Nawasalimu wa jina la YESU, jina kuu kupita majina yote. Jina langu ninaitwa Theoflida , ni mwanamke mwenye umri wa miaka 38 mkaazi wa Mbezi ya Kimara jijini Dar Es Salaam, japo kiasili ni mwenyeji wa wilaya ya Ulanga, mkoani Morogoro.. Nime amua kuandika waraka huu kwa madhumuni makuu mawili, kwanza ni kushuhudia MATENDO MAKUU ambayo YESU AMENITENDEA na pili, ni kuwa hasa wanawake wenzangu kutojihusisha kabisa na masuala ya WAGANGA WA KIENYEJI kwa sababu waganga wa kienyeji ni MAWAKALA WA KAZI ZA SHETANI HAPA DUNIANI na ni MASHETANI KABISA!... Nitaanza kwa kuelezea kisa kilicho nipelekea kuingia kichwa kichwa kwenye mikono ya wakala wa shetani.. Nilikuwa nimepanga chumba kimoja maeneo ya Tabata Mawenzi huku nikijihusisha na biashara ya genge. Jirani na nyumba niliyokuwa nimepanga, aliishi mwanaume mmoja na mke wake. Mwanaume huyu jina lake linaanzia na herufi K hivyo katika maelezo yangu nitakuwa nikimtaja kwa herufi K. K alikuwa ni mwanaume mwenye mafanikio makubwa katika mai...