Lebanon: Mwanachama wa ISIS Akamatwa kwa Kupanga Njama ya Kumuua Papa Leo XIV Wakati wa Ziara ya 2025
Idara ya Ujasusi ya Jeshi la Lebanon imethibitisha kukamatwa kwa raia wa Syria anayedaiwa kuwa mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Islamic State (ISIS), anayetuhumiwa kupanga njama ya kumuua Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Leo XIV, wakati wa ziara yake ya kihistoria nchini Lebanon mwaka 2025. Mtuhumiwa anafahamika kwa jina la kivita kama "Al-Daamish". Kwa mujibu wa chaneli ya MTV Lebanon na ripoti za kiusalama, Al-Daamish si jina geni katika ugaidi. Aliwahi kuwa mpiganaji wa Nusra Front kabla ya kuhamia ISIS, ambapo alipanda cheo hadi kuwa Naibu Gavana wa Aleppo ndani ya kundi hilo. Inadaiwa alikamatwa na utawala wa Bashar al-Assad na kutumikia kifungo cha miaka mitatu. Baada ya kuanguka kwa utawala wa Assad Desemba 2024 na kufunguliwa kwa magereza nchini Syria, alitoroka na kuingia Lebanon kinyume cha sheria. Njama ya Mauaji Ilipangwaje Vyanzo vya kiusalama vinasema kuwa baada ya kuingia Lebanon, Al-Daamish aliwasiliana tena na viongozi wake wa I...