Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Marekani Donald Trump wameeleza tofauti zao kuhusiana na biashara na Jumuiya ya NATO katika mkutano wao uliofanyika katika Ikulu ya White House ambako walijaribu kuonesha hali ya uchangamfu licha ya hali ya wasi swsi baina ya washirika hao wawili. Angela Merkel akiingia Ikulu ya white House pamoja na rais Donald Trump wa Marekani Wakati Trump anakaribia kuweka ushuru katika biadhaa za chuma na bati hivi karibuni ambavyo vitaathiri mauzo ya nje ya mataifa ya Ulaya, Merkel amesema uamuzi sasa uko mikononi mwa Trump juu ya iwapo kutoa msamaha kwa mataifa ya Umoja wa Ulaya. "Tulibadilish...