Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 17, 2016

Watu 20 wauwa kwenye mlipuko nchini Afghanistan

MTEULE THE BEST Image copyright EPA Wizara ya afya ya Afghanistan imesema takriban watu ishirini wameuawa na zaidi ya wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga lililofanyika kwenye mji mkuu Kabul. Baadhi ya taarifa zinasema kulikuwa na milipuko miwili. Shambulio hilo linaonyesha kuwa lililenga maandamano ya maelfu ya watu kutoka jamii ndogo ya Hazara, ambao hujikuta wakidhalilishwa na kufanyiwa ukatili. Walikuwa wakiandamana kupinga mpango wa serikali wa kuhamisha umeme kutoka kwenye majimbo yao katikati ya nchi.

Moyes ajiunga na Sunderland

MTEULE THE BEST David Moyes apata kazi Sunderland. Atachukua nafasi yake aliyekuwa meneja wa klabu hiyo Sam Allardyce David Moyes amebahatika kupata nafasi hiyo baada ya Sam Allardyce kuchaguliwa kuwa msimamizi wa timu ya kitaifa ya Uingereza. Moyes mwenye umri wa miaka 53, na aliyewahi kuwa meneja wa Manchester United na vilevile Everton amepata mkataba huo mpya wa miaka minne. Moyes anasema anafurahi kupata kazi na club hiyo kubwa ya Uingereza na anatazamia kwa hamu kurudi tena kufanya kazi katika ligi kuu ya Uingereza Premier League. Utakumbuka jinsi alivyolazimika kuihama Premier League wakati alipofutwa kazi kutokana na kutopata matokeo mazuri baada ya kuchukua uongozi wa Manchester United kutoka kwa Sir Alex Ferguson aliyekuwa anastaafu baada ya msimu wa mafanikio mazuri wa ushindi wa vikombe kadhaa katika mdaa wa miaka 26 huko Old Trafford.

Wakimbizi wamuokoa mwanasiasa Ujerumani

MTEULE THE BEST Mwanasiasa kutoka chama cha mrengo wa kulia cha Ujerumani ameokolewa baada na wakimbizi baada ya gari lake kugonga mti, zimeeleza ripoti za vyombo vya habari vya Ujerumani. Raia wawili wa Syria walitoa huduma ya kwanza kwa mwasiasa huyo wa chama cha National Democratic Party (NPD) Stefan Jagsch ambae aliejeruhiwakatika ajali katika jimbo la Hesse , liliarifu shirika la habari la DPA. Image copyright GETTY Image caption Wafuasi wa chama cha NPD wamekua wakishiriki maandamano ya kupinga wahamiaji Inasemekana wakimbizi hao waliokua wakipita karibu na ajali hiyo walikua wameondoka polisi walipowasili kwenmye tukio. Wanasiasa wa chama hicho cha NPD wamekua wakishiriki katika mfulurizo wa maandamano ya kupinga wahamiaji nchini Ujerumani. Hata hivyo afisa wa kikanda wa NPD Jean Christoph Fiedler aliwasifu wakimbizi hao wawili kwa ''kitendo hicho kizuri sana cha kibinadamu'', liliripoti gazeti la Frankfurter Rundschau. Mahakama ya katiba ya Uj...

JERAHA LA HISIA SEHEMU YA PILI

MTEULE THE BEST RIWAYA: JERAHA LA HISIA MTUNZI: George Iron Mosenya SEHEMU YA PILI Japokuwa alikuwa mtoto safari ya kwenda Uganda kwake ilikuwa mwisho wa kucheza na Naomi wake,hakupata hata fursa ya kumwambia kwaheri. Walter aliumia sana na hakuwa na la kufanya akafuata maelekezo aliyope "Bye da Maureen" Walter alimwaga dada yake ambaye alikuwa hatambui lolote lile pale alipo akili yake haikuwa vizuri tena,alikuwa ni mtu wa kukaa tuu,haongei bali anaunguruma,hacheki bali kupiga kelele hayo ndiyo maisha yake yalivyokuwa na elimu yake ya kidato cha tatu ikaishia hapo katika hali ya kusikitisha. Maureen hakujibu kitu Frank akamshika mkono Walter wakaondoka wakimwacha Maureen na msaidizi wa kazi pale ndani. * * * * Basi la Akamba liliwasili jijini Kampala nchini Uganda majira ya saa tano asubuhi siku iliyofuata Muga alikuwepo kituo cha mabasi kuwapokea wageni wake hao wawili. Frank na Walter "Saluuut!!" "Saluuut!!" walipeana salamu maswahiba...

JERAHA LA HISIA SEHEMU YA KWANZA

MTEULE THE BEST RIWAYA: JERAHA LA HISIA MTUNZI: George Iron Mosenya SEHEMU YA KWANZA "Kwa nini hutaki kusahau tabia yako ya kale,kwanini unanitesa hivi, unanifadhaisha,tazama jamii inavyoniangalia kwa jicho baya la kinafiki na dharau ndani yake, kumbuka kwamba hukuzaliwa ukiwa na tabia mbaya kama hii, ni kitu gani sikupi Naomi wangu eeh!!, ni wakati gani unanihitaji na usinione, huko unapoenda wanakupa nini kikubwa hicho niambie kama ni uhai wangu uchukue basi, niambie Naomi usiogope, jamii inaamini nimepotea njia lakini ni wewe macho yamekuona na moyo ukakupokea kikamilifu bila wasiwasi wowote,sasa kwa nini unitese hivi kwa nini unafurahia mimi kulia kila wakati, unapata raha kiasi gani kulewa na kuja nyumbani usiku, mbona hauheshimu pete yako hapo kidoleni, wewe ni mke wa mtu Naomi tambua hilo jaribu kusahau maisha yako ya zamani mpenzi wangu, nakupenda sana unajua, nafanya kazi kwa bidii kwa sababu yako na watoto wetu tutakaowazaa sina mama sina baba wewe ndiye...

SITAISAHAU FACEBOOK sehemu ya nne

MTEULE THE BEST SIMULIZI:SEHEMU YA NNE SITAISAHAU FACEBOOK Nilikuwa makini katika kulikanyaga lile zulia jekundu, sikutaka kuonekana mshamba katika hilo. Nilijilazimisha kutembea mwendo wa kilimbwende wakati niliamini kuwa iwapo nitathubutu kuingia katika mashindano ya ulimbwende basi nitashika nafasi ya mwisho ama sitapata walau kigezo cha kusimama jukwaani kama mlimbwende. Maana nilikuwa cha ufupi na nilikuwa na dalili ya kuwa kibonge. Niliongozwa hadi katika chumba kikubwa sana, kila kitu pale ndani kilikuwa cheupe kasoro ngozi yangu ambayo ilifanya kama uchafu pale ndani. Sikujali!!! “Utalala hapa ndani…na hawa watakuhudumia.” Nilipewa wakinamama wawili kwa ajili ya kunihudumia. Umri wao sidhani kama unatofauti sana na wa mwalimu Nchimbi yule mama yangu mzazi. Lakini matabasamu yao ni kama walikuwa na miaka kumi na nane. Ungekuwa wewe ungejisikiaje. Mwenzako nilijisikia kama malkia. Nilipata huduma zote za msingi hadi nilipopitiwa na usingizi na kuamka siku iliyofuata....

SITAISAHAU FACEBOOK SEHEMU YA TATU

MTEULE THE BEST Simulizi sehemu ya tatu SITAHISAHAU FACEBOOK Mchomo wa wivu ukanishambulia na kunijeruhi moyoni, nikaanza kuhisi zile ndoto zangu zimeanza kufifishwa. Happy alinisalimia akiwa na tabasamu mwanana. Dokta akiungana naye kutabasamu. Nami nikajilazimisha nikatabasamu!!! “Kesho nitarejea nyumbani mara moja….kuna dharula imejitokeza. Lakini kitu kimoja nahitaji mfanikiwe kupitia mimi.” Alianza kutueleza dokta, tukiwa ndani ya gari la kukodi. Kisha akaendelea, “Nitarejea hivi punde tu!! Na nikiwa huko nitakuwa nawasaidia, msisite kunieleza lolote nami nitawasaidia, hata mimi kufika hapa nilikuwa nasaidiwa kwa hiyo ni zamu yangu kusaidia.” Aliongea kwa ukarimu mkubwa. Kwa mahesabu ya harakaharaka zile dola thamani yake ilikuwa milioni sita za kitanzania. Hizo ndizo Dokta alituachia tugawane. Kwangu mimi ilikuwa kama ndoto ya mchana!!! Siku iliyofuata dokta huyu wa ajabu akarejea huko anapojua yeye!! Hakutaka kusindikizwa uwanja wa ndege. **** Ile hali ya kumsh...

SITAISAHAU FACEBOOK SEHEMU YA PILI

MTEULE THE BEST simulizi sehemu ya pili SITASAHAU FACEBOOK   Baada ya dakika mbili nilikuwa nimemaliza kuusoma ujumbe mrefu wa Dokta Davis. Nilikuwa natetemeka, mapigo ya moyo yalikuwa katika mwendokasi wa kutisha sana. Macho yalikuwa hayafumbi bali yanaitazama simu yangu!!! Nilikuwa simuoni Dokta Davis lakini nilikuwa katika TAHARUKI!!!!! SIKUAMINI!!!!! *Ni kitu gani Isabella amekisoma hadi kumtisha hivyo… **Je ni biashara gani hiyo ya mtandao. *** Na kipi kilimsibu Isabellla baadaye!!!! ENDELEA. Kilichonishangaza zaidi ni faida iliyoandikwa na Dokta Davis. Sikuipinga lakini mtaji wake haukuonekana kabisa, swali likawa ni biashara gani hii isiyohitaji mtaji lakini ina faida kubwa kiasi hichi?? Nilitaka kumuuliza lakini nikakumbuka kuwa tayari aliita biashara ya mtandao. Shida zilizokuwa zikinikabili sikutegemea kuwa naweza kumruhusu roho wa kukataa anitawale. Mara moja nikakubaliana na Davis kuwa naweza kuifanya biashara ya mtandao. Sikutaka hata ...

SITAISAHAU FACEBOOK

MTEULE THE BEST SIMULIZI: sehemu ya kwanza SITAISAHAU FACEBOOK “Isabela….Isabela…” nilisikia sauti ya mwanamke ikiniita, niligeuka mara moja maana sauti ile ni kama niliwahi kuisikia mahali. Lakini sikukumbuka ni wapi. Giza totoro lilinizuia kuweza kumtambua mtu yule aliyeniita kwa ufasaha kiasi kile tena gizani. Nilianza kujiuliza iwapo nirejee nyuma kurudi kumtafuta ama niendelee mbele ambako pia sikuwa na uhakika ni wapi. Manyunyu ya mvua yalikuwa yamenilowanisha hasa na nguo yangu ilikuwa imeshikana na mwili. Nilikuwa natetemeka huku michubuko kadhaa katika mwili wangu ikiniwashawasha. Kilikuwa kitendawili aidha niende mbele ama nirudi nyuma kuifatiliza hiyo sauti. Ile hali ya kujiuliza niende mbele ama nirudi nyuma ikanifanya niwe kama naigiza igizo lisilokuwa rasmi. “Isabelaaaa!!!.” Iliita tena sauti hii. Sasa ilisikika dhahiri kuwa sauti ile ilikuwa katika kulia, mwenye sauti ile alikuwa katika uchungu mkubwa na bila shaka aliuhitaji sana msaada wangu. Nilitamani ...