Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CONGO

SIMBA KUJUA MBIVU AMA MBICHI 28/12/2018 CAIRO

mteulethebest Draw ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika (Caf Champions League) itafanyika Cairo Misri siku ya Ijumaa December 28 na klabu ya Simba itawakilishwa na mwenyekiti wa bodi Swed Kwabi. -Shirikisho hilo limepanga pot 4 kila pot ina timu 4 na kila pot itatoa timu moja kwenye kundi moja. Pot hizo zimepangwa kulingana na Parfomance ya klabu kwa miaka mitano iliyopita kwa Caf Champions League na Caf Confederation Cup. -Pot 1 ina vilabu vya TP Mazembe (DR Congo) yenye pointi 66, Al Ahly (Egypt) yenye pointi 62, Wydad Casablanca (Morocco) yenye pointi 51 na Esperance de Tunis (Tunisia) yenye pointi 45. -Pot 2 ina vilabu vya Mamelodi Sundowns (South Africa) yenye pointi 40, AS Vita Club (DR Congo) yenye pointi 29, Horoya (Guinea) yenye pointi 19 na Club African (Tunisia) yenye pointi 12. -Pot 3 ina vilabu vya ASEC Mimosas (Ivory Coast) yenye Point 8.5, Orlando Pirates (South Africa) yenye pointi 8, FC Constantine (Algeria) na FC Platinum (Zimbabw...

Moto wateketeza ghala la tume ya Uchaguzi

Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeteketeza ghala la tume ya uchaguzi nchini Congo. Sehemu ya Ghala lililoteketea, kwa moto. Inasemekana kuwa Mashine zaidi ya 7000 za kura na vifaa vingine vilikuwemo kwenye ghala hilo la Kinshasa ikiwa ni masaa kadhaa tangu Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo (CENI) ilipotangaza kupokea vifaa mbalimbali vya uchaguzi ikiwemo mashine za kupigia kura. Kampeni za kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zinaendelea baada ya kuanza rasmi Novemba 22, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 23 mwezi Desemba. Tume hiyo ya Uchaguzi ilisema kuwa imeorodhesha wapiga kura milioni 40 wanaotarajia kushiriki uchaguzi huo katika vituo vya kupigia kura 80,000 ambavyo vitakuwa na 'mashine za kupigia kura" zaidi ya 100,000. Kampeni zinaendelea wakati huu, kukiwa na mvutano mkubwa kuhusu suala la matumizi ya mashine za kupigia kura, pamoja na changamoto za kiusalama, mashariki mwa nchi hiyo. Wanasiasa wa upinzani, akiwemo mmoja wa wagombea w...

Polisi yavunja maandamano ya Kanisa DR Congo

Watu wanane wameuawa Juampili na dazeni kadhaa kukamatwa na vikosi vya usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wakati wa maandamano yalioitishwa na Kanisa Katoliki kumshinikiza rais Joseph Kabila aachie madaraka Licha ya maombi, hasa kutoka kwa Umoja wa Mataifa kuheshimu haki ya raia kuandamana, wanajeshi walifyatua hewa ya kutoa machozi ndani ya makanisa na risasi za moto hewani kuvunja mikusanyiko ya waumini wa Kikatoliki, na katika kisa kimoja waliwakamata wavulana wanaohudumu kanisani kwa kuongoza maandamano mjini Kinshasa. Mawasiliano ya intanet yalikuwa chini mnamo wakati makundi ya Kanisa na kisiasa yakikaidi amri iliyowekwa na serikali na kuendelea na maandamano hayo. "Vifo nane -- saba mjini Kinshasa na kimoja Kananga," katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, chanzo kutoka Umoja wa Mataifa kililiambiam shirika la habari la Ufaransa AFP, na kuongeza kuwa kulikuwepo na watu 82 waliokamatwa, wakiwemo mapadri, katika mji mkuu na 41 katika maeneo mengine ...