VIBAKA WAVUNJA MAKAZI YA KADINALI ERNEST SIMONI (97) FLORENCE




Florence, Italia Tukio la kusikitisha limetokea katika Curia ya Piazza Duomo, Florence.

Makazi ya Muadhama Kadinali Ernest Simoni, (97), ambaye ni MAlbania na shahidi haiwa mateso ya Kanisa chini ya utawala wa Kikomunisti wa Enver Hoxha, yamevamiwa na wezi sugu.

Yaliyotokea

Kwa mujibu wa gazeti la Corriere Fiorentino na shirika la habari la Adnkronos, tukio limetokea mchana wakati hakuna mtu nyumbani. Kadinali Simoni yupo London kwa mwaliko wa kukutana na Mfalme Charles III wa Uingereza, huku mpwa wake Tonin Simoni na mkewe wakiwa mgahawani kwao Borgo Albizi.
Wezi walifanya kazi kwa utulivu wa kutisha. Walivunja mlango wa kinga na kubomoa sehemu ya ukuta kwa kutumia patasi nzito (scalpelli) kisha wakafungua makabati na masanduku. Waliondoka na kiasi cha takriban €30,000, vito vya dhahabu, na hata kadi ya ukaazi ya Kadinali.
Mpwa wake amesema: "Tumeshtushwa sana. Tulijihisi salama. Hatukutegemea kabisa wizi wa kinyama kama huu katikati ya Piazza Duomo. Hii ni aibu kwa jiji."

Imebaki Historia Yake

 Kadinali Simoni si mtu wa kawaida. Alizaliwa 1928, akahukumiwa kifo mara mbili kwa sababu ya imani yake, adhabu iliyobadilishwa kuwa miaka 28 ya kazi za kulazimishwa - kuvunja mawe, kuchimba madini mita 500 chini ya ardhi, na kusafisha mitaro ya Shkoder. Papa Fransisko alimteua kuwa Kadinali mwaka 2016 kama ishara ya heshima kwa mateso yake.

Jibu lililogusa mioyo ya wengi

Alipoarifiwa kwa simu akiwa London, Kadinali hakuulizia pesa wala dhahabu. Swali lake la kwanza lilikuwa: "Je, chumba changu cha sala kimeharibiwa? Je, sanamu ya Bikira Maria wa Medjugorje na ya Padre Pio ziko salama?"

Alipojibiwa kuwa hazijaguswa, akasema kwa tabasamu: "So, no big deal."

Kwa mtu aliyepoteza karibu maisha yake yote kwa ajili ya Kristo, €30,000 si hasara. Imani yake ndiyo hazina yake.

Polisi wa Carabinieri wanaendelea na uchunguzi kupitia kamera za usalama za eneo hilo.

Tumuombee Kadinali wetu aendelee kuwa na afya njema.

Chanzo: Adnkronos / Corriere Fiorentino - 18 Sept 2026
#Florence #CardinalSimoni #KanisaKatoliki

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU