Mwili wa mtu aliyeabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' waanguka London ''Mtu'' huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi Jumapili mchana Mwili wa mtu anayeshukiwa kuabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' umeanguka ndege hiyo ikielekea kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London. Mwili huo - unaoaminiwa kuwa wa mwanamume - ulipatikana umeanguka katika bustani ya Clapham siku ya Jumapili. Polisi wanasema mtu huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi. Mkoba, maji na vyakula vilipatikana katika eneo lililo chini ya gia ya ndege wakati ilipokua ikutua. Polisi wa wa jiji la London wamesema mwili huo utafanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake na kwamba kifo chake. Kenya Airways imesema kuwa ndege hiyo imefanyiwa uchunguzi na hakuna hitilefu yoyote ilioripotiwa. Msemaji wa shirika la ndege hiyo amesem...