Ruka hadi kwenye maudhui makuu

NDEGE YA KENYA YA DODOSHA ABIRIA UINGEREZA

Mwili wa mtu aliyeabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' waanguka London

''Mtu'' huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi Jumapili mchana

Mwili wa mtu anayeshukiwa kuabiri ndege ya Kenya Airways kisiri 'stowaway' umeanguka ndege hiyo ikielekea kutua katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London.

Mwili huo - unaoaminiwa kuwa wa mwanamume - ulipatikana umeanguka katika bustani ya Clapham siku ya Jumapili.

Polisi wanasema mtu huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi.

Mkoba, maji na vyakula vilipatikana katika eneo lililo chini ya gia ya ndege wakati ilipokua ikutua.

Polisi wa wa jiji la London wamesema mwili huo utafanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake na kwamba kifo chake.

Kenya Airways imesema kuwa ndege hiyo imefanyiwa uchunguzi na hakuna hitilefu yoyote ilioripotiwa.

Msemaji wa shirika la ndege hiyo amesema: "Ndege hii huchukua saa 8 na dakika 50 kukamilisha safari yake. Inasikitisha kuwa mtu alipoteza uhai wake baada ya kuingia ndege yetu kisiri.

"Kenya Airways inashirikiana na mamlaka husika mjini Nairobi na London katika uchunguzi wa tukio hili."

Sio mara ya kwanza kifo kama hiki kimeripotiwa katika ndege inayoelekea uwanja wa Kimataifa wa Heathrow.

Mwezi Juni mwaka 2015, mtu mmoja alipatikana akiwa amefariki katika paa la makao makuu ya Notonthehighstreet.com katika barabara ya Kew Road, Richmond, huku mwingine akipatikana katika hali mahututi baada ya kuning'inia katika ndege ya British Airways kutoka mjini Johannesburg.

Mwezi Agosti mwaka 2012, mwili wa mwanamume ulipatikana kwenye buti ya ndege iliyokuwa ikitoka mjini Cape Town Afrika Kusini, ilipotua katika uwanja wa Kimataifa wa Heathrow

DOMAINImage caption''Mtu'' huyo alianguka kutoka kwenye ndege ya Kenya Airways iliyokuwa ikisafiri kutoka mjini Nairobi Jumapili mchana

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

*DKT. MAGUFULI, MNANGAGWA WAWEKA HISTORIA MPYA*

Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Zimbabwe, Emerson Mnangagwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wameweka historia mpya kwa kukubaliana kushirikiana kwenye maeneo makuu matatu yenye tija pande zote. *Kwanza*, *Kuimarisha uchumi* wa nchi hizi mbili kwa kukuza uwekezaji na biashara ambao umeanza kuonesha matunda makubwa. Mathalani, katika eneo la biashara kumeonyesha mafanikio makubwa kila mwaka. Mfano mwaka 2016 biashara kati ya Tanzania na Zimbabwe ilikuwa ni Tsh. Bilioni 18.3. Mwaka 2017 biashara ilikuwa Tsh. Bilioni 21.1. *Pili*; *kushirikiana* vyema kwenye masuala ya *utalii* kwa kutumia wingi wa vivutio vya utalii kama vile mbuga za wanyama, fukwe, maeneo ya kihistoria pamoja na Mlima Kilimanjaro. *Tatu*; Kushirikiana na kuimarisha eneo la *huduma za kijamii* zikiwemo afya, utamaduni, elimu na kukuza lugha ya kiswahili ambapo Tanzania ina Waalimu wa kutosha na hivyo...

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...