Adrien Silva: Mchezaji aliyechelewa sekunde 14 ahamia Leicester kwa £22m

MTEULE THE BEST

Adrien Silva alitajwa kwenye benchi wakati wa mechi dhidi ya Huddersfield uwanjani King Power

Kiungo wa kati wa Ureno Adrien Silva hatimaye amefanikiwa kuhamia Leicester City, baada ya kushindwa majira ya joto klabu hiyo ilipochelewa kuwasilisha nyaraka zake kwa sekunde 14.

Fifa walikataa kuidhinisha uhamisho wa mchezaji huyo wa miaka 28 kutoka Sporting Lisbon wakati huo wakisema muda wa kuhama wachezaji ulikuwa tayari umepita.

Mreno huyo amekuwa akifanya mazoezi na Leicester kipindi chote cha majira ya joto kuimarisha kiwango chake cha uchezaji.

Uhamisho wake wa £22m ulikamilishwa Jumatatu na akatajwa kwenye benchi mechi ya Leicester nyumbani dhidi ya Huddersfield.



Silva, ambaye ni mzaliwa wa Ufaransa, alitoka akademi ya Sporting Lisbon, na amekuwa kwa mikopo Maccabi Haifa na Academica.


Adrien Silva amefunga bao moja katika mechi 20 alizochezea Ureno

Amechezea Ureno mechi 20 za kimataifa na kuwafungia bao moja na aliwachezea waliposhinda Euro 2016.

Silva amesema alipitia kipindi kigumu sana miezi hiyo minne akisubiri dirisha lifunguliwe tena Januari, lakini amekuwa akitia bidii kujiweka sawa kucheza.

Hayo yakijiri, Leicester wamemuita tena kiungo wao Harvey Barnes kutoka Barnsley alikokuwa kwa mkopo tangu Agosti


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

ZIJUWE SHERIA 17 ZA SOKA

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

KUMTUMAINIA MUNGU