Christopher Williams Jr na babake Mtoto wa umri wa miaka miwili nchini Marekani amefariki baada ya kujipiga risasi kichwani kwa bunduki ambayo imekuwa ikihifadhiwa na wazazi wake nyumbani kwao. Polisi wa Houston, Texas wanasema wazazi wa mtoto huyo - Christopher Williams Jr - walikuwa nyumbani wakati wa kutokea kwa kisa hicho. Polisi wanasema bunduki hiyo ambayo hutumia risasi za ukubwa wa 9mm ilipatikana eneo la tukio na kwamba ilikuwa inamilikiwa na babake. Kufikia sasa, bado haijabainika iwapo wazazi wake watashtakiwa. Watoto kadha wamekuwa wakijipiga risasi na kujiua kimakosa nchini Marekani miaka ya karibuni. Polisi wa Houston wamesema wanajaribu kubaini ni vipi mtoto huyo aliyepewa jina la utani "Junior" aliweza kuifikia bunduki hiyo. Mkuu wa kitengo cha waathiriwa maalum katika idara ya polisi ya Houston David Angelo ametoa wito kwa wazazi walio na bunduki kuchukua tahadhari zaidi. "Ni lazima uweke salama silaha, iwe ni kwa kuhakiki...