Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya UGAIDI

Shambulio la Kismayo: Mwandishi Hodan Nalayeh na watu kadhaa wafariki baada ya wapiganaji wa alshabab kuvamia hoteli Somalia

Kundi la wapiganaji wa al-shabab limetekeleza msururu wa mashambulizi katika miaka ya hivi karibuni Takriban watu saba wameuawa katika shambulio moja la hoteli kusini mwa Somalkia ikiwemo mwandishi wa runinga mwenye uraia wa Canada na Somali Hodan Nalayeh, kulingana na ripoti. Maafisa na wale walionusurika wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea muhanga aligongesha gari lililojaa vilipuzi katika Hoteli ya Asasey katika bandari ya Kismayo kabla ya washambuliaji hao kuvamia jengo hilo. Nalayeh na mumewe wameripotiwa kuwa miongoni mwa wale waliouawa. Kundi la wapinganaji la al-Shabab limekiri kutekeleza shambulio hilo. Walioshuhudia wanasema kuwa walisikia milio ya risasi baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari hilo kulipuka. Haijulikana iwapo washambuliaji hao walisalia ndani ya hoteli hiyo baada ya mlipuko huo. Afisa wa usalama Abdi Dhuhul aliambia chombo cha habatri cha AFP kwamba waziri mmoja wa utawala wa eneo hilo pamoja na wakili ni miongoni mwa waliofariki. Vyombo v...

MTANZANIA AHUKUMIWA KWENDA JELA MAISHA KENYA

: Mahakama jijini Nairobi imewahukumu washukiwa watatu wa ugaidi nchini Kenya waliopatikana na hatia ya kutekeleza shambulio la mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa. Miongoni mwa waliohukumiwa ni Rashid Charles Mbeserero anayetuhumiwa kuhusika katika shambulio hilo ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, wengine waliohukumiwa na Mtanzania huyo ni  Hassan Edin na Mohammed Abdi jina jingine Mohamned Ali Abikar ambao wao wamehukumiwa kwenda jela miaka 41 kila mmoja. Wote walipatikana na hatia ya kupanga shambulio hilo chini ya ushirikiano wa wanachama wa Kundi la Al-Shabab.Takriban wanafunzi 148 walifariki dunia katika shambulio hilo. Hukumu hiyo imepitishwa baada ya mahakama kujiridhisha kuwa watatu hao ni wanachama wa Kundi la Al-shabab kutoka Somalia

Basi la shule latekwa na kuteketezwa Italia

Basi la shule nchini Italia likiwa limeteketea kabisa Basi lililokuwa limebeba watoto wa shule wapatao 51 lilitekwa na dereva wake na kisha kutiwa moto karibu na Milan nchini Italia. Watoto hao wa shule, baadhi yao walifungwa kamba, waliokolewa baada ya kuvunjwa vioo vywa basi hilo upande wa nyuma na hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa vibaya.Watu kumi na wanne waliathiriwa na moshi uliotokana na kuteketea kwa basi hilo. Dereva wa basi hilo alikuwa na umri wa miaka arobaini na saba mwenye uraia wa nchini Italia ingawa ana asili ya kutoka nchini Senegal, inaarifiwa kwamba ametiwa nguvuni. Dereva huyo alisikika akitamba, akiwaambia waliokuwemo katika basi hilo kwamba hakuna hata mtu mmoja atakaye nusurika.Ulikuwa ni muujiza, vinginevyo yangekuwa ni mauaji ya halaiki, alinukuliwa akisema hayo mwendesha mashtaa mkuu wa mjini Milan, Francesco Greco. Mwalimu mmoja wapo alikuwa ndani ya basi wakati tukio hilo likitekelezwa, alimuelezea mtuhumiwa huyo kuwa alikuwa na silika ya hasira mar...

Putin Azungumuzia shambulio la kigaidi New Zealand

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa sababu kuu ya shambulizi la misikiti miwili New  Zealand ni kuitikisa nchi hiyo Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kuwa sababu kuu ya shambulizi la misikiti miwili New  Zealand ni kuitikisa nchi hiyo. Katika mkutano wake na wawakilishi wa jamii katika Crimea na Sevastopol, Putin amejadili mashambulizi ya kigaidi juu ya misikiti huko New Zealand. Putin alionyesha heshima yake kwa wale waliouawa katika shambulio hilo. "Lengo la mashambulizi makubwa ya kigaidi huko New Zealand ni kuitingisha nchi." alisema. Akionyesha kuwa vitendo vya kigaidi ni hatari kwa kila nchi, Putin amesema kuwa Urusi haitaruhusu mashambulizi hayo. Katika mji wa Christchurch, New Zealand, wakati wa sala ya Ijumaa, watu 50 waliuawa na gaidi aliyoshambulia misikiti miwili.

Mwanamke mmoja nchini Argentina aachiwa huru baada ya kutekwa kwa miaka 30

Mwanamke aliyeokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa miaka 30 (wapili kushoto) na mwanae wa miaka tisa wameungana na familia yao. Mwanamke mmoja raia wa Argentina ameokolewa na polisi baada ya kushikiliwa mateka kwa zaidi ya miaka 30. Operesheni ya kumnasua mwanamke huyo ilifanyika kwa ushirikiano wa polisi wa nchi za Argentina na Bolivia. Mahala ambapo alikuwa akishikiliwa mwanamke huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 45 lilikuwa halifahamiki toka miaka ya 80. Hata hivyo, mapema mwaka huu, polisi walipata taarifa kuwa alikuwa akishikiliwa katika eneo la Bermejo, kusini mwa Bolivia. Baada ya uchunguzi, polisi walifanikiwa kuitambua nyumba aliyokuwemo na kufanikiwa kumuokoa akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa. Majina ya mwanamke huyo na mtoto wake ambao waliokolewa mwanzoni mwa mwezi Disemba hayajatajwa na vyombo vya usalama. Katika taarifa iliyotolewa Disemba 25, polisi nchini Argentina wanasema walau mwanamke huyo amefanikiwa kurejeshwa na kuungana na fa...

Watu watano wauawa kwa shambulio la risasi Maryland Marekani

Polisi wakiimarisha usalama katika eneo la tukio Polisi katika jimbo la Maryland nchini Marekani wanasema watu watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio la risasi lililofanyika katika ofisi za kampuni ya Capital Gazette inayomiliki magazeti ya kila siku katika mji wa Annapolis. Wafanyakazi wa gazeti hilo wanasema mshambuliaji huyo ambaye ni mzungu anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 ambaye alijiharibu vidole vyake ili kuepusha kutambulika kwa alama za vidole alifyatua risasi hovyo kupitia mlango wa vioo. Tiyari amekamatwa na polisi. Rais Trump ametuma salam za rambirambi William Krampf ambaye ni Msaidizi mkuu wa polisi wa Anne Arundel amesema kwamba wamekuta pia vitu vilivyokuwa na muonekano wa vilipuzi na kuvidhibiti kwa haraka. Ameongeza kwamba watu zaidi ya 170 waliokuwa katika jengo hilo walisindikizwa na polisi katika kuhakikisha wanakuwa salama kutoka katika jengo hili ambalo pia lilikuwa na biashara nyingine. Kupitia mtandao wa twite...

Watu 10 wafa kwa kugongwa na gari kimakusudi nchini Canada

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau amesema shambulio hilo ni baya na la kijinga, ni moja ya mashambulizi ya kutisha zaidi katika historia ya karibuni ya Kanada. Waziri Mkuu Trudeau ameonyesha huruma zake kwa wale wanaohusika na mkasa uliotokea. Amesema raia wote wanapaswa kujisikia wako salama kutembea katika miji na miongoni mwa jamii. Bwana Trudeau amesema hali hii inafuatiliwa kwa ukaribu, na kwamba Canada itaendelea kufanya kazi na vyombo vya usalama nchini kote kuhakikisha usalama wa wananchi wake. Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau Waziri wa usalama wa umma nchini Canada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili  tahadhari katika kiwango cha mashambulizi ya kigaidi. Waziri wa usalama wa umma nchini Kanada Ralph Goodale amesema shambulio hilo ni baya na la kutisha lakini halihusiani na vitendo vya kigaidi. Waziri Goodale, amesema nchi yake haijabadili tah...