Waraka wa Papa kwa Wachile ni sawa na kutangaza 'hali ya hatari kiroho'
Makao makuu ya Kanisa Katoliki ya Vatican yamesema hatua ya Papa Francis kuomba radhi kutokana na kashfa ya udhalilishaji wa kingono uliofanywa na padri na askofu Chile ni sawa na kutangaza hali ya hatari kiroho katika Kanisa la Chile.Papa amewaomba waathirika kwenda Rome ili awaombe radhi pamoja na kuwaita maaskofu wote wa Chile kwa mkutano wa dharura kujadili namna ya kurekebisha madhara yaliyotokana na kashfa hiyo ambayo imeichafua taswira ya Kanisa Katoliki nchini Chile na sifa ya Papa. Msemaji wa Vatican Grek Burke amesema waraka wa Papa kwa Kanisa Katoliki Chile ni kukiri kuwa alifanya makosa katika mtizamo kuhusu madhila waliyopitia waathiriwa. Hapo jana, Papa alikiri kuwa alifanya makosa makubwa katika maamuzi aliyoyachukua kuhusu sakata la udhalilishaji wa kingono Chile.
Maoni