Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Marekani Donald Trump wameeleza tofauti zao kuhusiana na biashara na Jumuiya ya NATO katika mkutano wao uliofanyika katika Ikulu ya White House ambako walijaribu kuonesha hali ya uchangamfu licha ya hali ya wasi swsi baina ya washirika hao wawili.
Angela Merkel akiingia Ikulu ya white House pamoja na rais Donald Trump wa Marekani
Wakati Trump anakaribia kuweka ushuru katika biadhaa za chuma na bati hivi karibuni ambavyo vitaathiri mauzo ya nje ya mataifa ya Ulaya, Merkel amesema uamuzi sasa uko mikononi mwa Trump juu ya iwapo kutoa msamaha kwa mataifa ya Umoja wa Ulaya.
"Tulibadilishana mawazo. umuazi sasa una rais," Merkel aliwaambia waandishi habari baada ya Trump kulalamika juu ya kutokuwa na uwasa katika biashara kati ya Marekani na Ulaya, hususan katika upande wa magari.
Ziara ya haraka ya Merkel inakuja wiki hiyo hiyo wakati wa ziar ya siku tatu iliyofanywa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye , kama Merkel, alizungumza na trump kuhusu biashara na kumtaka kuibakisha Marekani katika makubaliano yaliyofikiwa na matiafa kadhaa ya kinyuklia na Iran.
Hakuna kiongozi kati ya hao wawili aliyeonekana kupata mafanikio, kumshawishi Trump katika masuala hayo mawili.
Angela Merkel (kushoto) katika mazungumzo na rais Donald Trump (kulia)
Uhusiano wa kibiashara wenye uwiano
Merkel amesema anaweza kuona majadiliano ya makubaliano ya kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani, akisema shirika la biashara la dunia , WTO halijaweza kufanikisha makubaliano ya kimataifa.
Trump alisema anataka uhusiano wa kibiashara unaowiana zaidi na Ujerumani na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya na anataka Ujerumani na mataifa mengine washirika wa NATO walipie fedha zaidi kwa ajili ya ulinzi wao, suala ambalo hulizusha mara kwa mara.
Tunahitaji uhusiano wa pande zote mbili,wenye kutendeana vizuri ambao hatuna. Tunafanyakazi kufanikisha hali hiyo na tunataka kuufanya uwe wa haki zaidi na kansela anataka kuufanya uwe wa haki zaidi," trump alisema.
Merkel aliondoka Ikulu ya white House , ikionekana kwamba hakuweza kupata ahadi kutoka kwa Trump kubakia katika makubaliano ya kinyuklia na Iran ama kupata msamaha wa kudumu kwa Ulaya katika ushuru wa biashara.
Hadi pale Trump atakapochukua hatua Meo mosi, ambayo ni Jumanne ijayo, ushuru katika chuma na bati kutoka mataifa ya Ulaya utaanza kutumika, huenda ukifuatiwa na hatua za kulipiza za Umoja wa Ulaya ambazo zitazusha vita vya biashara kati ya mataifa ya Ulaya na Marekani.
Kuhusiana na makubaliano ya kinyuklia na Iran, ambayo Trump huenda akayasambaratisha Mei 12, Merkel alikiri kwamba "hayajakuwa sahihi vya kutosha" lakini ni muhimu kuendelea nayo hata hivyo.
Trump na kansela wa Ujerumani Angela Merkel
Trump alitaka "makubaliano hayo mabaya" ambayo yaliipa Tehran ahueni ya vikwazo ili kuweza kuzuwia shughuli zake zenye utata za kinyuklia, yajadiliwe upya, jambo ambalo mataifa ya Ulaya yanaona kuwa ni jambo lisilokuwa sahihi, la hatari na lisilo la lazima.
Licha ya kuwapo kwa hali ya kutokubaliana , Trump aligusia ukosoaji wake mkali wa matumizi ya chini ya ulinzi ya Ujerumani , sera za uhamiaji za kufungua milango na biashara yenye mtazamo wa mauzo ya nje. Akimsifu Merkel kuwa ni "mwanamke wa aina yake," Trump alisisitiza "ni lazima tuwe na uhusiano wa kibiashara wa haki na unaonufaisha pande zote mbili kwa marafiki zetu na washirika wetu
Maoni