Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya SIMBA

Mabadiliko ndani ya Simba SC Tanzania ni muamko mpya?

Mmiliki mwenza wa Simba SC Mohammed Dewji anijtahidi kuona klabu hiyo inakuwa ndani na nje ya uwanja (Picha kwa hisani ya Mahmoud Bin Zubeiry) Siku ya Jumanne mashabiki wa mojawapo wa timu kongwe Tanzania watakusanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kusherehekea "Simba Day". Ni katika kuidhinisha wiki ya Simba au kwa umaarufu "Simba Week" na inahusisha mechi ya kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia pamoja na mechi za timu za wanawake walio chini ya miaka 20. Shughuli zilizopangwa kwa siku saba zimenuiwa kuongeza ukaribu na ushirikiano baina ya wachezaji na mashabiki wa timu hiyo pamoja na Simba kuisaidia jamii kupitia miradi tofuati. Ni sehemu ya azimio la Bilionea Mohammed Dewji, mmiliki mwenza wa klabu hiyo anayeitaka klabu hiyo ikuwe ndani na nje ya uwanja ili kuhakikisha ufanisi zaidi. "Niliwahi kukutana na mojawapo ya viongozi wa Zamalek (mnamo 2003) na niligundua wakati huo kuwa bajeti ya Zamalek ni mara 50 zaidi ya baj...

Tetesi za Soka Ulaya na Afrika Jumatano 03.07.2019: Maguire, Bale, Lacazette, Cocu, Ajibu, Dembele

Alexandre Lacazette Atletico Madrid wanataka kumsajili Alexandre Lacazette kuchukua nafasi ya mshambuliaji Antoine Griezmann, 28 ambaye anaelekea Barcelona. (Mirror) United watalazimika kilipa zaidi ya pauni milioni £90 kumnunua beki wa Leicester City na England, Harry Maguire - hatua itakayomfanya kuwa nyota huyo wa miaka 26 kuwa mlinzi ghali zaidi . (Telegraph) United pia imetuma maombi ya kumnasa kiungo wa kati wa Uhispania na Dinamo Zagreb-Dani Olmo, 21. (Mail) Real Madrid wana mpango wa kumjumuisha mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, katika mkataba utakaowawezesha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mail) Gareth Bale Mlinzi wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24, huenda akatia saini mkataba wa kujiunga na Manchester City mhumu ujao. (L'Equipe, via Manchester Evening News) Crystal Palace wanafanya kila juhudi kuhakikisha hawataiuzia Arsenal winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, na wana hasiri kwa sababu wanaamini G...

Mo Dewji atuma salaam Al Ahly, Esperance na Mamelodi

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji amesema kuwa klabu hiyo itashindana na timu kubwa barani Afrika msimu ujao katika dirisha la usajili. Mohamed Dewji Akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe Jumamosi hii, Mo Dewji amesema kuwa bajeti ya klabu hiyo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku huku kutokana na kukamilika kwa mabadiliko ya mfumo wa kiuendeshaji na kupanuka kwa vyanzo vya mapato ya klabu. " Mwaka juzi ukilinganisha na mwaka jana, bajeti yetu imekuwa ikizidi kwa asilimia 60 hadi 70 na mwaka huu bajeti unazidi. Kwakuwa mabadiliko yamefanyika vizuri, tumeanza kupata vyanzo vingi vya mapato ", amesema Mo. " Kiujumla tumejitayarisha kushindana na hizi klabu kubwa na kusajili wachezaji wazuri. Tayari kuna kamati maalum ambayo inalifanyia kazi suala la usajili, kuna wachezaji wengi mikataba yao inaisha. Wengi tutaendelea nao na wengine tutawaacha. Kwahiyo tutakuwepo kwenye ...

Vilabu bingwa Afrika: Droo ya Total CAF Confederation Cup

S imba ya Tanzania na Gor Mahia ya Kenya zapewa wapinzani Droo ya kombe la Vilabu bingwa barani Afrika hatimaye imetolewa. Katika michuano hiyo klabu ya Simba kutoka nchini Tanzania imepangwa kucheza dhidi ya mabingwa wa zamani wa kombe hilo TP Mazembe wa DR Congo huku mabingwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia wakimenyana dhidi ya klabu ya S Berkane kutoka Morocco. Droo hiyo iliofanyika siku ya Jumatano katika mji wa mkuu wa Misri, Cairo iliwakutanisha mabingwa hao huku safari ya michuano hiyo ikielekea kufika ukingoni. Baadhi ya magwiji wa kandanda waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na naibu katibu mkuu wa CAF Anthony Baffoe, chini ya usaidizi wa mshambuliaji wa zamani wa Cameroon Patrick Mboma pamoja na Emad Moteab kutoka Misri. Pia baadhi ya waliohudhuria walikuwa wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki. Jinsi Simba na Gor  M ahia zilivyotinga robo fainali Katika hatua ya kuelekea robo fainali klabu ya Simba ya Tanzania ilivunja mwiko wa miaka 25 baada ya kuilaza klabu ya Vit...

BAKULI LA YANGA LAENDELEA ILI WAWEZE KUPATA NAULI YA KUPANDA NDEGE

Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wake wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City Jumapili hii hivyo kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amewaomba wanachama kuichangia timu ili iweze kufafiri kwa ndege na kiasi kitakachopelea yeye ataongezea. Kikosi cha Yanga Zahera ambaye hayupo nchini amedai kitendo cha timu kusafiri tarehe 27 na kwenda kucheza tarehe 29 sio rahisi kwenda kwa basi hivyo ni lazima iende kwa ndege ili iweze kupata matokeo. ''Mimi kocha Mwinyi Zahera naomba wanachama waichangie klabu iweze kusafiri kwa ndege kwenda Mbeya ili tukacheze na tupate matokeo na mimi binafsi nitaongezea kiasi kitakachopelea'', amesema Zahera. Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera Aidha Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo amesema matokeo ya Yanga ni muhimu kwa wanachama na timu nzima ili kuendelea kuongoza ligi kwahiyo kila mmoja anayo sababu ya kuhakikisha timu inasafiri vyema. Yanga kwasasa inaongoza ligi ikiwa na alama 47 kwenye ...

SIMBA KUJUA MBIVU AMA MBICHI 28/12/2018 CAIRO

mteulethebest Draw ya makundi ya kombe la klabu bingwa barani Afrika (Caf Champions League) itafanyika Cairo Misri siku ya Ijumaa December 28 na klabu ya Simba itawakilishwa na mwenyekiti wa bodi Swed Kwabi. -Shirikisho hilo limepanga pot 4 kila pot ina timu 4 na kila pot itatoa timu moja kwenye kundi moja. Pot hizo zimepangwa kulingana na Parfomance ya klabu kwa miaka mitano iliyopita kwa Caf Champions League na Caf Confederation Cup. -Pot 1 ina vilabu vya TP Mazembe (DR Congo) yenye pointi 66, Al Ahly (Egypt) yenye pointi 62, Wydad Casablanca (Morocco) yenye pointi 51 na Esperance de Tunis (Tunisia) yenye pointi 45. -Pot 2 ina vilabu vya Mamelodi Sundowns (South Africa) yenye pointi 40, AS Vita Club (DR Congo) yenye pointi 29, Horoya (Guinea) yenye pointi 19 na Club African (Tunisia) yenye pointi 12. -Pot 3 ina vilabu vya ASEC Mimosas (Ivory Coast) yenye Point 8.5, Orlando Pirates (South Africa) yenye pointi 8, FC Constantine (Algeria) na FC Platinum (Zimbabw...

TFF YA THIBITISHA TIMU HAZIJAPEWA PESA ZA UBIGWA

'Simba na Mtibwa hazijapewa fedha za ubingwa'' Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa katibu Mkuu wake, Kidao Wilfred, limeweka wazi kuwa mabingwa wa michuano ya kombe la shirikisho nchini, ambao ni Simba na Mtibwa Sugar bado hawajapewa fedha za ubingwa. Wachezaji wa Simba walipokabidhiwa ubingwa wa ligi kuu. Akionge leo na wana habari Kidao amefafanua mambo mbalimbali likiwemo hilo la fedha za zawadi ya mashindano hayo ambapo ameweka wazi kuwa hata Simba bado hawajapewa. ''Ni kweli Mtibwa Sugar hawajapata fedha zao milioni 50 za ushindi wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) msimu uliopita 2017/18 lakini hata Simba ambao ni mabingwa wa msimu wa 2016/17 nao hawajapata kuna vitu tunaweka sawa'', amesema. Kidao amesema kwamba sababu kubwa ni kuwa kuna vitu vya kimkataba baina yao na wadhamini vinafanyiwa marekebisho kutokana na uongozi kuwa mpya madarakani hivyo kuna mapitio ya kuboresha vipengele vya mkataba na fedha hiz...

Simba yaicharaza Mbabane Swallows FC Kipigo cha mbwakoko

Timu ya Simba imeanza vizuri kwenye mashindano ya Ligi ya mabingwa Afrika kwakuapiga Mbabane Swallows FC 4-1 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.  Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 7 akimalizia pasi ya Nicolus Gyan kisha akafunga bao la pili dakika ya 32 kwa mkwaju wa penati baada ya Emmanuel Okwi kuchezewa rafu na mlinda mlango wa Mbabane.  Mbabane waliweza kutikisa nyavu za Simba dakika ya 24 lililofungwa na Guevane Nzambe na kufanya kipindi cha pili kumalizika kwa bao 2-1.  Simba walirejea kwa kasi kipindi cha pili na kufanikiwa kufanya mashambulizi na wakafunga bao la 3 lililofungwa na Meddie Kagere dakika ya 83 baada ya mlinda mlango wa Mbabane kuteleza akiwa na mpira kisha dakika ya 90 Clatous Chama alifunga bao la 4 akimalizia pasi ya Hassan Dilunga.  Simba watatakiwa wasiruhusu bao wakienda ugenini ili waweze kusonga mbele katika hatua ya michuano hii kwa kuwa Mbabane sio timu ya kubeza

Patrick Aussems akabidhiwa jina la mshambuliaji wa Al Hilal

Kocha wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems ameweka wazi kuwa amekabidhiwa jina la mshambuliaji Thomas Ulimwengu.  Ulimwengu ambaye amevunja mkataba wake na Al Hilal ya Sudan anatajwa kutakiwa na Simba kwa ajili ya kumtumia kwenye michuano ya kimataifa.  Mshambuliaji huyo alikuwa na Taifa Stars nchini Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa Afrika lakini hakuweza kucheza kutokana na kocha mkuu wa timu hiyo, Mnigeria, Emmanuel Amunike kumuweka benchi.  Ulimwengu amecheza mechi mbili tu chini ya Amunike ambazo zilikuwa ni dhidi ya Uganda na ile mechi ya kwanza ya Cape Verde, hivyo Mbelgiji alitegemea amuone akicheza na Lesotho lakini haikuwa hivyo.  Awali chanzo makini kutoka ndani ya Simba, kililiambia Championi Jumamosi kuwa, klabu hiyo ilikuwa kwenye mchakato wa kutaka kumsaini lakini kwa sasa inaonekana kama unaelekea kukwama kutokana na kocha kutomuona Ulimwengu akicheza licha ya kuambiwa ni mchezaji mzuri.  “Usajili wa Ulimwengu ba...

Klabu bingwa Africa: Kinnah Phiri kuwinda Simba

Mbabane Swallows wamkabidhi Kinnah Phiri  mtihani wa Simba Kocha wa zamani wa Mbeya City, Kinnah Phiri amekabidhiwa jukumu la kuiongoza klabu ya Mbabane Swallows katika mechi dhidi ya Simba. Phiri amepewa jukumu hilo la muda mfupi kutokana na kocha mkuu wa Mbabane Swallows, Thabo Vilakati kutumikia adhabu ya kifungo cha mechi nne kutoka CAF kwa kosa la kumpiga muokota mpira. Simba itapambana na Mbabane Swallows katika mechi ya raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumatano.

Simba: Lipuli FC Tunaikumbuka vizuri sana

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amesema kuwa timu yake imekiri kuwa bado wanakumbukumbu nzuri na namna ambavyo Lipuli ilivyokuwa klabu pekee iliyogoma kufungwa na Simba katika mechi zote mbili msimu uliopita.  Akiongea kuelekea mchezo wao wa ligi kuu kesho utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam, Manara ameweka wazi kuwa kocha wao Patrick Aussems anatambua uwezo wa Lipuli FC hivyo ameandaa kikosi kwaajili ya kusaka alama 3 na si vinginevyo.  ''Tunawajua Lipuli vizuri na tunafahamu ndio timu pekee iliyopata sare pacha msimu uliokwisha wa ligi lakini Simba ndio bingwa wa taifa hili na tunaingia kesho tukiwa kamili hivyo mashabiki wa Simba waje Taifa kesho saa kumi waone mpira wa raha kutoka kwa kocha wetu Aussems'', amesema.  Kwa upande wa Lipuli Fc kupitia kwa msemaji wao Festo Sanga wamesema wamejiandaa vyema kwaajili ya kushindana kutafuta alama 3 dhidi ya wenyeji wao Simba.  Msimu uliopita Lipuli haikufungwa na Simba baada ya kutoka sare ya...

Maneno ya Manara kwa Rostam 'Ukiingia Yanga unaanza kulipa madeni kama yote'

Baada ya Rostam Aziz kusema yeye ni shabiki wa timu ya mpira ya Yanga alipoulizwa na Rais na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.  Hatimaye Msemaji wa timu ya Simba,  Haji Manara amemuomba Rostam kuisaidia timu ya Yanga.  Manara kupitia ukarasa wake wa Instagram amesema kuwa Yanga walivyo na njaa akiingia ataanza kulipa madeni kama yote na mishahara.  "Sasa Shekh Rostam kwa kuwa umedeclere leo mbele ya bwana mkubwa kuwa ww ni Yanga na hali zao ni taabani sana kiasi cha kumlilia mtu aendelee kuwaongoza!! Hebu njoo huku kwenye mpira basi, au ww Yanga jina tu," aliandika Manara.  Aliongeza "Na walivyo na njaa ukiingia tu unaanza kulipa madeni kama yote na mishahara!!  Nategemea povu la kufa mtu toka Mbuteni."

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 30.10.2018

: Mauricio Pochettino, Antonio Conte, Loris Karius, Divock Origi, Jose Mourinho, Ousmane Dembele, Cristiano Ronaldo Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, amesema aliihama Real Madrid na kujiunga na Juventus kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania Florentino Perez hakumfanya ajihisi kama mchezaji anayethaminiwa na kudhaminiwa sana. (L'Equipe, kupitia Express) Real Madrid wanamtaka meneja wa sasa wa Tottenham Mauricio Pochettino awe meneja wao mpya wa kudumu kufikia mwisho wa mwezi huu. Miamba hao wa Uhispania walimfuta kazi Julen Lopetegui baada yake kuhudumu kwa miezi minne na nusu Jumatatu. Alifutwa baada ya Madrid kuchapwa 5-1 na Barcelona Jumapili. (Sun) Mazungumzo ya Real na kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ya kumtaka achukue mikoba ya ukufunzi Madrid yamekwama. Hii ndiyo sababu iliyochangia Santiago Solari ambaye ni mkufunzi wa timu ya akiba kuwekwa kwenye usukani. Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji Roberto Martinez ni miongoni mwa wanaopigiwa u...

Bilioni 20 za Mo kwa Simba zapangiwa matumizi

Mohammed Dewji ambaye ni mmiliki wa asilimia 49 ya hisa za klabu ya Simba. Mgombea pekee wa nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba Swed Mkwabi, ameweka wazi mipango yake na kuomba wanachama wa klabu hiyo wamchague.  Kampeni za uchaguzi huo wa Simba utakaofanyika November 4, 2018, zimefunguliwa rasmi jana, na leo Mkwabi ameweka wazi mipango yake kwa kusema atahakikisha pesa ya uwekezaji bilioni 20 itakayotolewa na Mohammed Dewji inaongezeka maradufu.  ''Bilioni 20 ni pesa nyingi lakini inahitaji weledi mkubwa wa kuifanya endelevu, inaweza ikachotwa ndani ya miaka mitatu ikaisha tukashindwa kuzalisha tena tukarudi tulikotoka kwa hiyo kama nitapata fursa kwa kushirikiana na wenzangu tutatengeneza misingi ya kibiashara kuitoa katika bilioni 20 kuifanya iwe zaidi'', ameeleza.  Aidha Mkwabi amesema kuwa ameshagundua wanachama wa Simba wanataka wajumbe wenye mtazamo wa kimaendeleo kwa ajili ya Simba na anaamini wanajua kuchuja mjumbe gani anafaa na yupi hafai hivyo hat...

Serikali yagomea wapelelezi wa nje kuchunguza sakata la MO Dewji

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Serikali haiwezi kuruhusu vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nje ya nchi kuchunguza tukio la kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’.  Masauni ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 16, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari.  Amesema anaamini polisi kuna wataalamu wanaoijua kazi yao, wanaifanya kwa kuzingatia maadili.  “Kuna haja gani kuleta vyombo vya nje wakati tuna jeshi bora na lenye uelewa mkubwa licha ya kukabiliwa na changamoto za hapa na pale,” amesema.  Amesema  polisi hawajashindwa kuchunguza jambo hilo na lipo ndani ya uwezo wao.  Alipoulizwa kuhusu familia ya Mo Dewji kutangaza dau la Sh1bilioni kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kupatikana kwa mfanyabiashara huyo, Masuani amesema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa si msemaji wa familia. Hata hivyo, amesema wananchi wana nafasi ya kutoa taarifa kwa polisi  ili wawe...

Mbaya wa Yanga alia hali ngumu, " Nakiona cha moto"

Mrundi wa Stand United aliyewapiga Yanga hat trick kwenye Uwanja wa Taifa, Alex Kitenge amekiri kwamba hali yake ni ngumu na anakiona chamoto.  Lakini habari ya kushtua ni kwamba tangu awapige Yanga kwenye mechi iliyomalizika kwa ushindi wa mabao 4-3 Jangwani, hajatumbukiza tena nyavuni mpaka leo.  Kacheza michezo minne bila kufunga hata bao la kuotea kati ya sita waliyocheza Stand.  “Mabeki wengi wamekuwa hawanipi nafasi ya kukaa na mpira nafikiri hii inatokana na kuwafunga Yanga mabao matatu, na kipindi nakuja nilikuwa mgeni wengi walikuwa hawanijui lakini sasa wameshaujua ubora wangu, ila nitajitahidi nirudi kwenye mbio za kuwania ufungaji bora kwa sababu hakuna ligi ambayo nimecheza nikakosa kuwa katika tatu bora ya ufungaji bora,’’ alisema Kitenge

Simba yawajibu wanaobeza usajili wao

Klabu ya soka ya Simba imesema inafanya usajili kutokana na mapendekezo ya benchi la ufundi, matakwa ya timu na ushiriki wa mashindano kwa msimu ujao na si pesa walizonazo, au kulipa kisasi kwa watani zao Yanga kama inavyosemwa sasa. Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara. Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaama na Msemaji wa timu hiyo Haji Sunday Manara, wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi za timu hiyo. Manara amesema wachezaji waliokuwepo wamefanya kazi kubwa hivyo kwa hali ya msimu ujao wanahitaji watu wa ziada, wenye uzoefu kwaajili ya kuongeza nguvu zaidi. “Kwa wachezaji wa ndani ukimtoa Kaseja, Dida ndio golikipa aliyecheza mechi nyingi za kimataifa, hivyo Pascal Wawa amekuja kuziba pengo la Juuko aliye kwenda Afrika ya kusini kwa majaribio, Kagere tunaye kwasababu ya kuwasaidia Okwi na Bocco kila mtu anaujuwa uwezo wake” , a mesema Manara. Mpaka sasa Simba imekamilisha Usajili wa wachezaji sita wapya wane wa ndani na wawili wa kimat...

Simba yawaacha nyota wake 

Kikosi cha Mabingwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC kimeondoka asubuhi ya leo Mei 31, 2018 kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya michuano ya Sportpesa Super Cup huku ikiwaacha nyota wake wanne bila ya kuwepo sababu maalum ya kufanya hivyo. Hayo yamebainika mara baada ya uongozi wa timu hiyo kukiweza wazi kikosi chenye jumla ya wachezaji 18 ambacho kimeondoka nchini bila ya kuwajumuisha Emmanuel Okwi, John Bocco, James Kotei pamoja na Nicholas Gyan. Hata hivyo eatv.tv ilifanya jitihada za kuutafuta uongozi wa Simba SC ili iweze kujibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na mashabiki wa timu hiyo kuhusiana na kikosi kizima kilichosafiri lakini kwa bahati mbaya juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda. Aidha, Kikosi kilichosafiri leo kimeongozwa na Aisha Manula, Said Mohamed, Ally Salim, Ally Shomary, Paul Bukaba, Erasto Nyoni, Yusufu Mlipili, Mohamed Hussein, Jonas Mkude. Wengine ni Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin, Marcel Kaheza, Moses Kitandu, Rashid Juma, Said Hamis Ndemla, Harun...

Simba na Yanga kuisaka mechi ya 4 msimu huu

Klabu za soka za Simba na Yanga zinaweza kukutana kwa mara ya nne msimu huu, endapo zitafuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya (SportPesa Super Cup) ambayo inafanyika katika msimu wake wa pili safari hii ikiwa nchini Kenya. Vigogo hao wa soka ya Tanzania watatakiwa kushinda mechi zao za kwanza za michuano hiyo wakianzia Robo Fainali ambapo Simba SC atacheza na Kariobangi Sharks Juni 3 na Yanga wakikipiga na Kakamega Homeboys Juni 4. Kwa msimu huu, tayari Simba na Yanga zimekutana mara tatu, wakianza Agosti 23 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mwaka 2017, mechi ambayo humkutanisha bingwa wa VPL na bingwa wa Kombe la FA. Katika mchezo huo Simba ilishinda kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 0-0. Timu hizo tena zilikutana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Oktoba 28, 2017 na kutoka sare ya 1-1, Simba wakitangulia kwa bao la Shiza Kichuya dakika ya 57, kabla ya Obrey Chirwa kuisawazishia Yanga dakika ya 60. Mechi ya tatu ilipigwa Aprili 29, mwaka huu ambapo bao la mlinzi, Erasto Edw...

Waangalizi huua Simba 250 kila mwaka nchini Tanzania

Afisa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) Dk. Dennis Ikanda alisema idadi ya simba ilianguka kutoka karibu 25,000 mwaka 2010 hadi 16,000 sasa.  Dodoma. Jumla ya viunga 250 huuawa kila mwaka nchini Tanzania na wachungaji wanaotisha hofu ya kutoweka kwa "mfalme wa jungle" katika nchi katika siku zijazo inayoonekana. Afisa kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) Dk. Dennis Ikanda alisema idadi ya simba ilianguka kutoka karibu 25,000 mwaka 2010 hadi 16,000 sasa. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani Dr Ikanda alibainisha kuwa Tanzania bado inajiunga na idadi kubwa ya simba za nchi nyingine yoyote lakini ikiwa mwenendo wa poaching una wasiwasi. Mada ya Siku ya Wanyamapori ya Dunia ilikuwa "Panya Kubwa: Wadudu Wa Chini" na ilikuwa na lengo la kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kulinda paka kubwa. Kuhusu asilimia 80 ya simba huishi katika bustani za kitaifa, Dr Ikanda alibainisha, lakini ni asilimi...