Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya IRAN

Marekani Yafanya Mashambulio ya Anga ya Kulipiza kisasi nchini Syria

 Jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi ya anga yaliyosahihi nchini Syria kujibu shambulio la ndege isiyo na rubani na kumuua mwanakandarasi mmoja wa Marekani na kuwajeruhi wafanyakazi watano wa Marekani.  Shambulio la awali lilifanywa na, na mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya, "makundi yenye uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran", kulingana na Idara ya Ulinzi.  "Mashambulizi hayo ya anga yalifanywa kujibu mashambulizi ya leo pamoja na mfululizo wa mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya vikosi vya Muungano nchini Syria na makundi yenye uhusiano na IRGC," Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin alisema.  Jiandikishe kwa RT

IRAN YALIPIZA KISASI YAKAMATA MELI YA UINGEREZA

Iran yakamata meli ya Uingereza eneo la Ghuba Kutakuwa na 'madhara makubwa''ikiwa Iran haitaachia meli ya mafuta ya uingereza wanayoishikilia, Waziri wa mambo ya kigeni Jeremy Aunt ameeleza. wamilili, Stena Impero kuwa wameshindwa kufanya mawasiliano na meli hiyo. Kamati ya dharura ya serikali hiyo, cobra, anakutana kwa ajili ya kuzungumzia jambo hilo. Bwana Hunt amesema kitendo hicho ''hakikubaliwi kabisa. ''Tunajua wazi kuwa hali hii haitakuwa rahisi kuitatua, kutakuwa na madhara makubwa,'' alisema. ''hatuangalii suluhu ya kijeshi.Tunatafuta suluhu ya kidiplomasia kutatua hali hii, lakini tunajua tunapaswa kushughulikia.'' Amesema wafanyakazi ndani ya meli walikuwa wa mataifa tofauti tofauti lakini hakuna raia wa Uingereza aliykuwa akifahamika kuwa ndani ya chombo hicho. Chombo cha kampuni ya Stena Impero ilikuwa ikisafiri majini ikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London. ''Balozi wetu mjini Tehran anf...

MAREKANI YALIPIZA KISASI KWA IRAN

Raisi wa Marekani Donald Trump amesema jeshi la maji la Marekani limetungua ndege isiyo na rubani ya Iran katika eneo la mpaka kati ya ghuba ya uajemi na ghuba ya Oman. Amesema meli ya jeshi lake ''ilichukua hatua'' siku ya Alhamisi baada ya ndege hiyo kusogea kwa takriban mita 914 karibu na chombo hicho. Iran haijasema chochote kuhusu hilo. Mwezi Juni, Iran iliangusha ndege ya kijeshi isiyo na rubani ya Marekani, na kusababisha hofu ya kutokea mzozo wa kijeshi. Awali Tehran ilisema imekamata ''meli ya kigeni'' na wafanyakazi wake 12 siku ya Jumapili kwa kusafirisha mafuta kinyume cha sheria. Iran imekuwa ikishutumiwa na Marekani kwa kushambulia meli zake tangu mwezi Mei.Tehran ilikana shutuma hizo. Raisi Donald  Trump  amesemaje ? Akizungumza Ikulu, Trump amesema ''Ninataka kuwajulisha kuhusu tukio lililotokea kwenye eneo la mpaka wa Hormuz leo lililohusisha meli yetu ya kijeshi. Chombo hicho kilichukua hatua ya kujilinda dhidi ya nde...

TRUMP AVUNZA MKATABA KUMKERA BARACK OBAMA SIRI HADHARANI

Barua mpya iliyovuja yadai Trump amevunja mkataba wa nyukilia 'ili kumkera Obama' Rais Donald Trump ameachana na mkataba wa nyukilia wa Iran ili kumkera Barack Obama, hiyo ni kwa mujibu wa barua ya siri iliyovuja kutoka kwa aliyekuwa balozi wa Uingereza nchini Marekani. Sir Kim Darroch alielezea hatua ya Trump kuvunja mkataba huo kama "ubadhirifu wa kidiplomasia" kwa mujibu wa gazeti la Mail on Sunday. Gazeti hilo linadai kuwa barua hiyo iliandikwa baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Borris Johnson kuirai Marekani mwaka 2018 kusalia ndani ya makubaliano hayo. Barua hii mpya inavuja katikakipindi ambacho polisis nchini Uingereza wameonya juu ya uchapishwaji wa barua hizo. Barua ya kwanza kutoka kwa balozi huyo ambayo ilikuwa inakosoa utawala wa Trump ilivuja wiki moja iliyopita na kusababisha majibizano ya hasira baina ya Uingereza na Marekani. Majibizano hayo yamesababisha Sir Kim kujiengua kwenye wadhifa wake licha ya serikali ya ...

Boti za Iran zajaribu kuzuiwia meli ya Uingereza kulipiza kisasi

Meli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose imeripotiwa kuifukuza mbali maboti ya Iran Maboti ya Iran yaliyosheheni silaha yameripotiwa kujaribu kuzuwia safari ya meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la kuwa maji la Strait of Hormuz - kabla ya ya kufukuzwa na meli ya kikosi cha majini cha Uingereza. Taarifa za vyombo vya habari zimenukuu maafisa wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya mafuta iliambiwa isimame katika maji ya Iran yaliyopo karibu ,lakini ikarudi nyuma na kuondoka baada ya onyo kutolewa na mele ya jeshi ya Uingereza. Iran imekuwa ikitishia kulipiza kisasi kufuatia kushikiliwa kwa moja ya meli zake za mafuta ambayo ilitekwa karibu na ibraltar wiki iliyopita. Makao makuu ya wizara ya Ulinzi nchini Marekani Pentagon yamesema kuwa yanataarifa juu ya tukio hilo lakini hayakutoa taarifa zaidi. Kwa mujibu wa taarifa , boti tano zinazoaminiwa kumilikiwa na jeshi la Iran Iranian Revolutionary Guard ziliikaribia meli ya mafuta ya Uingereza ilipokuwa ikiondoka eneo la...

Iran 'imeongeza urutubishaji wa uranium' baada ya vikwazo vya Marekani

inu cha Bushehr kinaweza kutumia madini ya uranium kama nishati Iran imekiuka makubalino ya kiwango inachopaswa kurutubisha cha madini ya uranium kwa mujibu wa mkataba wa 2015 ulioidhinishwa na mataifa yenye nguvu duniani, vyombo vya habari Iran vinaripoti. Shirika la habari la Isna limemnukuu waziri wa mambo ya nje nchini humo aliyethibitisha kuwa taifa hilo limerutubisha zaidi ya kilo 300 zilizotakiwa Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki limesema litwasilisha ripoti. Iran imeshinikiza urutubishaji huo wa uranium inayotumika kama nishati na pia silaha za nyuklia kufuatia kuidhinishwa upya vikwazo vya marekani dhidi yake. Mataifa ya Ulaya yameonya kuwa ukiukaji wowote utakuwa na athari zake. Je Marekani ina malengo gani Iran? Je unayafahamu yaliomo katika mkataba wa nyukilia wa Iran ? Trump ajibu kauli ya Iran aliyoiita ya ''kijinga na yenye matusi'' Iwapo hilo litathibitishwa na shirika la IAEA, linatoa fursa kuidhinishwa upya kwa vikwazo vili...

Rais Donald Trump afanya ziara ya kushutukiza nchini Iraq

Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Rais wa Marekani Donald Trump na mke wake Melania Trump wamefanya ziara ya ghafla ya krismasi ya kuwatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Iraq. Walisafiri kwenda huko usiku wa siku ya Krismasi kuwashukuru wanajeshi hao kwa huduma yao, mafanikio na kujitolea kwa mujibu wa White house. Bw Trump alisema Marekani haina mpango wa kuondoka nchini Iraq. Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya waziri wa ulinzi Jim Mattis kujiuzulu kufuatia mgawanyiko wa sera za Trump eneo hilo. Rais Donald Trump na Melania wawatembelea ghafla wanajeshi wa Marekani nchini Iraq Marekani ina wanajeshi 5,000 nchini Iraq kuunga mkono serikali katika vita dhidi ya kundi la Islamic State. Hata hivyo mkutano uliopangwa kati ya Bw Trump na waziri mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi ulifutwa. Ofisi ya Bw Mahdi ilisema hiyo ni kwa sababu ...

Iran yatoa masharti kuhusu mwafaka wa nyuklia

Iran inataka mataifa ya Ulaya kuwafidia ifikapo mwisho wa mezi Mei baada ya Marekani kujiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015, kwa mujibu wa afisa mwandamizi. Iran itaamua iwapo itasalia kwenye mpango huo. Makubaliano ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu ulimwenguni yaliondoa vikwazo dhidi ya Iran huku taifa hilo likitakiwa kusitisha mpango wake wa nyuklia. Tangu Rais Donald Trump aiondoe Marekeni kwenye makubaliano hayo mwezi uliopita, mataifa ya Ulaya yamekuwa yakijaribu kuhakikisha kuwa Iran inafaidika kiuchumi ili kuishawishi kuendelea kusalia kwenye mwafaka huo. Lakini jambo hilo linasalia kuwa changamoto baada ya kampuni za Ulaya kutishwa na vikwazo vya Marekani. Mataifa yaliyosalia kwenye mwafaka huo yanakutana Ijumaa (25.05.2018) kwa mara ya kwanza tangu Trump kujindoa kwenye makubaliano hayo, lakini wanadiplomasia hawaoni mwafaka huo ukidumishwa. Maofisa wa Uingereza, Uchina, Ufaransa, Ujerumani na Urusi wanakutana na naibu waziri wa masuala...

Merkel na Li watetea makubaliano na Iran

Kansela wa Ujerumani  Angela Merkel na waziri mkuu  wa China Li Keqiang wametetea makubaliano ya kinyuklia na Iran, wakati Li  akisema kusitisha makubaliano hayo kutaleta utata katika majadiliano na Korea kaskazini. Merkel   na  Li  walionesha  msimamo  wa  pamoja  kuelekea  Iran pamoja  na  biashara  huru, masuala  mawili  ambayo  yameshuhudia uingiliaji  kati  wa  Marekani  ambapo  rais  Donald Trump  alichukua hatua  hiyo. Hayo  yalijadiliwa  katika  mkutano  wao  katika  ziara ya  kansela  Merkel  mjini  Beijing. waziri mkuu wa China Li Keqiang (kushoto) akizungumza na kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kulia) Li  alionya  kwamba  kusitisha makubaliano  hayo  na  ...

Zarif afanya juhudi za kuokoa makubaliano ya kinyuklia

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Javad Zarif amesema nchi yake itahitaji uhakikisho kutoka mataifa mengine yenye nguvu  duniani iwapo iendelee kutekeleza mkataba wa kinyuklia wa mwaka  2015, baada ya Marekani  ikujitoa. Waziri wa mambo  ya  kigeni  wa Urusi  Sergei Lavrov  alikutana  na  mwenzake huyo wa  Iran mjini Moscow  Jumatatu  kujadili kile  kinachoweza  kufanyika  kulinda makubaliano  hayo  na  Iran  baada  ya  uamuzi  wa  rais  wa Marekani Donald Trump kujitoa  katika  mkataba  huo.  Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif Iran  jana  iliupa  Umoja  wa  Ulaya  siku  60 kutoa uhakikisho wa kuendelea  na  utekelezaji  wa  makubaliano  hayo  ya  kinyuklia baada...

Marekani yazitaka nchi nyingine kuishinikiza Iran

Serikali ya Marekani imezitaka nchi nyingine kuongeza shinikizo kwa Iran kutokana na kuhusika kwake katika mzozo wa Mashariki ya Kati. Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imelikosoa Jeshi la Mapinduzi la Iran, kutokana na vitendo vyake vya kuchangia katika kusababisha ushawishi wa kukosekana kwa amani na utulivu katika Mashariki ya Kati, licha ya watu wa Iran kuwa waathirika wa uchumi unaosuasua. Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Huckabee Sanders amevitolea mfano vitendo hivyo vya Iran ambavyo inavifanya katika nchi za Syria na Saudi Arabia na ameyataka mataifa mengine duniani kuishinikiza Iran kuachana na tabia yake hatari. Taarifa hiyo ya Marekani imevikosoa vikosi hivyo kwa kurusha makombora dhidi ya Israel katika milima ya Golan mwanzoni mwa juma hili, hali iliyosababisha Israel kujibu pia kwa mashambulizi siku ya Alhamisi dhidi ya vikosi vya Iran. Hali hiyo imezusha hofu ya kuzuka kwa mzozo katika ukanda huo na hivyo kuhatarisha amani na usalama wa Mashariki ya Kati...

Ulaya yaahidi kuyalinda makubaliano juu ya nyuklia ya Iran Umoja wa Ulaya umesema utaendelea kuheshimu makubaliano juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, na hautarejesha vikwazo dhidi ya nchi hiyo baada ya Rais Trump kuiondoa Marekani katika makubaliano hayo jana.

MTEULE THE BEST Umoja wa Ulaya umesema utaendelea kuheshimu makubaliano juu ya mpango wa nyuklia wa Iran, na hautarejesha vikwazo dhidi ya nchi hiyo baada ya Rais Trump kuiondoa Marekani katika makubaliano hayo jana. Nchi za Umoja wa Ulaya zimesema zitasimama kidete kuyatunza makubaliano juu ya mpango wa nyuklia wa Iran. Nchi za Ulaya ambazo zilihusika katika kujadili na kusaini makubaliano hayo ya mwaka 2015 kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran zinafanya kila juhudi kuyanusuru makubaliano hayo, ambayo yanakabiliwa na kitisho kikubwa kutoka na hatua ya Rais Donald Trump ya kuindoa Marekani hapo jana. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kufanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani, kumuhakikishia kwamba Umoja wa Ulaya utafanya uwezavyo kuendeleza ahueni ya kiuchumi ambayo Iran iliahidiwa ili ipunguze upeo wa mpango wake wa nyuklia. Tangazo la pamoja lililotolewa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na R...

Marekani yajiondoa mkataba wa nyuklia na Iran

MTEULE THE BEST Rais wa Marekani Donald Trump ameiondoa nchi yake kutoka kwa mkataba wa nyuklia kati ya Iran na mataifa ya magharibi, Jumanne (08.05.2018) akisema atavifufua tena vikwazo. Trump alisema mkataba huo umeoza kabisa kuanzia katika shina lake na anatumai kuafikiana makubaliano na Korea Kaskazini. Aliueleza mkataba kati ya Iran na nchi za Magharibi kuwa mbaya na unaoegemea upande mmoja. Kauli ya Trump imekuja wakati alipotangaza mipango ya kuiondoa Marekani kutoka mkataba huo wa kihistoria na Iran wa mwaka 2015 wakati wa hotuba aliyoitoa kupitia televisheni katika ikulu ya mjini Washington. Trump alisema kama angeuruhusu mkataba huo kuendelea kuwepo, kungetokea katika siku chache zijazo mashindano ya silaza hza nyuklia. Pia alisema mkataba wa maana ungeeweza kuafikiwa wakati huo, lakini hilo halikufanyika. Rais huyo wa Marekani ameieleza Iran kuwa "utawala wa ugaidi mkubwa". Trump amesema Wairan wanastahili serikali bora zaidi kuliko ile iliyopo...

Rouhani asema Marekani itajuta ikijitoa mkataba wa nyuklia

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kwamba endapo Marekani itajiondoa kwenye mkataba wa nyuklia kati ya nchi yake na mataifa yenye nguvu duniani, basi Marekani itajutia maisha yake yote. "Ikiwa Marekani itaondoka kwenye makubaliano ya nyuklia, mutaona hivi karibuni watakavyojutia kuliko ilivyowahi kuwatokezea kwenye historia," alisema mwanamageuzi Rouhani kwenye hotuba yake ya leo (Jumapili 6 Mei) akiwa kaskazini mwa Iran. "Trump anapaswa kujuwa kuwa watu wetu wameunganika, utawala wa Kizayuni (Israel) unapaswa kujuwa kuwa watu wetu wako kitu kimoja," alisema Rouhani. "Leo, mirengo yote ya kisiasa nchini Iran, ama iwe kulia au kushoto, wahafidhina, wanamageuzi na watu wa mrengo wa kati, wote wameungana," aliongeza. Rais Donald Trump wa Marekani ametishia kujiondoa kwenye makubaliano hayo wakati utakapofika muda wa kusainiwa upya tarehe 12 Mei, akiwataka washirika wa Ulaya "kuyarekebisha makosa makubwa yaliyomo" ama sivyo arejeshe upya v...

Marekani yaishutumu Iran kuvuruga amani Mashariki ya Kati

Waziri mpya wa mamabo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameishutumu Iran kwa shughuli zake katika kanda ya Mashariki ya Kati, ambazo amesema zinaivurga kanda hiyo. Katika ziara  yake ya kwanza nje ya nchi  saa kadhaa baada ya kuapishwa Mike Pompeo alikutana na viongozi wa Saudi Arabia  na Israel nchi mbili ambazo zinamahusiano maalumu ya kimkakati na Marekani na ambazo pia zina adui wa pamoja Iran  huku waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu akisisitiza kuwa makubaliano ya nyukilia na Iran lazima yabadilishwe au yavunjwe ingawa mataifa mengi makubwa duniani  yanayaona makubaliano hayo kuwa ndiyo njia inayoweza kuizuia Iran isiwe na silaha za nyukilia. Akizungumza pembezoni mwa waziri mkuu wa Israel baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa masaa mawili mjini Telaviv  waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo  alisema nia ya Iran kutaka kutawala siasa za  Mashariki ya Kati bado ipo palepale na akasema hawatapuuza vitendo hivyo vya Iran k...

Iran yaonya iko tayari kurejesha mpango wake wa kinyuklia

Iran imeonya iko tayari kurejesha mpango wake wa kutengeza silaha za kinyuklia kwa kile ilichokitaja kasi kubwa zaidi iwapo Marekani itajiondoa kutoka makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kuhusu mpango huo wa kinyuklia. Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif ameonya kuwa iwapo Marekani itajiondoa kutoka makubaliano hayo yajulikanayo JCPOA, basi nchi yake haitakuwa na budi bali kuongeza kasi shughuli zao za kinyuklia. Mapema mwezi huu, Rais wa Iran Hassan Rouhani alionya kuwa Marekani itajuta iwapo itajiondoa kutoka kwa makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya nchi sita zenye nguvu zaidi duniani na Iran yanayolenga kudhibiti mpango wa kinyuklia wa Iran na badala yake nchi hiyo ilegezewe vikwazo vya kiuchumi. Je, Marekani itajiondoa kutoka JCPOA? Rais wa Marekani Donald Trump amezitaka nchi za Ulaya kufanyia marekebisho makubaliano hayo ifikapo tarehe 12 mwezi Mei kwa kuiwekea Iran mbinyo zaidi la sivyo Marekani itajiondoa kutoka kwa makubaliano hayo yaliyofikiwa wakati wa utaw...

Urusi yaionya Marekani kutoingilia masuala ya Iran

Urusi imetoa onyo kwa Marekani kutojaribu kuingilia hali ya kisiasa nchini Iran. Urusi imetoa onyo kwa Marekani kutojaribu kuingilia hali ya kisiasa nchini Iran. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Ryabkov amekiambia kituo cha habari cha  TASS kuwa Urusi inaionya Marekani kutoingilia hali inayoendelea Iran. Kwa mujibu wa habari,Urusi inaamini kuwa hali ya Iran itarudi kuwa shwari. Urusi inaamini Marekani inajaribu kuingilia na kuharibu makubaliano ya JCPOA kati ya Iran na mataifa yenye nguvu katika suala zima la nyuklia. Hata hivyo Urusi imeahidi kusimamia na kulinda makubaliano hayo yaliyofanyika mwaka 2015. Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiandika maneno ya kuchochea maandamano nchini Iran kwa kupitia mtandao wake wa Twitter.

Saudia: Ayatollah Ali Khamenei wa Iran ni 'Hitler' mpya

Mwanamfalme wa Saudia amemtaja kiongozi wa kidini wa Iran kuwa 'Hitler' mpya wa eneo la mashariki ya kati huku kukiwa na wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili Mwanamfalme MOhammed bin Salman wa Saudia na rais Hassan Rouhani wa Iran Mwanamfalme wa Saudia amemtaja kiongozi wa kidini wa Iran kuwa 'Hitler' mpya wa eneo la mashariki ya kati huku kukiwa na wasiwasi kati ya mataifa hayo mawili. Akitaja kuongezeka kwa ubabe wa Iran katika eneo hilo, Mohammed Bin Salman amesema kuwa ni vyema kuzuia yaliotokea barani Ulaya katika eneo la mashariki ya kati. Saudia na Iran ni wapinzani na wamekuwa wakishutumiana kwa kuchochea ukosefu wa uthabiti katika eneo la mashariki ya kati. Hatahivyo hakuna tamko lolote liliotolewa na Iran kufuatia matamshi hayo ya hivi karibuni. Akizungumza na gazeti la The New York Times , Mohammed bin Salman alisema kuwa Iran haiwezi kuruhusiwa kusambaza ushawishi wake. ''Tulijifunza kutoka Ulaya kwamba kujionyesha kwamba wewe ni mtu mzuri ha...