MTEULE THE BEST Chelsea wameripotiwa kuwasiliana na Paris Saint-Germain kutaka kumsajili beki Serge Aurier, 24, huku kukiwa na taarifa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anakaribia kujiunga na Manchester United. (Manchester Evening News) Inter Milan wanataka kuwapiku Manchester United na Chelsea katika kumsajili beki Serge Aurier wa PSG. (Calciomercato) Meneja wa Monaco Leonardo Jardim amedokeza kuwa Kylian Mbappe, 18, anayenyatiwa na Real Madrid, Manchester City, Barcelona na Arsenal, huenda akaondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent) Philippe Coutinho, 25, ameachwa katika kikosi cha Liverpool kitakachocheza na Athletic Bilbao siku ya Jumamosi kwa sababu ya jeraha la mgongo. Mchezaji huyo ananyatiwa na Barcelona ili kuziba nafasi ya Neymar. (Mirror) Barcelona wamewasiliana na Borussia Dortmund kuhusu mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele, 20, ili kuchukua nafasi ya Neymar. (Daily Mail) Ousmane Dembele amesema anakaribisha taarifa ...