Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla
Viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana eneo lenye ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili.
Mkutano huo ndio wa pili kati ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un.
Unafanyika wakati pande hizo zinaendelea na jitihada za kuufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Korea Kaskazini na Kusini.
Siku ya Alhamisi Rais wa Marekani Donald Trump alifuta mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni lakini baadaye akasema kuwa unaweza kufanyika,
Mazungumzo hayo yalifanyika upande wa Korea Kaskazini katika kijiji kinachojulikana kama Panmunjom.
Bw Moon atatangaza matokeo ya mkutano huo siku ya Jumapili asubuhi.
Mazungumzo kati ya Bw Trump na Kim ikiwa yatafanyika yatajikita zaidi katika kuondolewa silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea na kumaliza misukosuko
Maoni