Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya DEREVA

Basi la shule latekwa na kuteketezwa Italia

Basi la shule nchini Italia likiwa limeteketea kabisa Basi lililokuwa limebeba watoto wa shule wapatao 51 lilitekwa na dereva wake na kisha kutiwa moto karibu na Milan nchini Italia. Watoto hao wa shule, baadhi yao walifungwa kamba, waliokolewa baada ya kuvunjwa vioo vywa basi hilo upande wa nyuma na hakuna hata mmoja aliyejeruhiwa vibaya.Watu kumi na wanne waliathiriwa na moshi uliotokana na kuteketea kwa basi hilo. Dereva wa basi hilo alikuwa na umri wa miaka arobaini na saba mwenye uraia wa nchini Italia ingawa ana asili ya kutoka nchini Senegal, inaarifiwa kwamba ametiwa nguvuni. Dereva huyo alisikika akitamba, akiwaambia waliokuwemo katika basi hilo kwamba hakuna hata mtu mmoja atakaye nusurika.Ulikuwa ni muujiza, vinginevyo yangekuwa ni mauaji ya halaiki, alinukuliwa akisema hayo mwendesha mashtaa mkuu wa mjini Milan, Francesco Greco. Mwalimu mmoja wapo alikuwa ndani ya basi wakati tukio hilo likitekelezwa, alimuelezea mtuhumiwa huyo kuwa alikuwa na silika ya hasira mar...

Chadema watoa taarifa kuhusu Jeshi la Polisi kumshikilia dereva wa Mbowe

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimelalamikia hatua ya  Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumshikilia kwa siku mbili  mtumishi wao Williard Urassa.  Urassa ambaye ni dereva wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikamatwa jana nje ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.  Taarifa iliyotolewa leo, Novemba 24, 2018 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imeeleza tangu Urassa alipokamatwa na polisi, jeshi hilo limekataa kumpatia dhamana huku likizuia mtu yeyote kuonana naye.  Hii ndio Taarifa kamili:   Kwa siku ya pili leo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Ndugu Williard Urassa, ambaye ni mtumishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Makao Makuu, bila kueleza sababu za kumshikilia, huku pia akinyimwa haki zake za msingi, kinyume cha sheria za nchi.  Ndugu Urassa ambaye ni Dereva wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, alikamatwa jana nje ya chumba cha Mahakama y...