Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya AFD

Berlin: maelfu waunga mkono na kupinga maandamano ya AfD

Wafuasi 5,000 wa  chama mbadala kwa Ujerumani (AfD) wameandamana mjini Berlin Jumapili, lakini idadi hiyo ilikuwa ndogo ikilinganishwa na walioandama kuipinga AfD. Maelfu ya watu wameandamana Jumapili katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin. Ni maandamano yanayohusisha pande mbili tofauti. Upande wa wafuasi wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia kinachojiita chama mbadala kwa Ujerumani AfD, kinachopinga uhamiaji pamoja na Uislamu. Na waandamanaji wanaoipinga AfD wakitumia kauli mbiu ya "Wacha chuki.” Maafisa zaidi wa polisi walishika doria kutenganisha pande hizo mbili za waandamanaji ili kuepusha vurugu. Katika ukurasa wao wa Twitter, idara ya polisi imesema wametumia kemikali ya pilipili ya kutoa machozi kuwazuia waandamanaji wasivunje mpaka uliowekwa kuwatenganisha. Beatrix von Storch, mwanachama muhimu wa AfD, amewaambia wafuasi wapatao 2,000 waliokusanyika katika maandamano hayo kwamba mchezaji soka wa timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil licha ya kuwa na uraia wa Ujerumani ...