Kikosi cha Mabingwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC kimeondoka asubuhi ya leo Mei 31, 2018 kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya michuano ya Sportpesa Super Cup huku ikiwaacha nyota wake wanne bila ya kuwepo sababu maalum ya kufanya hivyo.
Hayo yamebainika mara baada ya uongozi wa timu hiyo kukiweza wazi kikosi chenye jumla ya wachezaji 18 ambacho kimeondoka nchini bila ya kuwajumuisha Emmanuel Okwi, John Bocco, James Kotei pamoja na Nicholas Gyan.
Hata hivyo eatv.tv ilifanya jitihada za kuutafuta uongozi wa Simba SC ili iweze kujibu baadhi ya hoja zilizoibuliwa na mashabiki wa timu hiyo kuhusiana na kikosi kizima kilichosafiri lakini kwa bahati mbaya juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda.
Aidha, Kikosi kilichosafiri leo kimeongozwa na Aisha Manula, Said Mohamed, Ally Salim, Ally Shomary, Paul Bukaba, Erasto Nyoni, Yusufu Mlipili, Mohamed Hussein, Jonas Mkude.
Wengine ni Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin, Marcel Kaheza, Moses Kitandu, Rashid Juma, Said Hamis Ndemla, Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya pamoja na Mohamed Ibrahim.
Simba SC wanatarajiwa kufungua dimba na Kariobangi Sharks Juni 3, 2018 kabla ya mahasimu wao wa jadi, Yanga kuvaana na Kakamega Homeboys Juni 4, mechi zote zikichezwa uwanja wa Afraha, Nakuru, Gor Mahia itaanza na JKU Juni 3, wakati Singida United itaanza na AFC Leopards Juni 5.
Maoni