Urusi imetoa onyo kwa Marekani kutojaribu kuingilia hali ya kisiasa nchini Iran.
Urusi imetoa onyo kwa Marekani kutojaribu kuingilia hali ya kisiasa nchini Iran.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Ryabkov amekiambia kituo cha habari cha TASS kuwa Urusi inaionya Marekani kutoingilia hali inayoendelea Iran.
Kwa mujibu wa habari,Urusi inaamini kuwa hali ya Iran itarudi kuwa shwari.
Urusi inaamini Marekani inajaribu kuingilia na kuharibu makubaliano ya JCPOA kati ya Iran na mataifa yenye nguvu katika suala zima la nyuklia.
Hata hivyo Urusi imeahidi kusimamia na kulinda makubaliano hayo yaliyofanyika mwaka 2015.
Rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiandika maneno ya kuchochea maandamano nchini Iran kwa kupitia mtandao wake wa Twitter.
Maoni