MTEULE THE BEST
Application zinazowekwa kwenye simu za kisasa (Smartphone) zinafanya udanganyifu kwa watu walio kwenye uhusiano wa kimapenzi kuwa mgumu zaidi kubaini. Zama za mpenzi kumnasa mwenzie kilaini laini kwa kuchungulia meseji za simu au barua pepe zimeshapita.
Watu wa ‘michepuko’ siku hizi wanasaidiwa kwa kiasi kikubwa na teknolojia na imekuwa ngumu sana hata kugundulika.
App zifuatazo zinatakiwa kukutia wasiwasi kama ukiziona kwenye simu ya mpenzi wako:[img]https://www.jamiiforums.com/attachments/tinder-700x525-jpg.557722/[/img]
Utakuwa sahihi kwa asilimia 100 utaposema kwamba mpenzi wako anakagua watu wengine kama ukikuta app hii kwenye simu yake, au ni kwamba wanapenda tu kuangalia uzuri wa watu wengine.
Ashley Madison
[img]https://www.jamiiforums.com/attachments/upload_2017-8-4_10-24-57-jpeg.557723/[/img]
App hii inapatikana kwenye Google Play Store kwa watumiaji wa simu za Android na kwenye Apple App Store kwa wenye vifaa vinavyotumia iOS. Hivi karibuni, app hii ya Ashley Madison iliboreshwa uhifadhi wa taarifa za wateja wake na kufanya watumiaji wake wawe na usiri mkubwa kuliko wanaotumia mtandao wa Tinder.
OkCupid
[img]https://www.jamiiforums.com/attachments/upload_2017-8-4_10-26-5-jpeg.557725/[/img]
App inayoitwa OkCupid inamsaidia mtumiaji wa simu ya mkononi kutafuta aina ya mpenzi anayeendana naye (vitu wanavyopendelea, nk). Hii ilianza kwa kuwa tovuti na sasa wameamua kuweka app ili kuwarahisishia watumiaji wake.
Pure
[img]https://www.jamiiforums.com/attachments/upload_2017-8-4_10-26-51-png.557726/[/img]
Majina yanaweza kukuchanganya sana! Jina la app hii ni Pure: app ya kuunganisha watu wazima wanaotaka kuwa na uhusiano wa kingono, zikiwashawishi watu ‘wenye mtazamo ulio wazi’ wanaotaka kuwa na uhusiano huru wa kingono.
App hii inachohitaji ni picha ya selfie tu na ukishaiweka, mtumiaji anatumiwa ujumbe wanapotokea watu wanaotaka wawe na uhusiano wa kingono naye.
CoverMe
[img]https://www.jamiiforums.com/attachments/upload_2017-8-4_10-27-49-jpeg.557727/[/img]
App hii imejengwa kwa ajili ya kutuma ujumbe kwa lengo la kuficha ujumbe mfupi au simu unazopokea. Pia ina chaguo la kumuwezesha mtumiaji kuficha picha zilizopo kwenye simu ambapo utaziangalia kwa kuweka neno la siri tu.
Secret Photo Album
[img]https://www.jamiiforums.com/attachments/upload_2017-8-4_10-28-58-jpeg.557728/[/img]
Kama ulikuwa unapekua simu ya mpenzi wako kutafuta dalili za kuwa na mpenzi zaidi yako, utajisumbua kweli kuangalia kwenye kalkuleta ya simu? Bila shaka jibu lako ni HAPANA, na ndio sababu app hii imewekewa picha ya aina hii.
Ukishaifungua app hii mwanzo inaonekana kama kalkuleta kweli, lakini ukishaiweka neno la siri sahihi, inafunguka na kuonesha picha za siri ambazo hazionekani unapoangalia sehemu zinapohifadhiwa picha kwenye simu.
Maoni