: Pogba, Badiashile, Lukaku, Haller, Koscielny, Dias, De Ligt Manchester United wameongeza dau la £30m juu ya thamani ya kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 26, na sasa wanataka dau la £180m kumuuza mchezaji huyo waliyemnunua kwa dau la £89m in 2016.(Star) Juventus wamesitisha hamu yao ya kutaka kumsajili Pogba, wakitoa fursa kwa Real Madrid kumsaini mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mail) Manchester United huenda ikamsajili beki wa Monaco na Ufaransa 19 Benoit Badiashile,ambaye pia anawaniwa na Wolves - iwapo watamkosa beki a leicester na Uingereza Harry Maguire, 26. (L'Equipe, via Express) Inter Milan huenda wakalazimika kulipa takriban £90m ili kuweza kuwa na fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji na Man United Romelu Lukaku, 26, msimu huu (Telegraph) Arsenal itataka kulipwa dau la £8.8m ili kumuuza nahodha wake na beki wa Ufaransa Laurent Koscielny, 33 ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo na alikataa kuondoka na wenzake kuelekea Marekani kwa ...