Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MESSI

Ronaldo amchana Messi, amtaka abadilike

Nyota wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo ameibuka na kumzungumzia nyota wa Barcelona, Lionel Messi akisema angependa kumuona mchezaji huyo akicheza katika ligi kuu nchini Italia 'Serie A'. Cristiano Ronaldo na Lionel Messi Cristiano Ronaldo amemhimiza mpinzani wake huyo wa muda mrefu Lionel Messi, akimtaka  "kukubali changamoto" na kumfuata nchini Italia. Alipoulizwa kama anamuhitaji Messi au la!, Ronaldo amesema, " hapana, labda yeye ndiyo ananihitaji mimi. Nimecheza Ureno, Uingereza, Hispania, Italia na kwenye timu ya taifa pia, lakini yeye bado yuko kwenye timu moja. Labda yeye kama ananihitaji mimi ". " Kwangu mimi maisha ni changamoto, ninapenda hivyo na ninapenda kuwafanya watu wangu wawe na furaha. Ningependa siku moja nayeye aje kucheza Italia kama nilivyofanya mimi, akubali changamoto, lakini kama ana furaha pale alipo ninaheshimu uamuzi wake ", ameongeza Ronaldo. Aidha Cristiano amemzungumzia Messi kama ni mchezaji mkubwa...