Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KOREA KASKAZIN

Korea Kaskazini 'yaiba mabilioni kutengeza makombora'

Korea Kaskazini inasema jaribio la hivi karibuni la makombora yake ni onyo kwa Marekani na Korea Kusini Korea Kaskazini imeiba dola bilioni mbili (£1.6bn) kufadhili mpango wake wa silaha kupitia uvamizi wa kimtando, inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyovuja. Ripoti hiyo ya kisiri inasema Pyongyang inalenga mabenki na na ubadilishanaji wa sarafu ya crypto-currency kukusanya pesa. Vyanzo vya habari vimethibitishia BBC kwamba UN ilikuwa ikichunguza mashambulio 35 ya kimtandoa. Korea Kaskazini ilifyetua makombora mawili siku ya Jumanne ikiwa ni mara ya nne imechukua hatua hiyo katika kipindi cha chini ya wiki mbili Katika taarifa, Rais wa nchi hiyo Kim Jong-un amesema hatua hiyo ni onyo dhidi ya mazoezi ya pamoja ya kijeshi yanayofanywa na Marekani na Korea Kusini. Pyongyang imeelezea kuwa mazoezi hayo yanakiuka mkataba wa amani. How could war with North Korea unfold? Ripoti t iliyovuja na ambayo ilitumwa kwa kamati ya vikwazo vya Korea Kaskazini katika Baraza Kuu...

KOREA KASKAZINI YA TOA ONYO KALI KWA KOREA KUSINI

Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Korea Kusini kwamba ni vigumu kujilinda dhidi ya kombora lake jipya Korea kaskzini ilirusha makombora yake mawili katika bahari ya Japan Korea Kaskazini imetaja majaribio ya makombora yake mapya siku ya Alhamisi kuwa onyo rasmi dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa Korea Kusini. Kombora hilo la masafa mafupi lilirushwa katika bahari ya Japan , pia ikijulikana kama bahari ya magharibi kutoka Wonsan katika pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini. Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un alisema kuwa taifa lake lililazimika kuunda silaha ili kukabiliana na tishio la moja ka moja. Amesema kuwa jaribio hilo lilishirikisha mfumo wa kiufundi wa kuelekeza makombora. Matamshi ya bwana Kim yalioripotiwa katika vyombo vya habari yanajiri baada ya Korea Kaskazini kukosoa uamuzi wa Korea Kusini na Marekani kushiriki katika zoezi la pamoja la kijeshi mwezi ujao. Korea Kaskazini imetaja zoezi hilo la kijeshi kama maandalizi ya kulivamia taifa hilo. Ijapokuwa ...

KOREA KASKAZINI YA RUSHA MAKOMBORA

Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa mafupi baharini Haijulikani iwapo Kim Jong Un alisimamia uzinduzi huo Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa mafupi baharini kulingana na mkuu wa wafanyikazi wa umma nchini Korea Kusini. Makombora hayo yalizinduliwa mapema siku ya Alhamisi , yakisafiri umbali wa kilomita 430 na kupaa angani umbali wa kilomita 50 kabla ya kuanguka katika bahari ya Japan , ambayo pia inajulikana kama bahari ya mashariki. Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kukasirishwa na mipango ya zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Marekeni na Korea Kusini linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao. Korea Kaskazini imeonya kwamba mazoezi hayo yatarudisha nyuma mazungumzo ya taifa hilo kutojihami na silaha za kinyuklia. Kombora la kwanza lilirushwa mwendo wa saa 05.34 mapema alfajiri na la pili mwendo wa 5.57 kulingana na Korea Kusini. Makombora hayo yalirushwa karibu na mji wa Wonsan. Haijulikani iwapo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un alisimamisha uzinduz...

RUSSIA NA CHINA ZAFANYA DORIA YA PAMOJA MAREKANI YALIA

Doria ya pamoja ya Urusi - China yazua tumbo joto Japan na Korea Kusini Korea Kusini ilisema kuwa ndege ya kijeshi ya Urusi aina ya A-50 ilikiuka anga yake mara mbili Urusi inasema kuwa imetekeleza doria yake ya kwanza ya pamoja na China , hatua iliyozifanya Korea Kusini na Japan kutuma ndege za kivita angani. Waziri wa ulinzi nchini Urusi amesema kuwa ndege nne aina ya bombers zikisaidiana na zile za kivita zilipiga doria katika njia ambayo hazikupangiwa kupitia katika maji ya Japan na bahari iliopo mashariki mwa China. Korea Kusini inasema kuwa ndege zake zilirusha makombora ya kutoa onyo wakati ndege za kijeshi za Urusi zilipoingia katika anga yake. Japan imelalamika kwa Urusi na Korea Kusini kwa tukio hilo. Kisa hicho kilitokea juu ya visiwa vinavyozozaniwa vya Dokdo/Takeshima ambavyo vinamilikiwa na Korea Kusini lakini Japan pia inadai kuwa vyake. Korea Kusini inasema kuwa ndege za kijeshi za Urusi na China ziliingia katika anga yake ilio na ulinzi mkali ya KADIZ ...

Rais wa Syria Bashar al- Assad kutembelea Korea Kaskazini

Kauli ya Assad imeripotiwa kutolewa a;ipokutana na Balozi mpya wa Korea Kaskazini nchini Syria Rais wa Syria, Bashar al-Assad anapanga kutembelea nchini Korea Kaskazini,Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeeleza. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuhodhi ziara ya Kiongozi wa nchi tangu alipoingia marakani mwaka 2011 Hivi karibuni amekuwa na shughuli nyingi za kidiplomasia, kukutana na Rais wa China mwezi Mei na anatarajiwa kuhudhuria mkutano na Donald Trump mwezi huu Syria, mshirika wa Korea Kaskazini, haijasema lolote kuhusu mpango huo unaoripotiwa. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishutumiwa kushirikiana katika mapngo wa kutumia silaha za kemikali.Lakini nchi hizi zimekana shutuma hizo Tarehe ya ziara hiyo haijawekwa wazina vyombo vya Korea Kaskazini. Vilimnukuu bwana Assad siku ya Jumatano akisema ''ninakwenda kutembelea Korea Kaskazini na kukutana na Kim Jong-un." Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi...

Mkutano wa Singapore bado utafanyika Juni

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ataondoa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea na kuhudhuria mkutano wa Singapore Juni 12 wa kukutana  na Rais wa Marekani Donald Trump. Katika mkutano wa ghafla wa Jumamosi, Moon na Kim wamekubaliana kwamba mkutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini lazima ufanyike, kama Moon alivyosema katika mkutano wake na waandishi habari, mjini Seoul. "Mimi na mwenyekiti Kim tumekubaliana kwamba mkutano wa kilele wa Juni 12 lazima ufanyike kwa ufanisi, na jitihada yetu ya kupatikana rasi ya Korea isiyo na silaha za nyuklia, na utawala wa amani wa kudumu haipaswi kusimamishwa," amesema Moon. Rais wa Marekani Donald Trump kwa upande wake ameashiria kwamba maandalizi ya mkutano wa kilele wa Juni 12 yanaendelea, licha ya kuufuta mkutano huo wiki iliyopita. Mkutano huo kati ya viongozi wa Korea mbili ni mabadiliko ya hivi karibuni, katika wiki iliyogubikwa na misukosuko ya kidiplomasia kuhusi...

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla Viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana eneo lenye ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huo ndio wa pili kati ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un. Unafanyika wakati pande hizo zinaendelea na jitihada za kuufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Siku ya Alhamisi Rais wa Marekani Donald Trump alifuta mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni lakini baadaye akasema kuwa unaweza kufanyika, Mazungumzo hayo yalifanyika upande wa Korea Kaskazini katika kijiji kinachojulikana kama Panmunjom. Bw Moon atatangaza matokeo ya mkutano huo siku ya Jumapili asubuhi. Mazungumzo kati ya Bw Trump na Kim ikiwa yatafanyika yatajikita zaidi katika kuondolewa silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea na kumaliza misukosuko

Trump asema Korea Kaskazini imetoa majibu ya "ukarimu", "ufanisi"

Rais Donald Trump Rais Donald Trump amesema Ijumaa asubuhi kuwa Korea Kaskazini imetoa mrejesho wa “ukarimu” na “ufanisi" baada ya kusitisha mkutano wake na Kim Jong Un. “Ni habari nzuri sana kupokea kauli ya mrejesho ya upole na ufanisi kutoka Korea Kaskazini,” Trump amesema katika ujumbe wa Twitter Ijumaa asubuhi. “Hivi karibuni tutafahamu kile kitakachoendelea, ni matumaini yangu itakuwa ni utajiri na amani ya kudumu na ya muda mrefu. Ni wakati peke yake (na kipaji) utatuthibitishia hili. Korea Kaskazini imesema Ijumaa bado iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani” wakati wowote, [katika] mpangilio wowote.” Makamu Waziri wa Mambo ya Nje Kim Kye Gwan, mwakilishi katika mazungumzo ya nyuklia wa muda mrefu na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu, amesema katika tamko lililotangazwa na shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini iko “tayari kuipa Marekani muda na fursa” kufikiria suala la mazungumzo. Trump alijitoa ...

Korea Kaskazini yasema iko tayari kuzungumza na Marekani

Korea Kaskazini yasema bado ipo tayari kuzungumza na Marekani hata baada ya rais Donald Trump kuuvunja mkutano huo wa kilele kati yake na Kim Jong Un. Rais Trump alieleza hapo jana kwamba hatakutana na Kim Jong Un na sababu aliyoitoa ni kuwepo mazingira ya ghadhabu na uhasama wa wazi. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Kim Kye Gwan amesema nchi yake imesikitishwa na uamuzi huo wa Marekani. Mkutano huo ulionekana kama fursa ya kihistoria kwa Marekani kuweza kuishawishi Korea Kaskazini kuacha mpango wake wa silaha za nyuklia na siku ya Alhamisi, waandishi wa habari wa kimataifa walishuhudia Korea Kaskazini ilipokifunga kituo chake kikuu cha kufanyia majaribio ya nyuklia. Wakati Korea Kaskazini ilipotoa kauli kali dhidi ya makamu wa rais wa Marekani Mike Pence na mshauri wa masuala ya usalama wa Rais Trump, John Bolton, kauli hiyo ndio ilikuwa sababu ya Trump kuuvunja mkutano huo wa kilele kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Kiongoz...

Korea Kaskazini yamuita 'mjinga' Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence

Korea Kaskazini yamuita Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence 'mjinga' Afisa wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini amemlaumu Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence kwa kuwa "mjinga" na kuonya kuwa kutakuwa na maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo yatafeli. Choe Son-hui alisema Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa mazungumzo. Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa. Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumanne alisema Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo. Choe Son-hui amehusika kwenye mazungumzo mara kadha na Marekani kwa karibu miaka kumi iliyopita. Silaha za nyuklia zimekuwa ajenda kuu kwa miaka mingi kwa Korea Kaskazini Alimuita Mike Pence mjinga kwa kuifananisha Korea...

Kim Jong-un atishia kufuta mkutano wake na Trump

Korea Kaskazini imesema huenda ikaufuta mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia. Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa hamu kati ya Bw Trump na Bw Kim unatarajiwa kufanyika mnamo 12 Juni. Hayo yamejiri baada ya Korea Kaskazini kusema imejitolea kuhakikisha silaha za nyuklia zinaondolewa katika rasi ya Korea. Maandalizi ya mkutano huo wa Trump-Kim yamekuwa yakiendeleza, lakini sasa kumeingia shaka kuhusu hilo. Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limemnukuu naibu waziri wa mambo ya nje Kim Kye-gwan akisema iwapo Marekani "itatubana na kusisitiza kwamba ni lazima tusalimishe bila masharti silaha zetu za nyuklia basi hatutakuwa tena na hamu ya kushiriki mazungumzo hayo na itatulazimu kutafakari upya iwapo tutakubali mkutano unaotarajiwa kufanyika karibuni kati ya DPRK-US. Korea Kaskazini kir...

Korea Kaskazini imewaacha huru raia watatu wa Marekani

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Mike Pompeo, mwanadiplomasia wa Marekani alikutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini Korea Kaskazini imewaachia huru raia watatu wa marekani kutoka gerezani, ukurasa wa tweeter wa Rais wa Marekani Donald Trump umeeleza. hatua hiyo inaonekana kama dalili njema kuelekea mkutano wa kihistoria kati ya Rais Trump na mwenzie wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. Bwana Trump amesema atawakaribisha watu hao watakaporejea na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo ambaye amekuwa mjini Pyongyang kufanya maandalizi ya mazungumzo hayo. Kim Hak-song, Tony Kim and Kim Dong-chul walikuwa kifungoni baada ya kukutwa na hatia ya kufanya vitendo viovu dhidi ya serikali. Rais Trump ametangaza kuachiwa kwao siku ya Jumatano. Ruka ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump ''Afya yao inaonekana kuwa nzuri'', aliandika pia tarehe na mahali ambapo mazungumzo yatafanyika Haki mili...

Marekani yajiondoa mkataba wa nyuklia na Iran

MTEULE THE BEST Rais wa Marekani Donald Trump ameiondoa nchi yake kutoka kwa mkataba wa nyuklia kati ya Iran na mataifa ya magharibi, Jumanne (08.05.2018) akisema atavifufua tena vikwazo. Trump alisema mkataba huo umeoza kabisa kuanzia katika shina lake na anatumai kuafikiana makubaliano na Korea Kaskazini. Aliueleza mkataba kati ya Iran na nchi za Magharibi kuwa mbaya na unaoegemea upande mmoja. Kauli ya Trump imekuja wakati alipotangaza mipango ya kuiondoa Marekani kutoka mkataba huo wa kihistoria na Iran wa mwaka 2015 wakati wa hotuba aliyoitoa kupitia televisheni katika ikulu ya mjini Washington. Trump alisema kama angeuruhusu mkataba huo kuendelea kuwepo, kungetokea katika siku chache zijazo mashindano ya silaza hza nyuklia. Pia alisema mkataba wa maana ungeeweza kuafikiwa wakati huo, lakini hilo halikufanyika. Rais huyo wa Marekani ameieleza Iran kuwa "utawala wa ugaidi mkubwa". Trump amesema Wairan wanastahili serikali bora zaidi kuliko ile iliyopo...

Fahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa

Nchi nyingi barani Afrika ni kinyume cha sheria kulima, kuuza au kutumia bangi Lesotho Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho. Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini. Afrika Kusini Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa. Tangu mwezi machi mwaka 2017, baada ya mahakama kuu ya Western Cape kuhalalisha matumizi ya bangi majumbani bado matumizi yake ni kinyume cha sheria, mpaka pale sheria itakapobadilish...