Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 01.08.2017

MTEULE THE BEST



 


Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, hatojiunga na kikosi cha kwanza kwa ajili ya kuanza mazoezi siku ya Jumanne huku akiendelea kufuatilia uhamisho wake kuondoka Stamford Bridge. (Marca)

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ameiambia Chelsea kuwa hawatomuuza beki wa kushoto Alex Sandro, 26. (Sport Mediaset)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anataka kumsajili kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, baada ya Nemanja Matic kwenda Man Utd. (Mail)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp huenda akaamua kumfuatilia kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, 19, iwapo Philippe Coutinho, 25, ataondoka kwenda Barcelona. (Bild)

Bayern Munich wamekataa dau la pauni milioni 10 kutoka kwa AC Milan wanaomtaka Renato Sanches, 19, kwa mkopo. (Le10Sport)

Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, atakuwa na mazungumzo na meneja wake mpya Mauricio Pellegrino, wiki hii, huku Liverpool wakijiandaa kuvunja rekodi yao ya usajili kumchukua beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi. (Liverpool Echo)
Liverpool wamekataa kukata tamaa katika kumfuatilia beki wa Southampton Virgil van Dijk na watajaribu tena kufanikisha usajili huo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Mail)

Dau la euro milioni 100 kutoka kwa Barcelona kumtaka Philippe Coutinho, 25, limekataliwa na Liverpool. Barca walipanda dau jingine baada ya euro milioni 80 za awali pia kutupiliwa mbali huku Liverpool wakisisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi. (RMCSport)

Liverpool wanamnyatia kiungo wa Monaco anayesakwa pia na Arsenal, Thomas Lemar, 21. (Le 10Sport)

Inter Milan wanapanga kutoa dau la pauni milioni 35 kumtaka winga wa Liverpool Sadio Mane. (Daily Express)

Inter Milan huenda wakawazidi kete Arsenal katika kumsajili beki wa Nice, Dalbert, 23, kwa pauni milioni 17. (TMW)

Tottenham na Inter Milan zinafikiria kwanza kabla ya kutaka kumsajili beki wa Paris Saint-Germain Serge Aurier, 24, wakiwa na matumaini kuwa ada yake ya uhamisho itapunguzwa. (La Parisien)

Manchester United wamefikia makubaliano na beki wa kulia Serge Aurier, 24, wa PSG, lakini atalazimika kwanza kwenda mahakamani ili kupewa ruhusa ya kuingia Uingereza. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikutwa na hatia ya kumpiga polisi. (The Mirror)

Newcastle wanamtaka mshambuliaji Lucas Perez, 28, wa Arsenal, lakini hawapo tayari kutoa pauni milioni 13.4 wanazotaka Arsenal. (London Evening Standard)

Calgiari, Sassuolo na Verona za Italia zote zinamtaka beki wa Arsenal Carl Jenkinson, 25. (Corriere dello Sport)

Everton wataongeza bidii katika kutaka kumsajili kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, kwa kutoa pauni milioni 50 pamoja na beki Callum Connolly, 19. (Wales Online)

Wachezaji kadhaa wa Barcelona ‘wamechoshwa mno’ na sakata linaloendelea kuhusu uhamisho ambao huenda ukavuja rekodi ya dunia wa Neymar kwenda PSG, huku wengine wakiwa wamekata tamaa licha ya kumshawishi mchezaji huyo asiondoke. (SPORT)

Watford wanatarajia kukamilisha usajili wa Richardlison, 20, kutoka Fluminese katika siku chache zijazo baada ya mchezaji huyo kutoka Brazil kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza. (Hertfordshire Mercury)

Newcaste huenda wakamkosa kiungo wa Benfica Andreas Samaris, 28, mwenye thamani ya pauni milioni 17.5. (Mirrow

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...