Maxim Dadashev alipigwa vibaya na Subriel Matias Ijumaa Dadashev alishinda mapambano yake 13 kabla ya kupigwa Ijumaa Bondia raia wa Urusi Maxim Dadashev ameaga dunia baada ya pambano lake na Subriel Matias kumsababishia majeraha makubwa ya ubongo. Dadashev mwenye miaka 28, alishindwa kutembea mwenyewe baada ya pambano hilo ambalo mkufunzi wake Buddy McGirt alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali bila majibu. Pambano hilo lilipigwa Ijumaa wiki iliyopita. Na punde tu baada ya pambano Dadashev alikimbizwa hospitali. Madaktari waligundua kuwa damu ilikuwa ikimvuja kwenye ubongo na kufanyiwa upasuaji wa haraka, lakini akafikwa na umauti jana Jumanne. Shirikisho la ndondi la Urusi limesema tayari uchunguzi umeshafuguliwa juu ya mkasa huo. Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Umar Kremlev amedai kuwa kulikuwa na "aina fulani ya uvunjwaji wa taratibu", na kuongeza kuwa: "Tumempoteza Maxim Dadashev. Ilikuwa ni nyota y...