Marubani wanafunzi wa Afrika Kusini, waliotengeneza ndege aina ya Sling 4, wamewasili Kilimanjaro,Tanzania, wakiwa njiani kuelekea kwenye kituo chao cha mwisho, jijini Cairo.
Timu ya wanafunzi hao waliondoka Zanzibar siku ya Jumapili, baada ya kutumia siku kadhaa bila mafanikio kuzungumza na mamlaka za nchini Kenya ili waweze kutua jijini Nairobi.
''Mamlaka nchini Kenya wamesema hawajafurahishwa na njia zetu hivyo wakatuzuia kuingia,'' alisema kiongozi wa wanafunzi hao, Des Werner, Baba wa Megan Werner 17, mwanzilishi waU-Dream Global.
''Tunaweza kubadili njia lakini hatuna muda wa kufanya hivyo.Tunafikiri kama ni wagumu tusilazimishe kwenda. Hata hivyo ni nchi yao ndio inayokosa nafasi ya vijana wa nchini kwao kuzungumza na timu yetu kwa ajili ya kuwapa msukumo vijana wa nchini mwao.''
Ndege iliyotengenezwa na wanafunzi yatua Zanzibar
Wanafunzi kuendesha ndege kutoka Afrika Kusini mpaka Misri
Marubani hao wataelekea Uganda siku ya Jumanne lakini bado wanasubiri kibali cha kuruka mpaka Addis Ababa, safari ambayo iko kwenye mipango yao.
''Kidogo tuko nyuma ya ratiba lakini tutafanikisha.Kama mambo yakiwa sawa tunatarajia kuwa Cairo tarehe 7 mwezi Julai,'' ameeleza bwana Werner.
Wanafunzi hao wanaendesha ndege mbili aina ya sling 4 yenye viti vinne, ndege moja inayorushwa na marubani wadogo ambao wamekuwa wakibadilishana tangu walipotoka Cape Town tarehe 15 mwezi Juni na nyingine iliyoendeshwa na timu ya watu wenye uzoefu.
Bwana Werene, amesema timu yake wako na ari na kuwa hali ya safari kwa ujumla ni nzuri.
Ndege ilitengenezwa vipi?
Wanafunzi hao waliitengeneza ndege hiyo katika kipindi cha wiki tatu, wakiunganisha vifaa vilivyonunulia kwenye kampuni moja nchini Afrika Kusini.
"Nikiiangalia hii ndege, huwa ninaona fahari ya hali ya juu kwa kile nilichokifanya. Siamini kile tulichokifanya. Ninaiona kama mtoto wangu. Ninamtukuza mtoto (ndege)," ameeleza Agnes Keamogetswe Seemela, msichana kutoka katika jimbo la Gauteng mwenye umri wa miaka 15.
"Inapaa uzuri kabisa, na ukiwa juu, mwonekano wa chini ni mzuri kweli," ameeleza kulingana na safari ya kwanza ya ndege hiyo kutoka jiji la Johannesburg mpaka Cape Town, kabla ya kuanza safari ya Misri.
"Nilishiriki katika kuunda eneo la kti la ndege hiyo pamoja na mabawa yake."
Safari inaendelea
Vituo ambavyo ndege hiyo itasimama kutoka Afrika Kusini mpaka Misri.
Kitua cha kwanza cha safari hiyo ni mji wa kusini katika pwani ya Namibia wa Luderitz, na tayari wameshatua huko.
Ndege hiyo ina uwezo wa kupaa angani kwa muda wa saa sita na nusu, na itakuwa na vituo kadhaa katika nchi za Zimbabwe, Malawi, Tanzania, Kenya, Ethipia na Eritrea kabla ya kufika Misri.
Katika safari ya kurudi, watatumia njia tofauti na watasimama katika nchi za Uganda, Rwanda, Zambia na Botswana.
Kutakuwa na ndege nyengine aina ya Sling 4 pkwa ajili ya usaidizi.
Marubani hao wanafunzi wanapanga kuzungumza na wanafunzi wenzao katika nchi zote ambazo watasimama.
"Ni kitu kizuri kuona ni kwa namna gani watu wanavutia na kushawishika na kile ambacho tumefanya," amesema rubani Megan
Maoni