RC ARUSHA AONYA WAKANDARASI WABABAISHAJI Na Ferdinand Shayo,Arusha. Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo ameonya Wakandarasi wanaofanya ubabaishaji kwenye miradi ya barabara za vijijini Mkoani Arusha kwa kutopewa tenda za serikali na badala yake wachukuliwe hatua za kisheria. Gambo ametangaza marufuku kwa wakandarasi wababaishaji kupewa kandarasi wakati akikabidhi mikataba ya kwa wakandarasi wa wilaya za saba za mkoa wa Arusha ikiwemo Arusha,Meru na Karatu . Aidha amewataka Wakandarasi kuhakikisha kuwa wanakamilisha miradi kwa wakati na kutumia vizuri fedha za walipa kodi na kuepuka kutekeleza miradi chini ya kiwango. Katibu Tawala Wilaya ya Arusha Richard Kwitega amesema kuwa serikali imewapa kipaumbele Wakandarasi wazawa ili waweze kuleta tija kwenye miradi ya Barabara ambazo zitachochea maendeleo ya wananchi. Kaimu Mratibu wa Tarura mkoa wa Arusha Dickson Kanyankole amesema kuwa miradi hiyo itatekelezwa ka...