Noti za Tanzania Benki Kuu ya Tanzania imezipiga benki tano marufuku ya kuendesha biashara ya sarafu za kigeni kwa muda wa mwezi mmoja kwa kukiuka sheria kwa mujibu wa maafisa wa vyeo vya juu. Marufuku hiyo inakuja baada ya Benki Kuu kufanya ukaguzi wa ghafla kwenye maduka ya kubadilisha fedha za kigeni kwenye mji ulio kaskazini wa Arusha kituo cha utalii na bishara ya madini. Kwa sasa kuna zaidi ya benki 40 zinazotoa huduma kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki. Kwa nini zimepigwa marufuku? Benki ya Barclays Tanzania, Exim Bank, UBA Bank, BancABC na Azania Bank zote zilipigwa marufuku ya kuendesha biashara hiyo Novemba 23 kwa kukiuka sheria za biashara, kwa mujibu wa Alexander Ng'winamila, mkurugenzi wa masoko ya fedha katika benki kuu. "Benki zilizopigwa marufuku aidha zilifanya biashara nje ya viwango vya masoko au hazikuwasilisha kwa Benki Kuu rrekodi za biashara zao, suala ambalo ni kinyume na sheria," Ng'winamila aliliambia shirika la Reuters. Barc...