Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya EGYPT

Tanzania yatia saini ujenzi wa mradi wa umeme unaopigiwa kelele na wanamazingira, Rais Magufuli asema ni mradi wa lazima kwa maendeleo

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Stigler's Gorge ni jambo la lazima. Leo rais wa nchi hiyo John Magufuli ameweka saini na wakandarasi wa mradi huo kutoka Misri wakiwa pamoja na waziri mkuu wa nchi yao. Hatua hiyo inakuja baada ya miaka 40 tangu utafiti wa uzalishaji wa umeme kutoka mto Rufiji ambao unaweza kuzalisha megawati 2,100 kufanyika wakati huo Tanzania ikiongozwa na Mwalimu Julius Nyerere. Mradi huu unatarajiwa kutekelezwa na fedha za watanzania wenyewe kwa kiwango cha dola za kimarekani bilioni 2.9 ambayo ni sawa na takribani shilingi trilion 6.5 za kitanzania. Na kampuni itakayofanya kazi hiyo inatoka Misri. Rais Magufuli amesema kwamba walitumia muda kutafakari kuhusu mradi huu kwa sababu Tanzania imebarikiwa na vyanzo vingi sana vya uzalishaji umeme kama vile maji,gesi asilia,upepo,joto ardhi ,makaa ya mawe pamoja na madini ya urani. Na kufikia uamuzi huo wal...

Misri watoa ripoti ya Salah kuhusu Kombe la Dunia

Baada ya jana Mohamed Salah kuumia kwenye mchezo wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Real Madrid na Liverpool, Daktari wa timu ya taifa ya Misri Dkt. Mohammed Abu Ola amesema nyota huyo ana nafasi kubwa ya kucheza Kombe la Dunia. Dkt. Abu Ola amesema baada ya mchezo aliwasiliana na daktari wa timu ya Liverpool na kumweleza kuwa picha za mionzi (X-ray) zimeonesha bega la Salah limeteguka kwenye mfupa mdogo na matibabu yalianza haraka ili aweze kupona kwa wakati. Kwa mujibu wa Dkt. Abu Ola na daktari wa Liverpool Salah atakuwepo kwenye fainali za Kombe la Dunia. Salah aliumizwa na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos na kutolewa dakika ya 31 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo ambapo timu hizo zilikuwa bado hazijafungana.  Baada ya Salah kutoka Real Madrid walifanikiwa kushinda kipindi cha pili kwa mabao 3-1 na kutwaa ubingwa wa 13 na wa taatu mfululizo chini ya kocha Zinedine Zidane ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo. Mabao ya Real Madrid yalifungwa ...