Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 05.01.2018


Ryan Sessegnon

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Liverpool watamruhusu Philippe Coutinho, 25, kuhamia Barcelona mwezi huu wa Januari kwa £140m. (Times)


Chelsea wanamtaka meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone achukue nafasi ya Antonio Conte katika klabu hiyo mwisho wa msimu. (Times )


Chelsea wamezidisha juhudi zao za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Everton na England Ross Barkley, 24, na pia wameulizia kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa England na West Ham Andy Carroll, 28. (Mail)




Mchezaji wa Celtic na Scotland Kieran Tierney, 20, amejumuishwa katika orodha ya mabeki wa kushoto ambao Manchester United wanawatafuta kuimarisha safu yao ya ulinzi, pamoja na kinda wa Fulham Ryan Sessegnon, 17. (Daily Record)


Paris St Germain wanatarajiwa kutoa ushindani kwa Tottenham katika kutafuta saini ya Sessegnon ambaye thamani yake imekadiriwa kuwa £30m. (Mirror)


Juventus wana imani kwamba watafanikiwa kumchukua Emre Can kutoka Liverpool bila kulipa ada yoyote mwisho wa msimu.


Klabu hiyo ya Serie A imemuahidi mchezaji huyo wa miaka 23 mshahara wa £85,000 kwa wiki. (Guardian)


Manchester United wameanzisha mazungumzo ya kuongeza mikataba ya wachezaji wane kwa mwaka mmoja. Wachezaji hao ni viungo wa kati wa Uhispania Juan Mata, 29, na Ander Herrera, 28, beki wa England Ashley Young, 32, na beki Mholanzi Daley Blind, 27. (Mirror)


Manchester United wanataka sana kumnunua beki wa kushoto wa Juventus Sandro lakini wanavunjwa moyo na Juve kutotaka kumuuza mchezaji huyo wa miaka 26. (Express)


Tottenham wanatarajiwa kutoa mikataba mipya yenye donge nono zaidi kwa mshambuliaji wa England Harry Kane, 24, na beki wa Ubelgiji Toby Alderweireld, 28. (Independent)


Marseille wanamnyatia kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere lakini mchezaji huyo wa miaka 26 anataka kusalia na Gunners. (Mail)



Jack Wilshere

Mkufunzi mkuu wa Monaco Leonardo Jardim amesema hana nia ya kumuuza mshambuliaji wake Mfaransa Thomas Lemar, 22, kwa Liverpool mwezi huu. (Liverpool Echo)


Meneja wa Paris St-Germain Unai Emery amefungua mlango kwa winga wa Brazil Lucas Moura, 25, na mwenzake wa Ufaransa Hatem Ben Arfa, 30, kuihama klabu hiyo Januari. (L'Equipe)




Mbelgiji Thibaut Courtois, 25, anakaribia kutia saini mkataba mpya Chelsea baada ya klabu hiyo kumpa ujira wa zaidi ya £200,000 kwa wiki, hatua itakayomfanya kuwa kipa anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Telegraph)


Beki wa Chelsea David Luiz, 30, anataka sana kuondoka klabu hiyo na anatumaini Real Madrid watamtaka. (Mundo Deportivo - kupitia Express)


Mkufunzi mkuu wa Newcastle Rafa Benitez anatafakari uwezekano wa kutaka kumnunua nahodha wa Watford Troy Deeney, 29. (Northern Echo)



Sandro Ramirez

Newcastle na Burnley nao wanataka kumnunua kiungo wa kati Mhispania Jonathan Viera, 28, kutoka Las Palmas. (Telegraph)


Sunderland wanakaribia kumchukua mshambuliaji mchanga wa Liverpool Ben Woodburn mwenye miaka 18 kwa mkopo. (Star)


Everton wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Nice na Ivory Coast Jean Michael Seri, 26. (Sky Sports)


Meneja wa Everton Sam Allardyce hataki kumwachilia mshambuliaji Sandro Ramirez, 22, atoke nje kwa mkono Januari lakini anasema hana usemi wowote kuhusu hilo. (Liverpool Echo)


Crystal Palace wamewasilisha ofay a kutaka kumnunua beki wa kati wa Lille Ibrahim Amadou, 24. (Sun)


Besiktas wanataka kumnunua mshambuliaji wa Leicester na Algeria Islam Slimani, 29. (Leicester Mercury)


Islam Slimani alipokuwa Sporting Lisbon

Barcelona nao wanakaribia kumchukua beki wa kati wa Palmeiras ambaye ni raia wa Colombia Yerry Mina, 23. (Marca)


Manchester City nao wamesalia makini sana kutafuta walinzi sokoni kutokana na mahitaji ya kuwa katika michuano mingi. (Manchester Evening News)



Tamko la Bayern Munich kuhusu kiungo wa kati wa Schalke Leon Goretzka limekera klabu hiyo, na kuimarisha nafasi ya Liverpool kumnunua mchezaji huyo wa miaka 22. (Star)


Meneja wa zamani wa Bundesliga Jos Luhukay ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Carlos Carvalhal klabu ya Sheffield Wednesday. (Yorkshire Post


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...