Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 17, 2019

Mwanamfalme wa Saudia asema hana mpango wa kuinunua klabu Manchester United:

Manchester United: Mwanamfalme wa Saudia asema hana mpango wa kuinunua klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed Bin Salman amekanusha madai kuwa anantaka kuinunua Manchester United kwa kitita cha pauni bilioni 3.8. Tetesi ziliibuka mwishoni mwa wiki zikimuhusisha mwanamfalme huyo na kutaka kuinunua klabu hiyo tajiri nchini Uingereza. Wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazers wanadaiwa kuwa hawana mpango wa kuiuza timu yao. Wamiliki hao kutoka Marekani waliinunua Man United kwa kitita cha pauni milioni 790 mwezi Mei 2005. "Ripoti zinazomuhusisha Mwana Mfalme Mohammed Bin Salman kuwa anataka kuinunua Manchester United ni uongo mtupu," amesema waziri wa michezo wa Saudia Turki al-Shabanah. "Manchester United walifanya mkutano na mfuko wa uwekezaji wa umma PIF wa Saudia kuhusu nafasi ya udhamini. Lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa," ameeleza waziri huyo. Salman, 33, aliteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha ...

KUTANA NA TIMU IYOFUNGWA GOLI 20 JUMAPILI HII

Klabu ya Pro Piacenza yalazwa 20-0 katika mechi ya ligi Serie C Iwapo unadhania timu yako imekuwa na msururu wa matokeo mabaya wikendi hii basi fikiria kichapo hiki walichopewa Pro Piacenza katika ligi ya Itali. Klabu hiyo ya ligi ya Serie C iliowekwa katika kundi A ilishindwa magoli 20-0, ' ndio magoli ishirini bila jibu ' na wapinzani wao katika ligi hiyo Cuneo siku ya Jumapili jioni. Walikuwa nyuma kwa magoli 16 kwa bila wakati wa muda wa mapumziko huku mshambuliaji wa Cuneo Hicham Kanis akifunga magoli sita pekee kabla ya mapumziko naye mshambuliaji mwenza Eduardo Defendi akipata magili matano. Katika safu ya ulinzi ya Pro Piacenza kulikuwa na matatizo yaliosababisha mvua hiyo ya magoli. Wakiwa chini katika ligi hiyo ya tatu ya Itali, klabu hiyo ya kaskazini ina matatizo makubwa ya ufadhili. Walipokonywa pointi nane mapema katika kampeni yao na wameripotiwa kushindwa kuwalipa wachezaji wao tangu mwezi Agosti hatua iliosababisha kujiuzulu kwa wachezaji wengi wa ki...