Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 13.07.2019

: Pogba, Badiashile, Lukaku, Haller, Koscielny, Dias, De Ligt



Manchester United wameongeza dau la Ā£30m juu ya thamani ya kiungo wa Ufaransa Paul Pogba, 26, na sasa wanataka dau la Ā£180m kumuuza mchezaji huyo waliyemnunua kwa dau la Ā£89m in 2016.(Star)


Juventus wamesitisha hamu yao ya kutaka kumsajili Pogba, wakitoa fursa kwa Real Madrid kumsaini mchezaji huyo wa Ufaransa. (Mail)

Manchester United huenda ikamsajili beki wa Monaco na Ufaransa 19 Benoit Badiashile,ambaye pia anawaniwa na Wolves - iwapo watamkosa beki a leicester na Uingereza Harry Maguire, 26. (L'Equipe, via Express)



Inter Milan huenda wakalazimika kulipa takriban Ā£90m ili kuweza kuwa na fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji na Man United Romelu Lukaku, 26, msimu huu (Telegraph)

Arsenal itataka kulipwa dau la Ā£8.8m ili kumuuza nahodha wake na beki wa Ufaransa Laurent Koscielny, 33 ambaye anataka kuondoka katika klabu hiyo na alikataa kuondoka na wenzake kuelekea Marekani kwa mechi za maandilizi ya msimu ujao. (London Evening Standard)

Arsenal imeimarisha hamu yake ya kumsaini beki wa Benfica na Ureno Ruben Dias, 22, kufautia maamuzi ya hivi karibuni yaKoscielny . (Mail)

West Ham infanya mazungumzo na Eintracht Frankfurt over a deal to sign 25-year-old French striker Sebastian Haller for around Ā£40m. (Sky Sports)

Mshambulaji wa Manchester United na Jamhuri ya Ireland Mipo Odubeko, 16, ambaye aliifungia magoli 35 shule yake ya mafunzo ya soka msimu uliopita amekataa kuongeza kandarasi mpya.. (Mail)

Juventus imekubali dau la Ā£63m kumnunua beki wa Ajax na Uholanzi Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 19. (De Telegraaf - in Dutch)


West Ham wametaka kulipwa kitita cha Ā£10m ili kumsajiuli kiungo wa kati wa Equatorial Guinea Pedro Obiang, 27, licha ya klabu za Itali kama vile Bologna na Sassuolo kuonyesha hamu ya kumnunua mchezaji huyo. (Sun)

Tottenham inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Leeds na Uingereza Kalvin Phillips, ambaye klabu hiyo ya York Shire inasema ana thamani ya Ā£30m. (Mirror)

Manchester United bado ina hamu ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle na Uingereza Sean Longstaff kutoka Newcastle licha ya klabu hiyo kutokubaliana juu thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)

Lakini bei ya Newcastle ya Ā£50m inaweza kuilazimu United kumaliza hamu yao.. (ESPN

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAPENZI: Kuna faida na ni muhimu Mpenzi wako kuwa rafiki yako pia

Kuna faida kubwa kwa wapenzi kuwa marafiki KUTOKANA na mila mbalimbali, baadhi ya watu wamekuwa wakiamini kwamba mwanamke ni daraja la pili. Daraja la kwanza na lenye kuthaminiwa ni mwanaume. Yaani mwanamke hana kauli kwa mwanaume. Anakuwa kama mtumwa fulani hivi.  Mwanaume akiongea, basi ni maelekezo kama vile rais wa nchi anavyotoa maelekezo kwa watu walio chini yake. Hakuna wa kupinga. Akisema sitaki kitu fulani kifanyike, basi ni mpaka atakapotoa maelekezo mengine. Vinginevyo, maelekezo ya awali yatabaki kusimama kama sheria.  Wapo baadhi ya wanawake wanaofurahia aina hii ya uhusiano kwa sababu ya mazoea. Kwamba wamekuzwa hivyo, mwanaume ni mwanaume. Huu ni mfumo ambao watu wengi wamekuwa wakiuishi. Kuna ambao wanakubaliana nao, wengine hawakubaliani nao.  Watu wengi sana wamekuwa wakiishi katika malumbano katika mahusiano yao kutokana na mfumo huu wa maisha. Mwanamke hataki kuishi kama mtumwa, mume anakomaa kuonesha uanaume wake. Hakuna anayekubali kushuka,...

Urusi: Vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitafua dafu

MTEULE THE BEST Image caption Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov na mwenzeka wa Marekani Rex Tillerson Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov amemwambia waziri wa ulinzi nchini Marekani Rex Tillerson kwamba kuiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini hakutafua dafu. Taarifa iliochapishwa na wizara ya kigeni nchini Urusi inasema kuwa wawili hao walizungumza kwa njia ya simu na kushutumu majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliotekelezwa na Pyongyang . Lakini inasema kuwa bwana Lavrov alisisitiza kwamba diplomasia ndio njia ya pekee ya kumaliza wasiwasi katika rasi ya Korea, na kutaka hatua zozote dhidi ya taifa hilo kusitishwa akionya huenda zikasababisha madhara yasiojulikana. Waziri wa ulinzi nchini Marekani amesisitiza kuwa bado kuna fursa ya kidiplomasia katika kukabiliana na Korea Kaskazini. Mapema rais Trump alichapisha ujumbe katika akaunti yake ya Twitter akisema mazungumzo sio suluhisho.

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania

Fuvu la binadamu wa kale liligunduliwa miaka 60 iliyopita nchini Tanzania Miaka 60 siku kama ya leo ugunduzi mkubwa ulifanyika katika eneo la Olduvai Gorge, kwenye kreta ya Ngorongoro. Wanaakiolojia Louis na Mary Leakey waligundua fuvu la mtu anayeaminika kuwa ni wa kale zaidi waliyompa jina la Zinjanthropus. Ugunduzi huo uliofanyika saa nne asubuhi Julai 22, 1959 kipindi hicho kwenye eneo la Tanganyika ulikuwa wa vipande zaidi ya 100 ukasaidia katika kutambua asili ya watu wa awali duniani. Kabla ya ugunduzi huo, wanasayansi na wanahistoria walikuwa wakiamini kuwa binadamu wa kale walitokea Uchina baada ya ugunduzi wa mafuvu ya kale baina ya 1923 na 1927 nchini humo ya Homo eractus, ama maarufu kama Peking Man. Mafuvu hayo ya Uchina yalikuwa na umri wa takribani miaka 750,000. Mafuvu ya Olduvai eneo ambalo kwa sasa lipo Tanzania wakati wa ugunduzi wake lilikuwa na umri wa takribani miaka milioni 1.75, na hakuna mabaki ya mtu wa kale zaidi ambayo mpaka sasa yamegundul...