Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo Jumatatu Julai 8 limetangaza kusitisha mkataba na kocha Emmanuel Amunike. Taarifa fupi iliyotolewa na TFF inadai kuwa Amunike amekubaliana na TFF kusitisha mkataba huo. Shirikisho hilo pia limesema pia litatangaza Kocha wa muda atakaekiongoza Kikosi cha Timu ya Taifa kwa mechi za CHAN. "Makocha wa muda watatangazwa baada ya Kamati ya Dharura ya Kamati ya Utendaji (Emergency Committee) itakapokutana Julai 11,2019," inasema taarifa ya TFF. Mchakato wa kutafuta Kocha mpya umeanza mara moja. Amunike alipewa kibarua cha kuinoa Tanzania maarufu kama Taifa Stars mwezi Aprili 2018. Atabakia kwenye historia ya mpira Tanzania kwa kuingoza nchi hiyo kufuzu kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya miaka 39. Kabla ya hapo alinyanyua Kombe la Dunia 2015 akiwa kocha wa timu ya vijana wa chini ya miaka 17 Nigeria. Kocha hu...