Mpiga picha za wanayamapori amepiga picha ya Ndege mmoja aliyekuwa akilisha kinda wake kipande cha sigara kilichobaki baada ya kutumika, katika ufukwe mjini Florida nchini Marekani.
Katika ukurasa wa Facebook, Karen Mason amesema aliwaona ndege hao mwezi uliopita.
Alisema: ''kama utavuta sigara, tafadhali usiache mabaki ya sigara.''
Taasisi ya kutunza mazingira ya hifadhi nchini Uingereza imesema picha hiyo ''inasikitisha''.
Bi Mason alipiga picha nyingine ya kinda akiwa amebeba kipande cha mabaki ya sigara mdomo wake:
KAREN MASON
Ndege hufanya makosa kuwalisha makinda vipande vya sigara kwa kudhani ni chakula.
''Ndege wengi wana shauku kuhusu vitu ambavyo tunavitupa, na mara nyingi huchunguza kwa kuvijaribu ili kujua kama ni chakula au la,'' msemaji wa taasisi ya kulinda ndege aliiambia BBC.
''inasikitisha, mzazi huyu ameamua kuwa mabaki ya sigara kuwa kitu cha kumlisha kinda wake.
''Viumbe hawa wanajaribu kuendana na vitu tunavyofanya duniani; kila mwaka, tunaona wanyama wengi wakinasa, wakijeruhiwa na hata kufa kutokana na vitu vinavyosababishwa na binaadamu.Huwa tunawaona wanatumia takataka kutengeneza viota vyao.
''Kwa bahati mbaya kwa watu wengi, takataka zinaonekana kama hazina madhara, lakini hufanya eneo kuwa chafu; hatahivyo, picha za kusikitisha zikionyesha madhara ya takataka kwa viumbe.''
Vichujio vya sigara vinatengenezwa kwa nyuzi nyuzi za plastiki,hivyo huchukua miaka kuoza kwenye mazingira.
Mabaki ya sigara ni miongoni mwa aina ya takataka zinazokusanywa kwa wingi kwenye fukwe za bahari duniani, kwa mujibu wa wanaharakati wa mazingira.
Maoni