Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya LIBYA

Amana Kubwa ya Mafuta na Gesi Yagunduliwa Afrika Kaskazini

 Wakala wa Jiolojia wa Marekani (USGS) umetangaza kugundua mabonde mawili makubwa ya mafuta na gesi ambayo yanaenea katika maeneo makubwa ya Libya na Tunisia.  Katika tathmini yake ya kwanza, Mamlaka ya Habari ya Nishati ya Marekani (EIA) ilisema kuwa matokeo ya utafiti huo katika nchi za Afrika yana jumla ya mapipa trilioni 4 ya mafuta na futi za ujazo bilioni 385 za gesi asilia, ambayo ni sawa na mapipa trilioni 1.47 ya gesi asilia iliyotiwa kimiminika.  gesi.  Mnamo 2021, Libya ilikuwa nchi ya saba kwa uzalishaji wa mafuta ghafi ya OPEC na ya tatu kwa ukubwa barani Afrika, kulingana na EIA.  Libya inashikilia 3% ya mafuta duniani - na 39% ya hifadhi ya mafuta iliyothibitishwa ya Afrika.  Wakati huo huo, EIA inakadiria muundo wa Tunisia unashikilia futi za ujazo trilioni 23 za akiba iliyothibitishwa ya gesi ya shale na mapipa bilioni 1.5 ya rasilimali za mafuta ya shale zinazoweza kurejeshwa kitaalamu.

Muungano wa G7 na Umoja wa mataifa walaani mapigano mapya Libya

Vikosi tiifu kwa serikali ya Tripoli vimeripotiwa kuungana na serikali kulinda mji mkuu Mataifa yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani G7, pamoja na Umoja wa mataifa yamelaani vikali mapigano yaliozuka upya nchini Libya. Mataifa hayo yanataka pande zinazohasimiana Libya "kusitisha mara moja shughuli za kijeshi". Baraza kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa wito huo. Tripoli ni makao makuu ya serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa, na ambayo pia inaungwa mkono na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Vikosi vya kulinda usalama vya umoja wa mataifa katika mji huo vimekuwa katika hali ya tahadhari. Ghasia zimekumba Libya tangu utawala kiongozi wa nchi hiyo wa mda mrefu, Muammar Gaddafi kuangushwa na yeye kuuawa mwaka 2011. Nini kinachofanyika ? Kamanda Khalifa Haftar, ambaye ni kiongozi wa vikosi vya kijeshi vinavyopinga utawala wa Tripoli siku ya Alhamisi aliamuru vikosi vyake kuingia mji wa Libya. Hatua hiyo ilijiri wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Ma...

Urusi imeingia rasmi nchini Libya

Mkurugenzi wa idara ya usalama wa jeshi la Urusi(GRU) Luteni Jenerali Igor Segun amwambia waziri mkuu wa Uingereza bi Theresa May kwamba jeshi la Urusi limekwishaingia nchini Libya kwa malengo ya kuimaliza vita inayopiganwa nchini humo takribani miaka saba sasa. Urusi  imekwishafungua ngome zake za kijeshi nchini Libya katika miji ya Tobruk na Benghazi na tayari imekwishafunga mfumo wa ulinzi wa anga(S 300) katika miji hiyo.Luteni Jenerali Igor Segun aongeza kwa kusema kwamba ndani ya muda mfupi tu amani nchini Libya itarejea kama Syria kwani popote liingiapo jeshi la Urusi hakuna linaloshindikana na aitaja Syria kama mfano wa maeneo magumu ambayo wamefanikiwa kuyakomboa.