MTEULE THE BEST
RIWAYA: JERAHA LA HISIA
MTUNZI: George Iron Mosenya
SEHEMU YA KWANZA
"Kwa nini hutaki kusahau tabia yako ya kale,kwanini unanitesa hivi, unanifadhaisha,tazama jamii inavyoniangalia kwa jicho baya la kinafiki na dharau ndani yake, kumbuka kwamba hukuzaliwa ukiwa na tabia mbaya kama hii, ni kitu gani sikupi Naomi wangu eeh!!, ni wakati gani unanihitaji na usinione, huko unapoenda wanakupa nini kikubwa hicho niambie kama ni uhai wangu uchukue basi, niambie Naomi usiogope, jamii inaamini nimepotea njia lakini ni wewe macho yamekuona na moyo ukakupokea kikamilifu bila wasiwasi wowote,sasa kwa nini unitese hivi kwa nini unafurahia mimi kulia kila wakati, unapata raha kiasi gani kulewa na kuja nyumbani usiku, mbona hauheshimu pete yako hapo kidoleni, wewe ni mke wa mtu Naomi tambua hilo jaribu kusahau maisha yako ya zamani mpenzi wangu, nakupenda sana unajua, nafanya kazi kwa bidii kwa sababu yako na watoto wetu tutakaowazaa sina mama sina baba wewe ndiye baba na mama yangu katika hii dunia nipende japo kidogo tu hata kwa kujilazimisha Naomi na taratibu utazoea na utanipenda, na hata siku moja sitajisikia aibu kuwa na wewe" Yalikuwa maneno makali yaliyojaa simanzi kutoka kwa kijana Walter ama Dj kama wengi walivyomzoea, kwenda kwa mke wake wa ndoa Naomi Holela huku machozi yakimtoka kwa wingi sana, ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mkewe (Naomi). Ukumbi ulikuwa kimya, ni sauti hii pekee iliyopasua anga na kuyafikia masikio ya mwanamke ambaye hakushangazwa na maneno yale. Labda kwa sababu haikuwa mara ya kwanza kuyasikia ama la alikuwa hamuelewi mumewe. Hakuna aliyejua.
Naomi alikuwa amefika eneo la tukio katika ukumbi wa New Afrikasana majira ya saa saba usiku tofauti na saa mbili kama alivyotarajiwa, pale ukumbini ambapo mwanzoni walikuwepo wageni waalikwa wapatao sitini sasa alikuwa amebaki Walter na mlinzi wa ukumbi huo,Walter alimpokea Naomi kama mgeni wa heshima sana pale ukumbini kama mtu aliyekuja katika wakati muafaka, Naomi tayari alikuwa amelewa chakari jambo hilo Walter hakulijali alichofurahia ni kumuona Naomi machoni pake tena.
"Nipeleke nyumbani nikalale" ndilo jibu alilotoa Naomi baada ya kuyasikiliza maneno mengi ya Walter, maneno ambayo yalikuwa kama ngonjera zisizokuwa na mvuto mbele yake, wakati huo mlinzi ndio alikuwa amegeuzwa 'camera man' ukumbi ulikuwa umepooza sana.
"Kula basi japo keki kidogo halafu uzime mishumaa malkia wangu. Fanya hivyo kwa ajiri yangu nakuomba" alibembeleza Dj, kwa sauti tulivu sana.
"Na bia ziko wapi, panga hapo bia 28 ninywe nimalize ndio miaka yangu hiyo" alijibu Naomi na kumfadhaisha sana Dj.
“Naomi.” Aliita Walter kisha akaendelea, “hata uninyanyase vipi mimi nakupenda" alijikuta akijibu kwa ghadhabu kiasi flani kijana huyu ambaye pesa haikuwa na thamani kwake bali upendo kwa binti huyu.

Pesa yote ya maandalizi aliyotumia Walter kwa ajili ya Naomi ambaye ni mke wake aliyekuwa anasheherekea kutimiza miaka ishirini na nane (28), ikawa imepotelea hewani na hata dakika moja hakukumbuka kuiwaza wakati amemshika bega Naomi wakitoka ukumbini pale. Alikuwa na amani tele kila awapo na mwanamke huyu ambaye aliichukiza jamii nayo jamii ikamchukia haswaa. Lakini kasoro mwanaume mmoja tu. Walter.
Huyu alimpenda vile alivyo. Hakujali.
"Naomi unajua unapendwa sana na watu mke wangu, yaani walikuwa wamekuja wageni zaidi ya mia moja kwenye sherehe yako na wengine walikuwa wanazidi kumiminika, unapendwa mke wangu hadi nimeona wivu" Walter alimpamba mkewe na sifa za uongo ili mradi tu apate kumfurahisha na kujiona yeye ni mtu fulani katika jamii. Sasa walikuwa wanaliendea gari waweze kuondoka
"Wamekuja hao wote kunishangaa mimi?"Aliuliza Naomi kama mtu ambaye ameguswa.
"Ndio mke wangu! Yaani wote kwa ajili yako, nakwambia nimesikia wivu natamani ningependwa hivyo mimi"
"Waambie hivi waende kushangaa makaburini maiti anapandwa lakini haoti wasinishangae mimi bwana na kama ningewakuta ningewaeleza kwa mdomo wangu, ushamba tu!!" alijibu kwa jeuri na nyodo kitu ambacho Dj hakukitegemea lakini alicheka kuonyesha kuwa hajakwazika hata kidogo, moyoni alihisi ametekenywa na kitu kilichokuwa na ladha mbaya inayokera, harufu kali ya pombe nayo ilimuumiza kwa sababu hakuwa mtumiaji lakini hata hakuziba pua wala kukunja sura alitabasamu muda wote hadi wanafika nyumbani.
Kama mtoto mdogo vile Naomi alivuliwa nguo, viatu, heleni,wigi alilokuwa amevaa, bangili pamoja na kucha za bandia akiwa hoi kitandani.
Kisha Dj akajiweka pembeni yake wakalala.
"Naamini ni huyu uliyenichagulia na ni mimi wa kuishi nae sijapotea njia na kama nimepotea nirekebishe baba" aliomba ombi fupi kisha akaivuta shuka kajifunika na kuanza kuutafuta usingizi.
Hatimaye akalala.
Naomi alikuwa anakoroma!!!

* * * *
Miaka 18 iliyopita ndio ilikuwa mara yao ya kwanza na ya mwisho kuwa pamoja kabla ya kukutana tena ukubwani walipowekeana uchumba na hatimaye ndoa.
Familia zao zilikuwa hazifanani lakini wao walifanana, Naomi alikuwa anatoka familia ya kimaskini sana huku Walter akiwa anatokea kwa matajiri.
Walter alizoea sana kucheza na Naomi hata wazazi wake walitambua hilo, alikuwepo dada yake lakini Naomi ndiye alikuwa mambo yote hasa hasa kutokana na kulandana kiumri. Walter na Naomi walikuwa wakiachana miaka miwili
Alichokula Walter kikabaki alihifadhi kwa ajili ya Naomi, iwe biskuti, sambusa, Piza, na chochote kile alichodhani na Naomi kitampendeza.
Hakuna mtoto wa uswahilini aliyeruhusiwa kupenya geti la akina Walter tofauti na Naomi mtoto wa fundi baiskeli mzee Holela na mama mchoma vitumbua Mama Mashimi. Ilikuwa kama bahati kwa mtoto huyu wa kimaskini kupata nafasi hiyo ya kipekee, nafasi ya kwenda kuwatishia wenzake mtaani juu ya ufahari wa hali ya juu katika nyumba hiyo iliyokuwa maeneo ya Magomeni jijini Dar es salaam.
Wazazi wake Walter Bwana Andrew na Bi. Magreth walikuwa na hofu ya mtoto wao kufundishwa tabia mbaya ndio maana hawakutaka achangamane na watoto wa kimaskini, walijaribu kwa kila hali kuzuia hilo lakini juhudi na upendo aliokuwa nao bibi yake Walter kwa mjukuu wake huyo ulizidi amri za wazazi wake.
"Mwacheni mke wa mjukuu wangu tena msimkasirishe mume wangu kabisa asije akaniacha!!" ndivyo ajuza huyu wa miaka 70 alivyojenga mazoea makubwa ya wawili hawa, michezo yote ya uswahilini asiyoijua Walter alifundishwa na Naomi kivitendo kombolela, ukuti wa mnazi, kidali po, kujipikilisha na hatimaye kibaba na mama, alipata raha sana Walter kwa uwepo wa Naomi. Alijisikia fahari kujifunza matukio yanayotokea nje ya geti. Mambo yanayotokea katika dunia nyingine ambayo ni tofauti yao.

** * *
Ajali mbaya ya gari iliyotokea Tinde karibu kabisa na mji wa Kahama ilihusisha vifo vya watu watatu palepale.
Ilikuwa sio ajali ya kutupia jicho mara mbili, gari dogo lililokuwa linaingia barabarani linakutana uso kwa uso na lori kubwa aina ya Scania likiwa limepotea njia na kuiviringisha chini ya uvungu wake, ilikuwa vigumu kuamini kuwa gari ndogo aina ya starlet ilikuwa mpya mwezi mmoja uliopita.
Haikuhitaji kutumia taaluma uliyojifunza darasani kuweza kupata jibu kwamba wahusika ndani ya gari dogo tayari ni maiti kwa jinsi gari yao ilivyopondwa pondwa, ingekuwa ni filamu wangeweza kupona lakini kwa hali halisi kile ni kifo, mwendesha baiskeli aliyegongwa na lile lori alifahamika haraka kwa sababu alirushwa pembezoni mwa barabara na kutua juu ya jiwe alipopoteza maisha palepale bila kutoa hata neno moja la kutangaza urithi wa hiyo baiskeli iliyopona. Na wale waliokuwa ndani ya gari dogo hawakuwa na lolote la kusema, hawakupata muda wa kuhadithia maumivu waliyoyapata kabla ya kukata roho. Mashahidi pekee walikuwa ni wale wamiliki wa gari kubwa, hao ndio wangeweza kuigiza vilio vya uchungu vilivyotolewa na wahusika chini ya uvungu kabla ya mauti kuwachukua lakini hata wao hawakuwa na la kusema kwani walikuwa katika harakati za kumkwepa Israel asizitwae roho zao.
Simulizi ya safari hiyo ikabadilika, ghafla ikawa ya kuvutia mashabiki wakaongezeka barabarani kuja kuwa mashahidi wa nini kimetokea, hapakuwa na kingilio kutazama tukio hili lililotokea majira ya jioni.

* * *
Maandalizi ya safari yao hayakuwa makubwa sana, waliamini ilikuwa safari fupi ya kwenda leo na kurudi baada ya siku mbili, hawakuaga watu wengi tofauti na familia yao na hawakupata fursa ya kumuaga mtoto wao mdogo (Walter) kwani muda huo alikuwa bize anacheza michezo ya kitoto na rafiki yake.
Walikuwa ni Bw. na Bibi Andrew wazazi wa Walter, katika safari yao ya kwenda mji wa Kahama wilayani Shinyanga ambapo Bw. Andrew alikuwa anaenda kwa dhumuni la kuchukua ruhusa kazini kwake 'Kahama Gold Mines' ruhusa ya wiki mbili ambapo alitarajia kusafiri yeye na familia yake kwenda Moshi alipozaliwa kwa mapumziko mafupi na kuwasabahi wazazi wake.
Safari ya kwenda ilikuwa ndefu na yenye furaha mtu na mume wake walipiga domo mwanzo hadi mwisho wa safari mama Maureen ndiye alikuwa muongeaji mkuu baba Maureen akawa anafuatisha, aidha kwa kucheka, kuguna au kutikisa kichwa, lakini safari yao ya kurudi ilikuwa fupi lakini ndefu sana kwani licha ya gari yao kuishia kwenye tairi za Scania huo haukuwa mwisho wa safari wao walisafiri zaidi hadi mbinguni na kusema kwaheri katika uso wa dunia. Wakawa wamewahi kupanga foleni ya masisha mengine.
Zawadi walizokuwa wamewachukulia watoto wao, zikachanganyikana na damu zao pamoja na vipande vya mabati ya gari halafu wakaungana na petroli iliyokuwa imesalia katika tangi lililokuwa limepasuka.
Bwana na bibi Andrew wakaishia kuwa chakula cha barabara.
Miili yao ilibondeka vibaya lakini gari waliyokuwa wanatumia ndio iliwawezesha wanausalama kutambua wahusika wa ajali hiyo.
Taarifa kama upepo zikasambaa nchini kote kupitia vyombo vya habari na katika jumba la marehemu zilifika haraka sana, mtoto wao mkubwa (Maureen) ndiye alipokea simu ya mezani taarifa aliyopewa iliupasua moyo wake kwa mshtuko mkali ambao bibi yake aliutambua pale alipomwona anaachia mkonga wa simu unaanguka chini
"Umekuwaje we mtoto" bibi yake alimuuliza
"Baba na mama wametutoka" alijibu Maureen huku akiwa amesahau kuwa bibi yake ana presha ya kushuka, wakati anazidi kuishiwa nguvu akidhani bibi yake ndiye atamdaka, palepale bibi kama mtu mwenye mapepo alidondoka kwenye vigae pale sebuleni huku kisogo kikitangulia, Maureen alishuhudia damu ilivyotapakaa pale sebuleni lakini mwili haukuwa na nguvu hata chembe, kiungo pekee kilichofanya kazi ni macho.
Bibi, baba ,na mama ndani ya masaa machache wametoweka duniani.
Ni kwa mwanadamu gani anaweza kukabiliana na huzuni hii!!!
Walter kama kawaida shule wakiwa wamefunga basi mida yote yeye na Naomi, Naomi na yeye.
"Nikalete Juisi tunywe eti mama!" Walter alimwambia Naomi walipokuwa wakicheza kibaba na mama, Naomi kwa ishara ya kutikisa kichwa alikubali, Walter ambaye katika mchezo huo alikuwa baba akaondoka kwenda sebuleni.
Japokuwa alikuwa mtoto mdogo alijua maana ya damu aliyoishuhudia kutoka kwa bibi yake na hali aliyokuwa nayo dada yake (Maureen), filamu kadhaa alizokuwa amewahi kuangalia ziliamsha hisia ya uoga.
"Naomiiiii" alipiga kelele kuu, ndani ya dakika moja Naomi akawa amewasili tayari eneo lile
"Mamaaa" naye akapiga kelele mbiombio mtoto wa Kiswahili akaenda nje ambapo alimweleza mlinzi wa getini kilichotokea, sigara aliyokuwa nayo mdomoni ikaanguka naye bila kujibu kitu akatimua mbio kuingia ndani, alichoambiwa ndio hicho kilichokuwa kinatokea kweli sebuleni, alimkuta Walter anamtikisa dada yake huku akilitaja jina lake kwa sauti ya kukata tamaa.
Kwa bibi mlinzi hakuwa na sababu ya kusubiri daktari ampime ndo aujue ukweli, kwani tayari alikuwa maiti swali lilibakia kwa Maureen aliyekuwa amekodoa macho lakini haongei lolote lile.
Mlinzi alijaribu kupiga simu zote za mabosi wake lakini hazikupatikana katu. Akiwa hana hata senti tano mfukoni baada ya kutoa shilingi mia aliyokuwa nayo kununua sigara, mlinzi alihisi kuchanganyikiwa akili, breki za gari zikiambatana na honi kali zilirejesha matumaini, akatambua kuwa ni bosi wake amekuja.
Mungu wangu sijui namuelezaje!!! Aliwaza mlinzi kabla ya kwenda mlangoni.
“Atakuwa ni nani huyo??” Mlinzi alimuuliza Naomi, lakini hakusubiri jibu kwani aliamini alikuwa amekosea kuuliza.
Tofauti na alivyodhani kuwa huyo alikuwa ni bosi wake. La hakuwa yeye alikuwa mtu mgeni sana machoni pake, aliingia mbiombio bila hata kukaribishwa.
"Shkamoo bamdogo"Alisalimia Walter lakini hakupata jibu bwana yule tayari alikuwa amembeba juu juu Maureen na kumpakiza kwenye gari kisha akataka kuondoka mlinzi akaweka ngumu.
"Huyo ni bamdogo Frank" Walter akamwambia.
Huyo alikuwa ni mdogo wake bwana Andrew, ambaye ubize wake nje ya nchi ulisababisha yeye na kaka yake waonane ofisini na zaidi ya hapo kwa njia ya simu.
Madhara ya Sayansi na teknolojia!!!

Mshtuko alioupata Maureen kushuhudia bibi yake akikata roho na taarifa ya vifo vya wazazi wake wote wawili ilimsababishia matatizo makubwa ya akili ambayo daktari aliyaita mtindio wa ubongo. Dalili za kupona zilikuwepo japo kwa taratibu sana. Daktari hakuweza kutoa wakati sahihi bali aliwatia moyo ndugu hawa wa mgonjwa.
Wakiwa hawana ndugu mwingine Tanzania Maureen na Walter walichukuliwa na Frank ambaye ni mdogo wake baba yao, ni huyu ambaye alipewa taarifa mapema kwa njia ya simu kutokea eneo la tukio, namba yake pamoja na ile ya nyumbani zilikuwa baadhi ya namba zilizohifadhiwa katika kijitabu cha kumbukumbu cha bwana Andrew.
Maisha ya Tanzania yalisababisha Walter kuwakumbuka wazazi wake kila siku hali ya dada yake pia ilichangia kumfadhaisha mtoto huyu. Maziko ya watu watatu muhimu katika maisha yake, yaani Bibi, Baba na mama lilikuwa tatizo kubwa sana.
Makaburi ya Kinondoni yakawa yamemeza miili hii mitatu kwa pamoja.
Mama mkwe, mkwelima wake pamoja na mwanae wa kumzaa.
Kila mwenye damu na moyo wa nyama alitikiswa na tukio hili. Kilio cha kitoto japo chenye uchungu mkubwa kutoka kwa Walter kiliwaliza kina mama wengi, huku Maureen na mtindio wa Ubongo aliokuwa ameupata ukiamsha hisia kali.
Frank akawa ameubeba rasmi kwa moyo mmoja mzigo huu!!

*****
Kwa kutumia busara zake Frank aliamua kumtafutia Walter shule nchini Uganda na kumkabidhi kwa rafiki yake aliyeitwa Muganyizi ama kwa kifupi Muga ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kuandaa muziki, aliishi peke yake kwenye nyumba yake baada ya mkewe kuuawa kwenye vurugu za uchaguzi nchi jirani ya Kenya.
Hakuwa na kipingamizi cha kukaa na mtoto Walter alichofanya ni kumtafuta binti atakayekuwa anamhudumia Walter kwani yeye mara kwa mara alikuwa anabanwa na shughuli zake ambazo hazikuwa na siku maalum.
Japokuwa alikuwa mtoto safari ya kwenda Uganda kwake ilikuwa mwisho wa kucheza na Naomi wake, hakupata hata fursa ya kumwambia kwaheri rafiki huyu wa dhati na hata angemwambia je angemwambia ni wapi anaenda??
Walter aliumia sana na hakuwa na la kufanya akafuata maelekezo aliyopewa na baba yake huyo.
"Bye da Maureen" Walter alimwaga dada yake ambaye alikuwa hatambui lolote lile pale alipo akili yake haikuwa vizuri tena, alikuwa ni mtu wa kukaa tuu, haongei bali anaunguruma, hacheki bali kupiga kelele hayo ndiyo maisha yake yalivyokuwa na elimu yake ya kidato cha tatu ikaishia hapo katika hali ya kusikitisha. Maureen akawa ameurudia utoto akawa mtu wa kuhudumiwa kwa kila kitu!!
Maureen hakujibu kitu Frank akamshika mkono Walter wakaondoka wakimwacha Maureen na msaidizi wa kazi pale ndani.

***MAISHA hubadilika ghafla…..hakuna haja ya kujisifia kwa kufika leo badala yake mpe sifa muumba wako….
WALTER anatakiwa kuiacha ardhi aliyoizoea ya Tanzania na kutakiwa kuishi Uganda, dada yake ambaye waliishi wote kwa furaha..sasa ana utindio wa ubongo na eleimu yake ya kidato cha tatu imeishia hapohapo.
***BABA, MAMA, BIBI kutoweka duniani inaumiza sana kwa hakika…….
YOTE haya ni katika simulizi hii ya mapenzi….JERAHA LA HISIA itaendelea>>>>

Maoni