Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya KOREA KASKAZINI VS MAREKANI

Marekani yalipiza kisasi dhidi ya Urusi kuhusu mkataba wa nyuklia

Marekani yalipiza kisasi dhidi ya Urusi kuhusu mkataba wa nyuklia Ndege B-2 Inauwezo wa nyuklia huko Palmdale, California, 2014. Washington imeamua kuacha kushiriki data kwenye safu yake ya ushambuliaji, ikitoa mfano wa kusimamishwa kwa Moscow kwa mpango mpya wa START Marekani itaacha kupeana taarifa zinazohitajika chini ya mkataba wa mwisho uliosalia wa Washington wa silaha za nyuklia na Urusi kulipiza kisasi uamuzi wa Moscow mapema mwaka huu wa kusimamisha ushiriki katika makubaliano hayo huku kukiwa na mvutano kuhusu mzozo wa Ukraine. "Marekani imepitisha hatua halali za kukabiliana na Shirikisho la Urusi ukiukaji unaoendelea wa Mkataba Mpya wa KUANZA," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken alisema katika taarifa siku ya Alhamisi. Alidai kwamba kusimamishwa kwa Urusi kwa mkataba huo "ni batili kisheria" na kwamba Moscow ilisalia kuwa chini ya majukumu yake chini ya makubaliano. Hata hivyo, Washington itapunguza ahadi zake chini ya mkataba wa 2010, ...

NATO inaingia Asia - Korea Kaskazini

DPRK ilikashifu mipango ya Tokyo ya kufungua ofisi ya kwanza ya mawasiliano yenye makao yake makuu Asia kwa kambi ya kijeshi inayoongozwa na Marekani. Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imedai NATO inataka kuongeza ushawishi wake barani Asia, ikitaja kuongezeka kwa "ushirikiano wa kijeshi" na Japan, ambayo ilikuwa mwenyeji wa ujumbe kutoka kwa muungano wa kijeshi mwezi uliopita kujadili njia za kuongeza ushirikiano. Katika maoni yaliyotolewa na Shirika la Habari la Serikali la Korea (KCNA) siku ya Jumatatu, afisa wa Kituo cha Utafiti cha Wizara ya Mambo ya Nje cha Japan, Kim Seol-hwa, alisema Washington inasukuma hatua kwa hatua NATO kuingia Asia kupitia ushirikiano na mataifa yenye nguvu za kikanda. "Ni siri iliyo wazi kwamba Marekani ... imekuwa ikijaribu kuunda muungano wa kijeshi kama huu katika eneo la Asia-Pasifiki," alisema, akiongeza kwamba "mapambano ya kijeshi ambayo hayajawahi kutokea kati ya Japan na NATO yanazua wasiwasi mkubwa na tahadhari....

KOREA KASKAZINI YA TOA ONYO KALI KWA KOREA KUSINI

Korea Kaskazini yatoa onyo kwa Korea Kusini kwamba ni vigumu kujilinda dhidi ya kombora lake jipya Korea kaskzini ilirusha makombora yake mawili katika bahari ya Japan Korea Kaskazini imetaja majaribio ya makombora yake mapya siku ya Alhamisi kuwa onyo rasmi dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchokozi wa Korea Kusini. Kombora hilo la masafa mafupi lilirushwa katika bahari ya Japan , pia ikijulikana kama bahari ya magharibi kutoka Wonsan katika pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini. Kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un alisema kuwa taifa lake lililazimika kuunda silaha ili kukabiliana na tishio la moja ka moja. Amesema kuwa jaribio hilo lilishirikisha mfumo wa kiufundi wa kuelekeza makombora. Matamshi ya bwana Kim yalioripotiwa katika vyombo vya habari yanajiri baada ya Korea Kaskazini kukosoa uamuzi wa Korea Kusini na Marekani kushiriki katika zoezi la pamoja la kijeshi mwezi ujao. Korea Kaskazini imetaja zoezi hilo la kijeshi kama maandalizi ya kulivamia taifa hilo. Ijapokuwa ...

Rais wa Syria Bashar al- Assad kutembelea Korea Kaskazini

Kauli ya Assad imeripotiwa kutolewa a;ipokutana na Balozi mpya wa Korea Kaskazini nchini Syria Rais wa Syria, Bashar al-Assad anapanga kutembelea nchini Korea Kaskazini,Shirika la Habari la Korea Kaskazini limeeleza. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un kuhodhi ziara ya Kiongozi wa nchi tangu alipoingia marakani mwaka 2011 Hivi karibuni amekuwa na shughuli nyingi za kidiplomasia, kukutana na Rais wa China mwezi Mei na anatarajiwa kuhudhuria mkutano na Donald Trump mwezi huu Syria, mshirika wa Korea Kaskazini, haijasema lolote kuhusu mpango huo unaoripotiwa. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishutumiwa kushirikiana katika mapngo wa kutumia silaha za kemikali.Lakini nchi hizi zimekana shutuma hizo Tarehe ya ziara hiyo haijawekwa wazina vyombo vya Korea Kaskazini. Vilimnukuu bwana Assad siku ya Jumatano akisema ''ninakwenda kutembelea Korea Kaskazini na kukutana na Kim Jong-un." Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi...

Mkutano wa Singapore bado utafanyika Juni

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ataondoa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea na kuhudhuria mkutano wa Singapore Juni 12 wa kukutana  na Rais wa Marekani Donald Trump. Katika mkutano wa ghafla wa Jumamosi, Moon na Kim wamekubaliana kwamba mkutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini lazima ufanyike, kama Moon alivyosema katika mkutano wake na waandishi habari, mjini Seoul. "Mimi na mwenyekiti Kim tumekubaliana kwamba mkutano wa kilele wa Juni 12 lazima ufanyike kwa ufanisi, na jitihada yetu ya kupatikana rasi ya Korea isiyo na silaha za nyuklia, na utawala wa amani wa kudumu haipaswi kusimamishwa," amesema Moon. Rais wa Marekani Donald Trump kwa upande wake ameashiria kwamba maandalizi ya mkutano wa kilele wa Juni 12 yanaendelea, licha ya kuufuta mkutano huo wiki iliyopita. Mkutano huo kati ya viongozi wa Korea mbili ni mabadiliko ya hivi karibuni, katika wiki iliyogubikwa na misukosuko ya kidiplomasia kuhusi...

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla

Viongozi wa Korea wafanya mkutano wa ghafla Viongozi wa Korea Kaskazini na Kusini wamekutana eneo lenye ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huo ndio wa pili kati ya rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un. Unafanyika wakati pande hizo zinaendelea na jitihada za kuufanikisha mkutano wa kihistoria kati ya Korea Kaskazini na Kusini. Siku ya Alhamisi Rais wa Marekani Donald Trump alifuta mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 12 mwezi Juni lakini baadaye akasema kuwa unaweza kufanyika, Mazungumzo hayo yalifanyika upande wa Korea Kaskazini katika kijiji kinachojulikana kama Panmunjom. Bw Moon atatangaza matokeo ya mkutano huo siku ya Jumapili asubuhi. Mazungumzo kati ya Bw Trump na Kim ikiwa yatafanyika yatajikita zaidi katika kuondolewa silaha za nyuklia kutoka rasi ya Korea na kumaliza misukosuko

Trump asema Korea Kaskazini imetoa majibu ya "ukarimu", "ufanisi"

Rais Donald Trump Rais Donald Trump amesema Ijumaa asubuhi kuwa Korea Kaskazini imetoa mrejesho wa “ukarimu” na “ufanisi" baada ya kusitisha mkutano wake na Kim Jong Un. “Ni habari nzuri sana kupokea kauli ya mrejesho ya upole na ufanisi kutoka Korea Kaskazini,” Trump amesema katika ujumbe wa Twitter Ijumaa asubuhi. “Hivi karibuni tutafahamu kile kitakachoendelea, ni matumaini yangu itakuwa ni utajiri na amani ya kudumu na ya muda mrefu. Ni wakati peke yake (na kipaji) utatuthibitishia hili. Korea Kaskazini imesema Ijumaa bado iko tayari kufanya mazungumzo na Marekani” wakati wowote, [katika] mpangilio wowote.” Makamu Waziri wa Mambo ya Nje Kim Kye Gwan, mwakilishi katika mazungumzo ya nyuklia wa muda mrefu na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu, amesema katika tamko lililotangazwa na shirika la habari la serikali la Korea Kaskazini iko “tayari kuipa Marekani muda na fursa” kufikiria suala la mazungumzo. Trump alijitoa ...

Korea Kaskazini yasema iko tayari kuzungumza na Marekani

Korea Kaskazini yasema bado ipo tayari kuzungumza na Marekani hata baada ya rais Donald Trump kuuvunja mkutano huo wa kilele kati yake na Kim Jong Un. Rais Trump alieleza hapo jana kwamba hatakutana na Kim Jong Un na sababu aliyoitoa ni kuwepo mazingira ya ghadhabu na uhasama wa wazi. Naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Kim Kye Gwan amesema nchi yake imesikitishwa na uamuzi huo wa Marekani. Mkutano huo ulionekana kama fursa ya kihistoria kwa Marekani kuweza kuishawishi Korea Kaskazini kuacha mpango wake wa silaha za nyuklia na siku ya Alhamisi, waandishi wa habari wa kimataifa walishuhudia Korea Kaskazini ilipokifunga kituo chake kikuu cha kufanyia majaribio ya nyuklia. Wakati Korea Kaskazini ilipotoa kauli kali dhidi ya makamu wa rais wa Marekani Mike Pence na mshauri wa masuala ya usalama wa Rais Trump, John Bolton, kauli hiyo ndio ilikuwa sababu ya Trump kuuvunja mkutano huo wa kilele kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un. Kiongoz...

Korea Kaskazini yamuita 'mjinga' Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence

Korea Kaskazini yamuita Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence 'mjinga' Afisa wa cheo cha juu wa Korea Kaskazini amemlaumu Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence kwa kuwa "mjinga" na kuonya kuwa kutakuwa na maonyeshano ya ubabe wa nyuklia ikiwa mazungumzo yatafeli. Choe Son-hui alisema Pyongyang haitaweza kuibembeleza Marekani kwa mazungumzo. Siku za hivi karibuni pande hizo mbili zimeonya kuwa mkutano wa Juni 12 unaweza kuharishwa au kufutwa kabisa. Korea Kaskazini ilisema itafikiria tena iwapo itahudhuria mkutano ikiwa Marekani itaendelea kusisitiza kuwa iachane na mpango wa silaha za nyuklia. Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumanne alisema Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo. Choe Son-hui amehusika kwenye mazungumzo mara kadha na Marekani kwa karibu miaka kumi iliyopita. Silaha za nyuklia zimekuwa ajenda kuu kwa miaka mingi kwa Korea Kaskazini Alimuita Mike Pence mjinga kwa kuifananisha Korea...

Kim Jong-un atishia kufuta mkutano wake na Trump

Korea Kaskazini imesema huenda ikaufuta mkutano kati ya kiongozi wake Kim Jong-un na Rais wa Marekani Donald Trump iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kwamba taifa hilo la bara Asia ni lazima liharibu au kusalimisha silaha zake za nyuklia. Mkutano huo ambao umesubiriwa kwa hamu kati ya Bw Trump na Bw Kim unatarajiwa kufanyika mnamo 12 Juni. Hayo yamejiri baada ya Korea Kaskazini kusema imejitolea kuhakikisha silaha za nyuklia zinaondolewa katika rasi ya Korea. Maandalizi ya mkutano huo wa Trump-Kim yamekuwa yakiendeleza, lakini sasa kumeingia shaka kuhusu hilo. Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA limemnukuu naibu waziri wa mambo ya nje Kim Kye-gwan akisema iwapo Marekani "itatubana na kusisitiza kwamba ni lazima tusalimishe bila masharti silaha zetu za nyuklia basi hatutakuwa tena na hamu ya kushiriki mazungumzo hayo na itatulazimu kutafakari upya iwapo tutakubali mkutano unaotarajiwa kufanyika karibuni kati ya DPRK-US. Korea Kaskazini kir...

Korea Kaskazini imewaacha huru raia watatu wa Marekani

MTEULE THE BEST Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Mike Pompeo, mwanadiplomasia wa Marekani alikutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini Korea Kaskazini imewaachia huru raia watatu wa marekani kutoka gerezani, ukurasa wa tweeter wa Rais wa Marekani Donald Trump umeeleza. hatua hiyo inaonekana kama dalili njema kuelekea mkutano wa kihistoria kati ya Rais Trump na mwenzie wa Korea Kaskazini Kim Jong-un. Bwana Trump amesema atawakaribisha watu hao watakaporejea na waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo ambaye amekuwa mjini Pyongyang kufanya maandalizi ya mazungumzo hayo. Kim Hak-song, Tony Kim and Kim Dong-chul walikuwa kifungoni baada ya kukutwa na hatia ya kufanya vitendo viovu dhidi ya serikali. Rais Trump ametangaza kuachiwa kwao siku ya Jumatano. Ruka ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump ''Afya yao inaonekana kuwa nzuri'', aliandika pia tarehe na mahali ambapo mazungumzo yatafanyika Haki mili...

Marekani yajiondoa mkataba wa nyuklia na Iran

MTEULE THE BEST Rais wa Marekani Donald Trump ameiondoa nchi yake kutoka kwa mkataba wa nyuklia kati ya Iran na mataifa ya magharibi, Jumanne (08.05.2018) akisema atavifufua tena vikwazo. Trump alisema mkataba huo umeoza kabisa kuanzia katika shina lake na anatumai kuafikiana makubaliano na Korea Kaskazini. Aliueleza mkataba kati ya Iran na nchi za Magharibi kuwa mbaya na unaoegemea upande mmoja. Kauli ya Trump imekuja wakati alipotangaza mipango ya kuiondoa Marekani kutoka mkataba huo wa kihistoria na Iran wa mwaka 2015 wakati wa hotuba aliyoitoa kupitia televisheni katika ikulu ya mjini Washington. Trump alisema kama angeuruhusu mkataba huo kuendelea kuwepo, kungetokea katika siku chache zijazo mashindano ya silaza hza nyuklia. Pia alisema mkataba wa maana ungeeweza kuafikiwa wakati huo, lakini hilo halikufanyika. Rais huyo wa Marekani ameieleza Iran kuwa "utawala wa ugaidi mkubwa". Trump amesema Wairan wanastahili serikali bora zaidi kuliko ile iliyopo...

Kiongozi wa Korea Kaskazini avuka mpaka na kuingia Korea Kusini

Rais w a Korea kaskazini Kim jong un na mwenzake wa Kusini Moon Jae-in Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kuingia Korea Kusini kwa kuvuka mstari wa kijeshi uliowekwa kugawanya mataifa hayo mawili tangu vita vya Korea 1953. Katika hatua ilioshangiliwa kwa mbwembwe za kila aina kiongozi wa Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kaskazini walisalimiana kwa mikono katika mpaka huo. Bwana Kim alisema kuwa anatumai kwamba kutakuwa na mazungumzo ya kufana baada ya ufunguzi mzuri wakati mazungumzo hayo yalipoanza. Mkutano huo wa kihistoria utaangazia maswala ya silaha za kinyuklia na uwezekano wa makubaliano ya amani. Mengi yatakayozungumzwa ni mambo ambayo tayari yameafikiwa awali lakini wachanganuzi wengi bado wana wasiwasi kuhusu uaminifu wa Korea Kaskazini katika kukubalia kuacha shughuli ya utengezaji wa silaha za kinyuklia. Hatahivyo shughuli zote za taifa lote la Korea Kusini zilisimama kwa muda ambapo viongozi hao wawili walisalimiana kwa mikono katikati y...

Trump ampongeza mkurugenzi wa CIA Mike Pompeo, kwa ziara yake ya siri huko Korea Kaskazini

Ziara ya bwana Pompeo's (left) nchini Korea Kaskazini ililenga kuandaa mkutano kati ya Trump na Kim Mkurugenzi wa shirika la ujasusi Marekani CIA ,Mike Pompeo ameunda "uhusiano mzuri" na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un walipokutana wiki iliyopita, Rais Trump amesema katika ujumbe wake wa Twitter. Akithibitisha taarifa zilizopo kwenye vyombo vya habari kuhusu mkutano huo wa siri mjini Pyongyang, Trump amesema mkutano ulimalizika "bila ya tashwishi". Ziara hiyo ya kushtukiza inadhihirisha mawasiliano ya kiwango cha juu kati ya Marekani na Korea kaskazini tangu 2000. Rais Donald Trump anatarajiwa kuandaa mkutano na Bwana Kim kufikia mwezi Juni. Bado ratiba inaandaliwa, rais wa Marekani amesema. Mkutano huo ulioandaliwa kuandaa mkutano mwengine kati ya rais Donald Trump na Kim Jong Un ulifanyika wikendi ya sikukuu ya Pasaka. Bwana Trump alikuwa amekiri kufanyika kwa mazungumzo ya hadhi ya juu na Pyongayng. ''Tumekuwa na ma...