Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya PAPA

PAPA FRANCISCO NA MAPADRE WATANZANIA & CDF MABEYO

▪︎Katika picha ni Papa Francisco akiwa na Mapadre watanzania wanaosoma na kufanya utume wako nchini Italia pamoja Na Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. ▪︎Ikumbukwe Maaskofu wote nchini Tanzania wako katika ziara ya Kichungaji yalipo makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani mjini Vatican tangu May 14 hadi May 21, 2023. ▪︎Pia katika ziara hiyo wameambatana na Mapadre kadhaa akiwemo Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padre Chesco Msaga C.PP.S Naibu Katibu Mkuu (TEC) bila kumsahau Padre Thomas Kiangio Msimamizi  wa Jimbo Katoliki Tanga. . . RADIO MARIA TANZANIA

Waraka wa Papa kwa Wachile ni sawa na kutangaza 'hali ya hatari kiroho'

Waraka wa Papa kwa Wachile ni sawa na kutangaza 'hali ya hatari kiroho' Makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican yamesema hatua ya Papa Francis kuomba radhi kutokana na kashfa ya udhalilishaji wa kingono uliofanywa na padri na askofu Chile ni sawa na kutangaza hali ya hatari kiroho katika Kanisa la Chile.Papa amewaomba waathirika kwenda Rome ili awaombe radhi pamoja na kuwaita maaskofu wote wa Chile kwa mkutano wa dharura kujadili namna ya kurekebisha madhara yaliyotokana na kashfa hiyo ambayo imeichafua taswira ya Kanisa Katoliki nchini Chile na sifa ya Papa. Msemaji wa Vatican Grek Burke amesema waraka wa Papa kwa Kanisa Katoliki Chile ni kukiri kuwa alifanya makosa katika mtizamo kuhusu madhila waliyopitia waathiriwa. Hapo jana, Papa alikiri kuwa alifanya makosa makubwa katika maamuzi aliyoyachukua kuhusu sakata la udhalilishaji wa kingono Chile.

Papa aizuru Myanmar inayotuhumiwa kwa mauaji Ziara hii huenda ni jukumu zito kidiplomasia katika miaka minne ya Papa Francis kama kiongozi wa kanisa katoliki.

Papa Francis aliondoka Roma Jumapili usiku Papa Francis anaanza ziara ya wiki nzima nchini Myanmar na Bangladesh leo Jumatatu, wakati wasiwasi unaendelea wa kimataifa kuhusu usalama na ulinzi kwa wasilamu wa Rohingya. Anatarajiwa kukutana na Aung Sun Suu Kyi na mkuu wa jeshi Myanmar. Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar - Rohingya. Ni jina lisilo tumika na serikali ya kiraia na jeshi - wakieleza kuwa ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh na kwahivyo hawapaswi kuorodheshwa kama mojawapo ya makabila nchinihumo. Nchi hiyo yenye idadi kubwa ya maBudda inajitayarisha kumkaribisha Papa Lakini mashirika ya kutetea haki za binaadamu wanamuomba awaite hivyo, yakieleza kuwa nilazima Papa Francis aoneshe huruma kwa watu walionyimwa uraia na tangu Agosti wamekabiliwa na kile kamishna wa haki za binaadamu katika Umoja wa mataifa amekitaja kuwa 'kinachoonekana kuwa mauaji ya kikabila...

Papa Francis apiga marufuku uuzaji wa sigara Vatican

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage caption Licha ya sigara kuiletea mamilioni ya fedha Vatican ,papa Francis amesema kuwa hawezi kuruhusu binaadamu kuathiriwa kiafya Papa Francis ameagiza marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya Vatican , kuanzia mwaka ujao. Msemaji wa Vatican Greg Burke alisema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu. Takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua sigara zilizopunguzwa bei . Mauzo hayo yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya yuro kila mwaka. Lakini bwana Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu. Mtoto amvua kofia Papa Francis Alinukuu takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka. ''Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaopata'' ,alisema. ''Ni kitu ambacho ni lazima...