwanamfalme huyo na kutaka kuinunua klabu hiyo tajiri nchini Uingereza. Wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazers wanadaiwa kuwa hawana mpango wa kuiuza timu yao. Wamiliki hao kutoka Marekani waliinunua Man United kwa kitita cha pauni milioni 790 mwezi Mei 2005. "Ripoti zinazomuhusisha Mwana Mfalme Mohammed Bin Salman kuwa anataka kuinunua Manchester United ni uongo mtupu," amesema waziri wa michezo wa Saudia Turki al-Shabanah. "Manchester United walifanya mkutano na mfuko wa uwekezaji wa umma PIF wa Saudia kuhusu nafasi ya udhamini. Lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa," ameeleza waziri huyo. Salman, 33, aliteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha ...