Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UN

Umoja wa Mataifa Waonya Dhidi ya Kugawanya Dunia 'Katika Pande Mbili'

Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa mataifa ya G7 kujiepusha na kugawanya ulimwengu katika kambi za mtindo wa Vita Baridi zinazofungamana na Marekani au China. Wakati huo huo, viongozi hao wa Magharibi walizifanya Urusi na China kuwa kiini cha taarifa ya pamoja kuhusu silaha za nyuklia. Akizungumza na gazeti la Kyodo News la Japan wakati viongozi wa Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani walipokutana Hiroshima siku ya Jumamosi, Guterres alitoa wito wa "mazungumzo na ushirikiano hai" kati ya mataifa ya G7 na China kuhusu masuala ya hali ya hewa. mabadiliko na maendeleo. "Ninaamini ni muhimu kuepuka mgawanyiko wa dunia kuwa mbili, na ni muhimu kuunda madaraja ya mazungumzo ya dhati," alisema.

Damage To Zaporozhye Nuclear Power Plant From Ukrainian Shelling Repaired — Official

Uharibifu wa Kiwanda cha Nguvu za Nyuklia cha Zaporozhye Kutoka kwa Makombora ya Kiukreni Imekarabatiwa - Rasmi  Kituo hicho kimekarabatiwa kikamilifu kutokana na uharibifu uliosababishwa na makombora ya Ukraine na ulinzi wa usalama umewekwa;  afisa wa Rosenergoatom alisema kabla ya ziara ya mkuu wa IAEA Rafael Grossi Jumatano.  "Tulichukua hatua za ziada ili kuhakikisha usalama wa nyuklia na kuunda muundo wa kuhakikisha uadilifu wa kituo cha kuhifadhi taka za nyuklia," Renat Karchaa, mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Opereta wa NPP wa Urusi. Grossi alifika Jumatano kukagua viwango vya usalama vya tovuti, ambavyo Karchaa alisisitiza vilifunikwa baada ya juhudi zilizofanywa tangu Septemba iliyopita kupata vifaa vya miundombinu vinavyohusiana na vifaa vya mionzi.

Kura ya UNSC Kuhusu Azimio la Urusi Inaongeza Tuhuma - Moscow

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu lilikataa azimio lililoungwa mkono na Urusi la kutaka uchunguzi huru wa kimataifa ufanyike kuhusu milipuko iliyoharibu pakubwa mabomba ya gesi ya Nord Stream 1 na 2 msimu wa vuli uliopita.  Wanadiplomasia wa Urusi walipendekeza kuwa matokeo ya kura hiyo yalitokana na shinikizo la kidiplomasia lililotolewa na nchi za Magharibi.  Rasimu ya azimio, ambayo ilitaka kuunda tume huru ya kimataifa kuchunguza “vipengele vyote vya hujuma” ya mabomba ambayo yaliunganisha moja kwa moja Urusi na Ujerumani chini ya Bahari ya Baltic, pamoja na kutambua wafadhili na waandaaji wa shambulio hilo, iliungwa mkono.  na nchi tatu (Urusi, Uchina, na Brazili).  Hakuna nchi iliyopiga kura dhidi ya waraka huo, na watu 12 hawakupiga kura, na kusababisha azimio hilo kukataliwa.  Vassily Nebenzia, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Moscow, alisema kwamba baada ya kura hiyo, “tuhuma [kuhusu] nani anahusika na hujuma kwenye Nord Stream...

Kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Awad Ibn Auf kwanini amejiuzulu

Bwana Ibn Auf ameondoka madarakani siku moja baada ya kuwa mkuu wa baraza la jesi Mkuu wa baraza la Jeshi la Sudani amejiuzulu siku moja baaba ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir yaliyosababishwa na wimbi la maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. Waziri wa ulinz Awad Ibn Auf alitangaza uamuzi huo kwenye TV, na kumtaja mrithi wake Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan. jeshi limesema kuwa litaendelea kuwa madarakani kw amiaka miwili na baadae utafanyika uchaguzi. Lakini viongozi wa maandamano wanasema hawataondoka mitaani hadi jeshi litakapokabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia. Kuanguka kwa Bwana Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza mwezi Disemba mwaka jana ambapo waandamanaji walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu. Bwana Ibn Auf alikuw amkuu wa ujasusi katika jeshi wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007. James Copnal...

Kiongozi wa mapinduzi ya Sudan Awad Ibn Auf kwanini amejiuzulu

Bwana Ibn Auf ameondoka madarakani siku moja baada ya kuwa mkuu wa baraza la jesi Mkuu wa baraza la Jeshi la Sudani amejiuzulu siku moja baaba ya kuongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Omar al-Bashir yaliyosababishwa na wimbi la maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. Waziri wa ulinz Awad Ibn Auf alitangaza uamuzi huo kwenye TV, na kumtaja mrithi wake Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan. jeshi limesema kuwa litaendelea kuwa madarakani kw amiaka miwili na baadae utafanyika uchaguzi. Lakini viongozi wa maandamano wanasema hawataondoka mitaani hadi jeshi litakapokabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia. Kuanguka kwa Bwana Bashir kulifuatia maandamano na vurugu zilizoanza mwezi Disemba mwaka jana ambapo waandamanaji walilalamikia kupanda kwa bei za bidhaa muhimu. Bwana Ibn Auf alikuw amkuu wa ujasusi katika jeshi wakati wa mzozo wa jimbo la Darfur ulioibuka mwaka 2000. Marekani ilimuwekea vikwazo mwaka 2007. James Copnal...

Muungano wa G7 na Umoja wa mataifa walaani mapigano mapya Libya

Vikosi tiifu kwa serikali ya Tripoli vimeripotiwa kuungana na serikali kulinda mji mkuu Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani G7, pamoja na Umoja wa mataifa yamelaani vikali mapigano yaliozuka upya nchini Libya. Mataifa hayo yanataka pande zinazohasimiana Libya "kusitisha mara moja shughuli za kijeshi". Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa wito huo. Tripoli ni makao makuu ya serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa, na ambayo pia inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Vikosi vya kulinda usalama vya umoja wa mataifa katika mji huo vimekuwa katika hali ya tahadhari. Ghasia zimekumba Libya tangu utawala kiongozi wa nchi hiyo wa mda mrefu, Muammar Gaddafi kuangushwa na yeye kuuawa mwaka 2011. Nini kinachofanyika ? Kamanda Khalifa Haftar, ambaye ni kiongozi wa vikosi vya kijeshi vinavyopinga utawala wa Tripoli siku ya Alhamisi aliamuru vikosi vyake kuingia mji wa Libya. Hatua hiyo ilijiri wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Ma...

Rais Donald Trump afanya ziara ya kushutukiza nchini Iraq

Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Rais wa Marekani Donald Trump na mke wake Melania Trump wamefanya ziara ya ghafla ya krismasi ya kuwatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Iraq. Walisafiri kwenda huko usiku wa siku ya Krismasi kuwashukuru wanajeshi hao kwa huduma yao, mafanikio na kujitolea kwa mujibu wa White house. Bw Trump alisema Marekani haina mpango wa kuondoka nchini Iraq. Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya waziri wa ulinzi Jim Mattis kujiuzulu kufuatia mgawanyiko wa sera za Trump eneo hilo. Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Marekani ina wanajeshi 5,000 nchini Iraq kuunga mkono serikali katika vita dhidi ya kundi la Islamic State. Hata hivyo mkutano uliopangwa kati ya Bw Trump na waziri mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi ulifutwa. Ofisi ya Bw Mahdi ilisema hiyo ni kwa sababu ...

Bunge la Umoja wa Ulaya latoa azimio la kulinda haki za binadamu Tanzania

Rais wa Tanzania akiwa na mjumbe wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Balozi Roeland van de Geer Bunge la Umoja wa Ulaya limetoa njia iitakayo kwa mustakabali wao juu ya uhusiano kati yao na Tanzania kutokana kile walichokiita kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binaadamu Tanzania. Azimio hilo limeeleza namna ambavyo hali ya kisiasa nchini Tanzania inavyokandamiza uhuru wa wananchi kutokana na sheria kali zilizopo dhidi ya asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, vyombo vya habari na vyama vya siasa na huku hofu kubwa ikitanda kwa wapenzi wa jinsia moja. Vilevile wamekemea matukio yote ya chuki na vurugu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kuitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa Paul Makonda anaacha kuwatishia watu jamii hiyo na haki kutendeka. Hata hivyoserikali ya Tanzania ilijitenga na msimamo wa kiongozi huyo wa Dar es salaam. Bunge hilo limetaka uchunguzi huru kufanyika ili ukweli juu ya mashambulio na unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari, wapenzi wa jinsia mo...

BANGI KUTUMIKA HADHARI SASA

Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi? Sehemu mbalimbali duniani mtazamo kuhusiana na matumizi ya mmea wa cannabis yaani bangi unabadilika kwa kasi. Serikali mpya ya Mexico ina mpango wa kuhalalisha matumizi ya bangi kama njia ya kujiburudisha, sawa na ilivyofanya utawala mpya wa Luxembourg. Wakati huo huo, viongozi wakuu nchini New Zealand, wanakusudia kuandaa kura ya maoni ya namna watakavyoshughulikia swala hilo. Jinsi maoni ya umma - na yale ya serikali- yanavyobadilika, ni dhahiri kuwa mataifa mengi yatafuata mkondo huo. Maswali yanayoibuka ni kwa namna gani nchi hizo zitadhibiti matumizi na usambazaji wa mmea huo? Ni nini hasa kinachopelekea mataifa mbalimbali katika kulegeza kamba kwenye sheria zake, au hata kuamua kuidhinisha ,matumizi ya bangi moja kwa moja? Vita dhidi ya mihadarati Ilikuwa mwaka 2012 ambapo Uruguay, ilipoandika historia kwa kuwa taifa la kwanza duniani kuruhusu matumizi ya bangi kwa minajili ya kujiburudisha. Hatua hiyo, ...

Mtanzania Joyce Msuya ateuliwa naibu katibu mkuu wa UNEP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amemteua Mtanzania Joyce Msuya kuwa Naibu Katibu Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mazingira duniani, UNEP. Afisi kuu za shirika hilo la UN huwa jijini Nairobi, Kenya. Bi Msuya atachukua nafasi ya Ibrahim Thiaw wa Mauritania, ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu. Hadi wakati wa kuteuliwa kwake Jumatatu, Bi Msuya alikuwa mshauri wa Makamu Rais wa Benki ya Dunia kwa ukanda wa Asia Mashariki na Pacific jijini Washington, DC wadhifa alioushikilia tangu mwaka jana. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, kwa mujibu wa UN alisema "Bi Msuya analeta uzoefu wake wa zaidi ya miaka 20 kwenye nyanja za maendeleo ya kimataifa kuanzia masuala ya mashirika, mikakati, uendeshaji, ufahamu wa usimamizi na ubia alioupata wakati akifanya kazi huko Afrika, Amerika Kusini na Asia." Alishika nyadhifa mbalimbali katika ngazi ya uandamizi kwenye Benki ya Dunia ikiwemo mwakilishi wa Benki ya Dunia na Mkuu wa...

Mashambulizi dhidi ya Syria hayakuwa halali-Ripoti ya Bunge la Ujerumani

Ripoti ya wataalamu wa masuala ya sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani imesema mashambulizi yaliyofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa dhidi ya Syria mapema mwezi Aprili yalikiuka sheria ya kimataifa. Ripoti ya wataalamu wa sheria za kimataifa katika Bunge la Ujerumani, imesema mashambulizi yaliyofanywa na nchi tatu za Magharibi hayakuwa halali kisheria. Marekani, Uingereza na Ufaransa ziliishambulia Syria kwa makombora tarehe 14 Aprili, kwa madai kwamba zilikuwa zikiiadhibu serikali ya Rais Bashar al-Assad, ziliyemshutumu kutumia gesi ya sumu kuwashambulia raia katika mji wa Douma. ''Matumizi ya nguvu za kijeshi dhidi ya nchi huru, kama hatua dhidi ya ukiukaji wa sheria na kanuni za kimataifa unaodaiwa kufanywa na nchi inayoshambuliwa, ni uvunjaji a sheria ya kimataifa inayozuia matumizi ya ghasia,'' imesema ripoti hiyo ya wataalamu wa kisheria wa Bunge la Ujerumani, Bundestag. Ripoti hiyo iliombwa na chama cha mrengo wa kushoto (Die-Linke) cha Uj...

Wafadhili waichangishia fedha Congo

Wafadhili wanakutana mjini Geneva Uswisi Ijumaa katika harakati za kuchangisha dola bilioni 1.7 kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo inakabiliwa na mzozo. Wataalam wanasema huenda mzozo huo ukapindukia na kuwa janga kubwa. Mkutano huo unakuja wakati kukiwa na hofu kwamba  mizozo ya kikabila, ufisadi na hali mbaya ya usalama ni mambo yanayozusha hofu ya umwagikaji damu. Kwa wale walioachwa bila makao, kitisho ni cha kweli. Raia mmoja wa Congo alielezea mzozo wa kikabila katika mkoa wa Ituri kwa kusema, "ni kama wakati tulipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe." Kulingana na makadirio ya shirika la msalaba mwekundu karibu Wacongo 70,000 wamekimbilia Uganda kwa kuuvuka mto Albert tangu Januari. Ituri ni mkoa mmoja tu kati ya mingi ambayo makundi yaliyojihami na wahalifu wanawasumbua raia. Ukosefu wa usalama umezidisha idadi ya wakimbizi wa ndani ya nchi Zaidi ya hayo kuna mzozo wa kisiasa unaozunguka suala la urais ambapo watu wengi wanamtaka rais Joseph...

Guterres: Uhamiaji umekuwepo Duniani tangu jadi

MTEULE THE BEST Tarehe 18, Desemba ni Siku ya Uhamiaji Duniani. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema suala la uhamiaji limekuwepo tangu jadi na utaendelea kuwepo siku zote. Katibu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema jibu katika kushughulikia suala la uhamiaji ni ushirikiano mzuri wa kimataifa katika kuangazia sababu zinazochangia ongezeko la wahamiaji ili kuhakikisha manufaa yake yanasambazwa kwa usawa na haki za binadamu zinalindwa ipasavyo. Umoja wa Mataifa umesema katika historia ya mwanadamu, uhamiaji umekuwa kielelezo cha kuonyesha ujasiri na ari ya watu binafsi kukabiliana na changamoto mbele yake ili kutimiza ndoto ya kuwa na maisha bora. Katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi pamoja na kuimarika katika teknolojia za mawasiliano na usafiri, kumechangia pakubwa katika kurahisisha kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa watu na kuongeza idadi ya watu ambao wana dhamira na uwezo wa kuhamia kwingine duniani. Nyakati hizi za sasa zimetoa fur...