Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya COLOMBIA

Kansela Angela Merkel apokea tuzo ya 'Taa ya Amani'

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametunukiwa tuzo ya Fransisca ya ‘'Taa ya Amani". Bibi Merkel amepewa tuzo hiyo kutokana na juhudi zake za kuhamasisha ushirikiano na amani miongoni mwa watu. Wakati akipokea tuzo hiyo kansela wa Ujerumani Angela Merkel alisema njia ya amani na maridhiano mara nyingi hufaulu pale panapokuwa na jitihada na uvumilivu mwingi, na alisisitiza kuwa njia hiyo sio kizuizi cha imani ya kidini. Akitolea mfano matatizo katika Umoja wa Ulaya unaojumuisha mataifa 28, bibi Merkel amesema ni muhimu kuangalia mbali zaidi ya upeo wa kitaifa, na kuongeza kuwa ni lazima uwepo uwezekano wa kuupa moyo Umoja wa Ulaya. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel Kansela wa Ujerumani alielezea juu ya amani na jinsi inavyoendelea kuwa dhaifu duniani, akitolea mfano vita vya Balkans, iliyokuwa zamani Yugoslavia kwenye miaka ya tisini.Pia alizungumzia hatua ya Urusi ya kulitwaa jimbo la Crimea  mnamo mwaka 2014 pamoja na vita vya hivi karibuni vya wenyewe kwa wenye...