Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 17, 2018

Mnangagwa anusurika jaribio la mauaji

Picha za televisheni ya shirika la utangazaji la Zimbabwe zimeonesha mripuko mkubwa kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Rais Emmerson Mnangagwa katika kile kinachotajwa kuwa jaribio la mauaji dhidi yake. Msemaji wake, George Charamba, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba rais huyo mwenye umri wa miaka 75, ambaye kwenye mkutano huo alikuwa ameambatana na makamu wake wawili, yuko salama kwenye ikulu ndogo mjini humo. "Rais ameondoshwa akiwa salama. Yuko kwenye nyumba ya serikali ya Bulawayo. Tunashukuru kwamba ulikuwa ni mripuko, na kwa hakika ulitokezea karibu sana na jukwaa kuu," alisema Charamba. Shahidi mmoja ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba mripuko ulitokea muda mchache baada ya Mnangagwa kumaliza hotuba yake na wakati akiondoka jukwaani. Picha zilizotumwa mitandaoni zinamuonesha kiongozi huyo akiwapungia mkono wafuasi wake, akinyanyua hatua kuondoka jukwaani na kuanza kutembea kutoka meza kuu, ambapo sekunde...